Uturuki inataka urafiki zaidi na Israeli, hii ina maana gani?

Chanzo cha picha, ADEM ALTAN
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mavlut Chavushoglu na Waziri wa nishati Fatih Donmez wanaitembelea Israeli Jumatano. Uhusiano baina ya nchi mbili yalimekuwa magumu kwa miaka mingi.
Kulingana na ripoti, hii ni ziara ya kwanza kufanywa na waziri wa Ututruki nchini Israeli katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Lakini Chavushoglu na Donmez wanatembelea maeneo ya Wapalestina kabla ya kukutana na na Waziri mkuu mwenzake wa Israeli.
Katika siku za hivi karibuni, Uturuki na Israeli zimekuwa zikifanya juhudi za kuboresha uhusiano wao kwa pamoja. Issac Herzog, Rais wa Israeli, aliitembelea Uturuki, Rais wa Israeli, aliitembela Uturuki mwezi Machi. Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko makubwa katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Mwaka huu, kikosi cha makomando kiliwauwa wanaharakati kumi wa Uturuki ili kuvunja kizuizi cha kiuchumi cha Gaza ambao walikuwa wamepanda meli ya watalii ya Uturuki inayofahamika kama Mavi Marmara.
Mpasuko wa kidiplomasia baina ya nchi mbili ulimalizika mwaka 2016 wakati Israeli ilipotangaza kulipa fidia kutokana na tukio hilo.
Lakini hali ya wasi wasi imesalia kuhusu suala la Palestina na hadhi ya Jerusalem.
Uturuki inajaribu kuboresha mahusiano na mataifa mengi yenye nguvu ya kanda ya mashariki ya kati, sio tu Israeli. Hivi karibuni ilijaribu kuimarisha uhusiano wake na Muungano wa nchi za kiarabu , Saudi Arabia na Misri.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hakuna mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.
Kwa sasa, hakuna mahusiano ya kidiplomasia baina yan chi hizo mbili kwangazi ya mabalozi. Katika mwaka 2018, Uturuki ilimuondoa balozi wake baada ya vifo vya Wapalestina vilivyotokea baada ya vikosi vya Israeli kuwafyatulia risasi waandamanaji Wapalestina.
Chavushoglu amesema kwamba atafanya mazungumzo na waziri wa mamboya nje wa Israeli Yer Lapid kwa ajili ya kuwarerjesha tena mabalozi wan chi hizo mbili. Tofauti hukusu maeneo ya Wapalestina na hadhi ya Jerusalemu zimekuja kama kikwazo katika njia ya uhusiano wa karibu baina ya nchi mbili. Maafisa wa Uturuki wamekuwa wakisema kwamba uhusiano na Israeli hautakuwa wa kawaida kwa garama ya Palestina.
Uturuki pia inalaani vikali makabiliano ya hivi karibuni yaliyofanyika katika msikiti wa Al-Aqsa na kulitaja suala hilo kama pingamizi la kuboresha mahusiano.
Uturuki, hatahivyo, imesalia kuwa kimya kuhusu mauaji ya Meri 11 ya mwandishi wa habari wa Al Jazeera Shirin Abu Akleh.
Haijatoa tamko lolote la wizara yake ya mambo ya nje , wala Rais Erdogan hakusema lolote wazi kuhusu mauaji hayo.
Ni nini kitatokea kwa suala la Wapalestina?
Unaweza pia kusoma:
Rais Recep Tayyip Erdogan pia amesema kuwa mahusiano ya kisiasa na kiuchumi na Israeli ni "kando na suala la Jerusalem."
Balozi wa Wapalestina mjini Ankara, Fayed Mustafa, aliliambia gazeti linalounga mkono serikali ya Uturuki Sabah tarehe 23 Mei kwamba kuyafanya mahusino na Israeli kuwa ya kawaida haimaanishi kupuuza maslahi ya Wapalestina.
Gazeti la Sabah pia aliandika kwamba Chavushoglu pia atakutana na mweznake wa Walestina Riyadh al-Maliki wakati wa ziara na kufany amazungumzo na Baraza la muungano wa serikali linalojujmuisha wajumbe wa Uturuki na Wapalestina.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya Israeli, Chavushoglu anataka kwenda Al-Aqsa biula ulinzi wa maafisa wa Israeli au usalama.
Mwezoi Februari, msemaji wa rais Ibrahim Kalin na naibu waziri wa mambo ya nje Sadat Onal walifanya ziara katika eneo hilo. Kalin pia alipiga picha mbele ya msikiti wa Al-Aqsa Mosque.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je wote wataungana kwasababu ya gesi ?
Gazeti la upinzani lisilo la kidini la Jamhooriyat limeripoti kwamba suala lingine linaloweza kuzungumziwa wakat iwa ziara hiyo linaweza kuwa ni ushirikiano wa nishati.
Kuna matumaini madogo ya "maendeleo thabiti" kuhusu kusafirishwa kwa gesi asilia ya Israeli kuelekea Ulaya kupitia Uturuki , ilisema ripoti, na kuongeza kuwa ziara inaweza "hatua ya kwanza kuelekea katika kuaminiana ."
Maafisa wa Uturuki na vyombo vya habari hivi karibuni waliibua matarajio kuhusu mradi wa aina hii wa ushirikiano wa nishati baada ya shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, wakati Ulaya sasa inatafuta vyanzo vya nishati mbali na Urusi.
Wakati wa ziara ya Herzong mwezi Machi, Erdogan alisema kuwa Uturuki iko tayari kushirikiana na Israeli juu ya nishati na miradi ya usalama usalama.
Hivi karibuni, pia alisema kwamba nchi zote mbili zitaharakisha mchakato wa Mafuta na gesi asilia katika mashariki mwa Mediterranean. Wakati huo huo, pia alisema kwamba ni 'mwenye matumaini sana' kuhusu hilo.












