Fahamu uwezo wa kijeshi wa taifa la Uturuki

.

Chanzo cha picha, RT

Maelezo ya picha, Jeshi la Uturuki

Ushawishi wa jeshi la Uturuki umeonekana kuendelea kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni, cha karibuni kabisa kilichotokea ni kupelekwa kwa wanajeshi wa Uturuki kwenda nchini Libya na operesheni za hapo awali kaskazini mwa Syria.

Wakati huo huo, Taliban, ambayo ilichukua madaraka nchini Afghanistan mwezi mmoja uliopita na hivi karibuni iliunda serikali ya mpito, kwa usaidizi wa Uturuki.

Taliban wanajaribu kutojitenga ulimwenguni, na bado wanajaribu kudumisha uhusiano mzuri na China na Uturuki, na kudhibiti uwanja wa ndege huko Kabul.

Lakini je, jeshi la Uturuki lina nguvu kiasi gani?

Uturuki, ambayo pia ni mwanachama wa NATO na ina kituo kikubwa cha jeshi huko Mogadishu, Somalia, na limeelezewa na jeshi la ulimwengu kuwa jeshi lenye nguvu zaidi katika Mashariki ya Kati.

Jeshi la Uturuki linashika nafasi ya tisa katika orodha ya wanajeshi 137, likikadiriwa kuwa na matumizi ya dola bilioni 8 kila mwaka.

Serikali ya Uturuki imezingatia ufadhili wa kijeshi katika miaka ya hivi karibuni, kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa mnamo mwaka 2016, na Ankara imeanzisha uhusiano wa kijeshi na Urusi, Qatar na Somalia, ambayo ina kambi yake kuu nje ya Uturuki.

Kulingana na GFP, Uturuki ina nguvu zaidi kuliko Ujerumani, Italia, Misri, Iran, Israeli, Pakistan, Australia, Canada na Saudi Arabia, ikifuatiwa na Uingereza.

Nguvu ya jeshi la anga la Uturuki

.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ndege za kivita za Uturuki

Uturuki, yenye idadi ya watu milioni 80, imeajiri watu wanaokadiriwa kuwa milioni 42 na ina jumla ya wanajeshi 735,000.

Kulingana na taarifa ya The Global Fire Power, Uturuki ina takriban wanajeshi 355,000, wakati kikosi cha akiba kina wanajeshi 380,000.

Uturuki ni moja wapo ya mataifa yenye nguvu zaidi ulimwenguni, na ndege 1,067 za aina mbalimbali.

Kuna ndege 207 za kivita za Kituruki.

.

Chanzo cha picha, TDM

Maelezo ya picha, Ndege za kubeba mizigo za Uturuki

Kuna ndege 87 za kijeshi za mizigo za Uturuki na ndege 289 za mafunzo ya jeshi la anga.

Jeshi la Uturuki lina helikopta 792, kati ya hizo, 94 ni za kufanya mashambulizi.

Hivi karibuni Uturuki pia ilinunua makombora ya kujikinga dhidi ya uvamizi ya S-400 kutoka Urusi.

Nguvu ya jeshi la ardhini la Uturuki

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Makombora ya mfumo aina ya s-400 ya Urusi

Vikosi vya ardhini vya Uturuki ni kikosi cha jeshi cha saba chenye nguvu zaidi duniani.

Kuna vifaru 3,200 vya Uturuki na magari 9,500 ya kivita.

Jeshi la Uturuki pia lina makombora 1,120, BMs 350 na aina nyingine za silaha, zenye uwezo wa kujisukuma au kujifyatua zenyewe.

Nguvu ya jeshi la majini la Uturuki

.

Chanzo cha picha, Turkey Navy

Maelezo ya picha, Jeshi la majini la Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alizindua ndege ya kwanza aina ya dash wiki chache zilizopita, na kusema kuwa nyingi zaidi zinatengenezwa.

Jeshi la majini la Uturuki lina boti 34 za doria, manowari 12, meli 16 za kivita.

Jeshi la wanamaji la Uturuki pia linamiliki Rasi ya Anatolia, ambayo ni meli ya kivita.

Rais Erdogan amesema kuwa ifikapo mwaka 2022 wataanzisha moja kwa moja shughuli ya ujenzi wa maeneo ya mazoezi nchini Uturuki.

Hilo litawezasha uendeshaji wa shughuli kutoka mbali.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, .

Taarifa ya tovuti ya Global Fire Power pia inajumuisha majeshi 10 yenye nguvu zaidi duniani kwa kuyataja:

1. Marekani

2. Urusi

3. China

4. India

5. Ufaransa

6. Japan

7. Korea Kusini

8. Uingereza

9. Uturuki

10. Ujerumani