Mzozo wa Israel na Palestina: Je mataifa ya Kiarabu yanaweza kuinyamazisha Israel?

Chanzo cha picha, Getty Images
Saudi Arabia na Uturuki zina uadui na Dola ya Ottoman, wakati zote ni nchi zilizo na Waislamu wengi wa Sunni.
Inasemekana kuwa pia kuna ushindani kati ya uongozi wa ulimwengu wa Kiislamu kati ya hao wawili.
Saudi Arabia inamiliki Makka na Madina nayo Uturuki ikiwa mrithi wa Dola kubwa ya Ottoman.
Saudi Arabia na Uturuki huzungumza waziwazi kuwaunga mkono Wapalestina kuhusu mapambano yanayoendelea kati yao na Israeli .
Rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akizungumza zaidi akiunga mkono raia wa Palestina zaidi ya serikali ya Saudia.
Amekuwa akitoa taarifa tatu au nne kila siku na amekuwa akizungumza na viongozi wa mataifa ya Kiislamu kuhusu suala hilo.
Rais Erdogan pia alimpigia simu rais wa Urusi Vladimir Putin na kumtaka kuipatia funzo Israel.
Kabla ya vita ya dunia ya kwanza , Palestina lilikuwa eneo la dola ya Ottoman . Katika hali hiyo, bwana Erdoan ana haki ya kuzungumza na kujigamba.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tofauti zilizopo kati ya mataifa ya Kiislamu kuhusu suala la Palestina
Lakini pia kuna tofauti kuhusu uungwaji mkono wa Palestina kutoka kwa Uturuki.
Saudia haina uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Israel huku Uturuki ikiwa na uhusiano mzuri na taifa hilo.
Mwaka uliopita utawala wa rais Trump uliyashinikiza mataifa ya Ghuba kuimarisha uhusiano mzuri na Israel.
Matokeo yake yalifichuliwa. UAE na Bahrain ziliimarisha uhusiano wao na Israel.
Baada ya tukio hilo Sudan na Morocco pia ziliamua kuimarisha uhusiano mzuri na Israel.
Sudan na Morocco ni mataifa yenye Waislamu wengi.
Shinikizo kama hiyo pia ilikuwa kwa Saudia .
Lakini Saudia haikufanya hivyo na kusema kwamba Palestina haitakuwa na uhusiano mzuri na Israel hadi pale itakapokuwa huru chini ya miapaka ya 1967.
Saudia pia imekuwa ikitaka mashariki mwa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Palestina.
Uturuki ilikuwa ikiikosoa UAE na Bahrain kuhusu hatua yao ya kuimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Israel, Uturuki imekuwa na uhusiano mzuri na Israel tangu 1949.
Taifa hilo ndilo taifa la kwanza la Kiislamu kutambua Israel.
Hata 2005, rais Erdogan alienda Israel katika ziara ya siku mbili akiandamana na kundi kubwa la wafanyibaishara .
Wakati wa ziara hiyo alikutana na waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na kusema kwamba mpango wa kinyuklia wa Iran hautishii Israel pekee bali ulimwengu mzima.
Kumekuwa na chuki kati ya mataifa hayo maiwli tangu tukio la Mavi Marmar mwaka 2010.
Katika tukio hilo makomando wa Israel waliingia katika gari la Uturuki na kuwauwa watu 10.
Lakini licha ya tukio hilo mataifa hayo mawili yana uhusiano wa kibiashara .
Uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili ulikuwa na thamani ya zaidi ya $ 6 b kufikia mwaka 2019.

