‘Usiwe kijana wa madhabahu ya Putin’ - Ukosoaji usio wa kawaida wa Papa Francis kwa Patriaki Cyril kwa msaada wake kwa vita vya Ukraine

Cirilo y Francisco.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cirilo na Francisco walifanya mkutano wa kihistoria nchini Cuba mnamo Februari 2016.

Viongozi wawili wa kidini muhimu zaidi ulimwenguni wamehusika katika ubadilishanaji wa maneno na mivutano ambayo ni nadra sana kuonekana katika historia ya hivi karibuni ya Ukristo.

Sababu? - Vita katika Ukraine.

Papa Francis, mkuu wa Ukatoliki, alimwomba Patriaki Cyril, sawa na Papa Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi, asiwe ''kijana wa madhabahu ya Putin'', kwa msaada aliotoa kwa uvamizi wa Kremlin katika nchi jirani.

Kama Francis alivyothibitisha katika mahojiano na gazeti la Italia Il Corriere della Sera, Machi mwaka jana alikuwa na mazungumzo na mwenzake wa Urusi ili kujaribu kumfanya Cirilo, ambaye yuko karibu sana na Putin, amzuie rais wa Urusi kuendelea na mashambulizi.

''Nilizungumza naye kwa dakika 40 kupitia Zoom,'' papa alisema, ambaye alikumbuka kwamba katika dakika 20 za kwanza patriki alimsomea karatasi mkononi, ''uhalali wote wa vita.''

''Nilisikiliza na kumwambia: Sielewi lolote kati ya haya. Ndugu, sisi si mapadre wa serikali, hatuwezi kutumia lugha ya siasa, badala yake ya Yesu. Baba wa taifa hawezi kuwa kijana wa madhabahu ya Putin,'' alisema.

Wataalamu wa masuala ya Kanisa wanasema kuwa maneno ya Francis yamekuwa njia panda inayojulikana kati ya viongozi hao wa kidini.

putin y cirilo

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika taarifa yake, Kanisa la Othodoksi la Urusi limeyataja matamshi ya papa kuwa ''majuto'' na kuongeza kuwa maneno hayo hayachangii umoja wa kidini.

''Inasikitisha kwamba mwezi mmoja na nusu baada ya mazungumzo na Patriaki Cyril, Papa Francis amechagua sauti isiyo sahihi ili kuwasilisha yaliyomo kwenye mazungumzo,'' Idara ya Mahusiano ya Kigeni ya Patriarki wa Urusi ilisema.

''Kauli kama hizo hazichangii katika kuanzisha mazungumzo ya kujenga kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Othodoksi la Urusi, ambayo ni muhimu sana wakati huu,'' taarifa hiyo inaongeza.

Kufutwa kwa mkutano

Papa pia alifichua kwamba, baada ya mazungumzo hayo, alimwomba patriarki kufuta mkutano ambao viongozi wote wa kidini walikuwa wamepanga ufanyike mnamo mwezi Juni huko Yerusalemu.

''Itakuwa ni mkutano wetu wa pili wa ana kwa ana, hauhusiani na vita. Lakini sasa, pia anakubali kwamba haupo kwa sababu inaweza kuwa ishara isiyoeleweka,'' Francis aliliambia gazeti la Italia.

Vyombo vya habari kadhaa vya Magharibi viliripoti Jumatano kwamba Cirilo atakuwa miongoni mwa watu waliojumuishwa na Uropa katika kifurushi kipya cha vikwazo dhidi ya Urusi kwa vita vya Ukraine.

Ingawa mwishowe Umoja wa Ulaya bado unaweza kurekebisha orodha hiyo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kidini wa Urusi mashuhuri kukabiliwa na vikwazo kutoka kwa umoja huo.

Cirilo y Francisco

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Cirilo na Francisco walikuwa wamekutana Havana kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016

Akizungumza na shirika la serikali TASS, msemaji wa Kanisa la Othodoksi la Urusi, Vladimir Legoida, alihoji ikiwa Ulaya inapanga kumuwekea vikwazo Cyril, ambayo, kwa maoni yake, ni ''ukosefu wa akili''.

''Kadiri vikwazo vinavyozidi kuwa vya kubagua, ndivyo wanavyopoteza akili ya kawaida na ndivyo inavyokuwa vigumu kupata amani, ndiyo maana Kanisa la Othodoksi la Urusi husali katika kila ibada kwa baraka za Mtakatifu wake Patriaki,'' msemaji huyo alisema.

"Ni wale tu ambao hawajui kabisa historia ya Kanisa letu wanaweza kujaribu kuwatisha makasisi na waumini wake," aliongeza.

putin y cirilo

Chanzo cha picha, Getty Images

Tangu kuanza kwa vita, Cyril amekuwa akiipendelea na hata amebariki wanajeshi na silaha ambazo Kremlin imetuma kwa nchi jirani.

Mnamo mwezi Machi, mkuu huyo wa kanisa alisema mzozo huo ulikuwa ''upanuzi wa mapigano ya kimsingi ya kitamaduni kati ya ulimwengu mpana wa Urusi na maadili ya Magharibi yanayozingatia uhuru,'' akirejelea hotuba za awali za Putin.

Mbali na kutokemea kwa uthabiti mauaji ya watu wasio na hatia nchini Ukraine au kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, Cyril alienda mbali zaidi na kusema katika huduma kubwa za televisheni kwamba kubariki wanajeshi waliopo vitani huko Kremlin ni lazima na muhimu kwa mustakabali wa Ukristo.

''Kinachotokea leo ni muhimu zaidi kuliko siasa. Tunazungumza juu ya wokovu wa mwanadamu, ubinadamu unakwenda wapi, uko upande gani kwa heshima ya Mungu Mwokozi,'' alisema.

Dini ya Orthodox, iliyopigwa marufuku wakati wa enzi ya Usovieti, imepata umaarufu mkubwa wakati wa serikali ya Putin na wataalam kadhaa wa maswala ya kidini wanasema kuwa rais wa Urusi anataka kuipa umaarufu kama ilivyokuwa wakati wa mfalme.

Mgawanyiko mpya

Ukristo wa Orthodox ni mojawapo ya jumuiya kubwa zaidi za Kikristo duniani, baada ya Ukatoliki na Kanisa la Kiprotestanti.

Ina wafuasi wapatao milioni 260, haswa katika Uropa, Urusi na nchi zingine ambazo zilikuwa sehemu ya Muungano wa Kisovieti wa zamani.

Kati yao, karibu milioni 100 hufuata partriaki wa Moscow, kulingana na data kutoka Kituo cha Utafiti cha Pew.

Walakini, uungaji mkono wa Cyril kwa Putin na vita umeanza kusbabisha mgawanyiko mpya kati ya makanisa anuwai ambayo yalitoa heshima kwa baba mkuu.

Mapadre wengi wa Ukraine wameamua kuacha kulifuata Kanisa la Urusi baada ya kuanza kwa uvamizi huo na kwa mujibu wa ripoti, waumini wengi wa Kanisa la Orthodox wameacha kumwombea Baba wa Kanisa huyo wakati wa ibada, ambayo inachukuliwa kuwa ishara kubwa zaidi ya uasi duniani.

iglesia

Chanzo cha picha, Getty Images

Takwimu kutoka Chuo cha Theolojia cha Kyiv zinaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya parokia 12,000 za Patriaki ya Moscow huko Ukraine wametangaza kwamba wanataka kujitenga.

Mnamo mwezi Machi, Kanisa la Orthodox la Urusi huko Amsterdam pia liliripoti kuvunja uhusiano na kiongozi huyo wa kidini.

línea