Kwanini idadi ya Wachina inatarajiwa kupungua

Chanzo cha picha, Chen Fuping / Getty Images
Idadi ya watu nchini China inatarajiwa kupungua kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha njaa kilichotokea miaka 60 iliyopita. Kwa nini? Na hii itaathiri ulimwengu kwa njia gani?
Taifa kubwa zaidi duniani linakaribia kupungua.
China inachukua zaidi ya theluthi moja ya idadi ya watu duniani, lakini baada ya miongo minne ambapo idadi ya watu nchini humo imeongezeka kutoka milioni watu 660 hadi bilioni 1.4, idadi ya watu wake itapungua mwaka huu, kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha njaa chakati ya mwaka 1959-1961.
Kulingana na takwimu za hivi punde kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya China, idadi ya watu nchini humo iliongezeka kutoka bilioni 1.41212 hadi bilioni 1.41260 tu mwaka wa 2021 - ongezeko la chini la watu 480,000 tu, sehemu ndogo ya ukuaji wa kila mwaka wa milioni nane au zaidi muongo mmoja uliopita.
Ingawa kutopata watoto wakati wa hatua kali za kupambana na Covid kunaweza kuchangia kupungua kuzaliwa watoto, hali hii imekuwa ikiashiria kwa miaka.
Kiwango cha jumla cha kuzaliwa watoto nchini Uchinakilikuwa 2.6 mwishoni mwa miaka ya 1980, zaidi ya 2.1 inayohitajika kuchukua nafasi ya vifo. Imekuwa kati ya 1.6 na 1.7 tangu 1994, na ilishuka hadi 1.3 mnamo mwaka 2020 na 1.15 tu mnamo mwaka 2021.
Kwa kulinganisha, nchini Australia na Marekani jumla ya kiwango cha watoto wanaozaliwa ni 1.6 kwa kila mwanamke na 1.3 nchini Japan.
Haya yametokea licha ya China kuacha sera ya mtoto mmoja mwaka 2016 na kuanzisha sera ya watoto watatu
Nadharia zinatofautiana kuhusu kwa nini wanawake wa China wanasita kupata watoto licha ya motisha za serikali. Sababu moja ni kwamba idadi ya watu imezoea familia ndogo. Nyingine inahusu kupanda kwa gharama ya maisha, huku wengine wakifikiri huenda kunatokana na kuongezeka kwa umri wa kuoa, jambo ambalo huchelewesha kuzaliwa watoto na kuzima tamaa ya kupata watoto.
Aidha, China ina wanawake wachache walio katika umri wa kuzaa kuliko inavyotarajiwa. Kutokana na sharia ya kuwa na mtoto mmoja tu tangu 1980, wanandoa wengi walichagua mtoto mvulana, na kuinua uwiano wa jinsia wakati wa kuzaliwa kutoka wavulana 106 kwa kila wasichana 100 hadi 120, na katika baadhi ya mikoa hadi 130.

Chanzo cha picha, Sheldon Cooper/Getty Images)
Idadi ya watu nchini China iliongezeka kwa kupungua tangu kipindi cha njaa ya 0.34 tu kati ya 1,000 mwaka jana. Makadirio yaliyotayarishwa na timu katika Chuo cha Shanghai cha Sayansi ya Jamii yamepunguza mwaka huu - kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha njaa - kwa 0.49 kati ya elfu moja.
Mabadiliko yamekuja miaka kumi mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Hivi majuzi zaidi kama 2019 Chuo cha Sayansi ya Jamii cha China kilitarajia idadi ya watu kufikia kilele mnamo mwaka 2029, kwa watu bilioni 1.44. Ripoti ya Matarajio ya Idadi ya Watu ya Umoja wa Mataifa ya 2019 ilitarajia kilele baadaye, mwaka 2031-32, kufikia bilioni 1.46.
Timu ya Chuo cha Sayansi ya Jamii ya Shanghai inatabiri kushuka kwa mwaka kwa asilimia 1.1 baada ya 2021, na kusukuma idadi ya watu wa China hadi milioni 587 mnamo 2100, chini ya nusu ya ilivyo leo hii.
Sababu za utabiri huo ni kwamba jumla ya kiwango cha uzazi cha Uchina hupungua kutoka 1.15 hadi 1.1 kati ya sasa na 2030, na kubaki huko hadi 2100.
Kushuka huku kwa kasi kutakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa China.
Idadi ya watu walio katika umri wa kufanya kazi nchini China ilifikia kilele mwaka wa 2014 na inakadiriwa kupungua hadi chini ya theluthi moja ya kilele hicho ifikapo mwaka 2100. Idadi ya wazee wa China (watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi) inatarajiwa kuendelea kuongezeka kwa muda kupita idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi ifikapo mwaka 2080.

Chanzo cha picha, Wang Huabin / Getty Images
Hii ina maana kwamba wakati sasa kuna watu 100 wa umri wa kufanya kazi wanaopatikana kusaidia kila wazee 20, ifikapo mwaka wa 2100, Wachina 100 wenye umri wa kufanya kazi watalazimika kusaidia takriban wazee 100.
Kupungua kwa wastani kwa mwaka kwa asilimia 1.73 kwa idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi nchini China kunaweka mazingira ya ukuaji wa chini wa uchumi, iwapo kuongezeka watu hakutakuwa kwa njia ya haraka.
Gharama za juu za wafanyikazi, zikichochewa kwa wafanyakazi, zinatarajiwa kusukuma uzalishaji kutoka China hadi nchi zenye nguvu kazi kama vile Vietnam, Bangladesh na India.
Tayari, gharama za wafanyikazi wa utengenezaji nchini Uchina ni mara mbili juu kuliko huko Vietnam.
Wakati huo huo, China italazimika kuelekeza zaidi rasilimali zake za uzalishaji katika utoaji wa huduma za afya, matibabu na huduma kwa wazee ili kukidhi mahitaji ya idadi ya wazee inayoongezeka.
Licha ya utabiri kwamba hii itakuwa "karne ya Uchina", makadirio haya ya idadi ya watu yanaonyesha kwamba ushawishi unaweza kuhamia mahali pengine - pamoja na nchi jirani ya India, ambayo idadi yake yawatu inatazamiwa kuipita China ndani ya muongo huu unaokuja.