Chanzo cha picha, Getty Images
Since 2010, during the reign of Ardo अर्an, relations between Turkey and Israel have been close.
Kundi la wapiganaji wa Hamas, kundi la wanamgambo wa KIpalestina waliojihami limeorodheshwa Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya kama kundi la gaidi lakini Uturuki inalichukulia kundi hilo kama kundi la kisiasa.
Mataifa ya Ulaya yamekuwa yakiionya Uturuki kuhusu uwepo wa Hamas katika ardhi yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uhusiano kati Saudia na Hamas umekuwa mbaya
Tangu kuanzishwa kwa kundi la Hamas mwaka 1980, limekuwa na uhusiano mzuri na Saudia kwa miaka mingi.
Mwaka 2019, wafuasi kadhaa wa Hamas walikamatwa Saudia. Hamas ilikuwa imetoa taarifa ikiishutumu Saudia kwa hilo.
Hamas pia ililalamika kwa kudai Saudia iliwatesa wafuasi wake nchini humo.
Hamas iliendelea kupanuka na kuanzisha uhusiano na Iran 2000.
Talmiz Ahmed ambaye alikuwa balozi wa India katika mataifa ya Ghuba , anasema kwamba Hamas ni shirika la Waislamu wa Sunni huku Iran , taifa la Waislamu wa Shia, lakini wote wako karibu na siasa za Kiislamu.
Ahmed anasema kwamba licha ya Iran kuwa karibu na kundi hilo Haiisaidii Hamas.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uhusiano wa Hamas na Iran
Hatua ya kundi la Hamas kujitenga na Saudia iliendelea kwasababu ya uhasama uliopo kati ya Saudia na Iran.
Hakuna taifa linaloipinga Israel katika eneo la mshariki ya kati kama Iran.
Ni kutokana na hatua hiyo ndiposa uhusiano kati ya Hamas na Iran upo karibu mno.
Hamas ilishinda uchaguzi wa utawala wa Palestina 2007 na uwepo wake uliimarika baada ya ushindi huo.
Lakini uhusiano kati ya Hamas na Saudia pia haukuwa thabiti.
Wakati mapinduzi ya Arab spring yalipoanza 2011, watu wa Syria pia walienda barabarani na kufanya maandamano dhidi ya rais Bashar al Asaad.
Iran ilimuunga mkono Bashar al-Asaad na Hamas haikufurahia hatua hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokana na hali hiyo , kulikuwa na tofauti kati ya Iran na Hamas.
Lakini tabia ya Saudia dhidi ya mapinduzi hayo kuhusu Misri haikufurahisha Hamas.
Saudia ilikuwa ikipinga serikali ya kidemokrasia ya Misri .
Kutokana na hatua hiyo uhusiano kati ya Hamas na Iran uliimarika zaidi.
Ujumbe wa Hamas uliwasili Iran mwezi Julai 2019 na kukutana na kiongozi wa kidini wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei.
Nchini Saudia viongozi wa Hamas wanahusishwa na kundi la Muslim Brotherhood.
Na kufuatia vita kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa Hamas hivi majuzi, kundi hilo lilitoa wito kwa mataifa ya mashariki ya kati , Iran na Saudia kuwa na umoja.
Msemaji wa Hamas aliambia jarida la Newsweek , Israel imetusi msikiti wa Al-Aqsa .
'Hiyo ndio sababu tunarusha mabomu ya roketi .
Wanataka kuziondoa familia za Kipalestina kutoka mashariki mwa Jerusalem''.

Chanzo cha picha, Getty Images
Al Aqsa ndio eneo la tatu takatifi miongozi mwa Waislamu na eneo takatifu zaidi kwa Wapalestina.
''Tunataraji kwamba Saudia na Iran zitawacha tofauti zao . Iwapo hilo litafanyika itakuwa vyema kwa Wapalestina. ''
Je mataifa ya Kiislamu yataweza kufanya lolote?
Talmiz Ahmed, ambaye alikuwa balozi wa India katika nchi kadhaa za Ghuba, anasema, "Tatizo la Palestina na Israeli lilikuwa shida ya Kiarabu kabla ya 1967, lakini baada ya ushindi wa Israeli katika Vita vya Waarabu na Israeli mnamo 1967, ilibaki kuwa shida tu ya Israeli na Palestina ni. Iwapo kuna mtu yeyote anayeweza kuitatua, basi ni Waisraeli na Wapalestina. ''
Talmiz Ahmed anasema, "Mwitikio wa nchi za Kiislamu sio zaidi ya kujifanya tu.













