Mzozo wa Ukraine : Je kombora la Neptune lililotumika kuiangamiza meli ya kivita ya Urusi ni kombora la aina gani?

Limekuwa ni mojawapo ya maswali makubwa tangu kuzama kwa meli ya kikosi cha majini cha Urusi inayofahamika kama Moskva, ikiwa ndio meli kuu ya jeshi la majini la Urusi katika Bahari nyeusi, iliyolipuka na kuzama wiki hii.

Nini kilichotokea kwa zaidi ya wanajeshi 500 waliokuwa wakisafiri ndani yake?

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilithibitisha Jumatano wiki iliyopita kulipuka kwa "moto" katika boti na kuhakikisha kuwa ilikuwa imewaokoa wanajeshi wake.

Siku moja baadaye, iliripoti kwamba meli hiyo ilikuwa imezama kutokana na "hali mbaya ya hewa."

Haikuelezea zaidi juu ya sababu, lakini Ukraine ilihakikishiwa kabla ya Urusi kuthibitisha taarifa kwamba ilikuwa imepigwa na makombora mawili aina ya Neptune.

Tangu wakati ule , hatma ya wahudumu ya meli muhimu zaidi ya Urusi katika Bahari nyeusi iliibua kila aina za dhana.

Jumamosi, wizara ya ulinzi ya Urusi ilichapisha picha zinazoonyesha kile inachosema ni abiria wanajeshi wa kikosi cha majini wanaohudumu katika meli ya Moskva.

Haijulikani ni lini picha hizi zilichukuliwa au iwapo kweli walikuwa ni wafanyakazi wa meli hiyo, lakini ni mara ya kwanza kwamba Urusi imewaonyesha wanajeshi kama manusura wa kile kilichotokea katika meli.

Lakini je kombora la Neptune lililotumika kuiangamiza meli hiyo ni la aina gani?

Maafisa wa jeshi mjini Kyiv wanasema kwamba waliishambulia meli ya kivita ya Urusi Moskva na kombora lililoundwa Ukraine kwa jina Neptune.

Mfumo huo wa kombora uliundwa na wahandisi wa jeshi la Ukraine kutokana na tisho lililokuwa likitolewa na Urusi katika bahari nyeusi baada ya kuuteka mji wa bandari wa Crimea 2014.

Kulingana na gazeti la Kyiv, jeshi la wanamaji wa Ukraine lilipokea mzigo wa kwanza wa kombora hilo linaloweza kuruka kwa umbali wa kilomita 300 mwezi Machi mwaka uliopita.

Tangu uvamizi uanze , Ukraine imepokea idadi kubwa yamsaada wa vifaa vya kijeshi kutoka kwa washirikla wake , ikiwa ni pamoja na makombora ya kukinga ndege na vifaru yenye gharama ya £100m ambayo Uingereza ilitangaza kuwa ingetuma wiki iliyopita.

Historia ya meli ya kivita ya Moskva

Ikiwa ni meli iliotengenezwa nchini Ukraine wakati wa enzi za Usovieti , meli hiyo ilianza kuhudumu mapema miaka ya themanini kulingana na vyombo vya habari vya Urusi.

Meli hiyo ya kurusha makombora kwa mara ya kwanza ilipelekwa Syria ambapo iliwapatia ulinzi wanamaji wa Urusi.

Ilikuwa imebeba makumi ya makombora ya kushambulia meli, makombora ya kuangamiza nyambizi, na makombora ya Torpedo, ripoti zilisema.

Moskva ndio meli ya pili kwa ukubwa nchini Urusi kuangamizwa tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Je meli ya Moskva ilikuwa na ulinzi wa aina gani?

''Meli hiyo ilikuwa ndio meli ya tatu kwa ukubwa nchini Urusi na mojawapo ya meli zinazolindwa sana nchini humo '', alisema mtaalamu wa jeshi la wanamaji Jonathan Bentham kutoka kituo cha kimataifa cha mafunzo ya kimkakati akizungumza na BBC.

Meli hiyo ilikuwa ikijihami na mfumo wa kujilinda na makombora ya angani ambao iwapo ungetumika vyema ungeipa fursa tatu za kujilinda kutoka kwa shambulio la Neptune.

Mbali na ulinzi wa masafa marefu na masafa mafupi ilikuwa na mifumo ya kujilinda dhidi ya aina sita ya makombora ya masafa mafupi (CIWS}. Bwana Bentham anasema kwamba Moskva ilikuwa na uwezo wa kujilinda kwa makombora ya angani kupitia kuzunguka digirii 360.

'Mfumo huo wa CIWS una uwezo wa kurusha risasi 5,000 kwa dakika moja' .

Iwapo shambulio hilo litathibitishwa kutoka kwa kombora, basi linazua swali kuhusu silaha za kisasa za Urusi .

Iwapo ilikuwa na makombora ya kutosha kutekeleza shambulio ama pengine ilikuwa na hitilafu ya kimitambo.

''Ukweli ni kwamba mtu angelifikiria kwamba kutokana na mfumo huo wenye ngome tatu za kujilinda ingelikuwa vigumu sana kuishambulia'' , alisema mtaalamu hiyo.

Kwanini shambulizi la Moskva kuitikisa Moscow

Urusi inasema meli yake ya ya makombora katika bahari ya Black Sea Moskva imeharibiwa vibaya na moto uliosababishwa risasi zake kulipuka.

Maafisa wa Ukraine hata hivyo wanasema meli hiyo imepigwa na makombora yake mawili - lakini hii bado haijathibitishwa.

Mykola Bielieskov ni mtafiti katika Taasisi ya Kitaifa ya Ukraine ya Mafunzo ya Kimkakati mjini Kyiv - ambayo inaishauri serikali ya Ukraine kuhusu masuala ya kijeshi. Anasema tukio hilo "ni chombo chenye nguvu sana cha kisaikolojia kusaidia ari".

Hata hivyo, anabainisha kuwa Moskva "ni meli ya zamani" - na imekuwa meli mpya zaidi za Urusi ambazo zimekuwa zikiipiga Ukraine na "makombora ya cruise ya Kalibr".

"Lakini bado, ni kinara kwa meli ya Bahari Nyeusi ya Urusi na hakika ni uharibifu mkubwa - sio tu katika uwezo wa nyenzo lakini pia kwa ari.

"Na kwa upande mwingine ni kuongeza nguvu sana kwa ari ya Kiukreni.

Hiki ni kikwazo kikubwa kwa juhudi za vita vya Urusi, kwa sababu za kijeshi na kimaadili. Moskva ni meli ya zamani ya enzi ya Sovieti lakini imekuwa kinara wa meli za Bahari Nyeusi za Urusi tangu 2000.

Meli hiyo ya kivita ya tani 12,500 imekuwa sehemu ya meli za Urusi zinazopiga doria nje ya bahari na kutishia bandari ya Odesa ya Ukraine.

Waukraine wanaijua kama meli iliyoamuru watetezi wao wa Kisiwa cha Snake kujisalimisha na waliambiwa "kwenda kuzimu".

Kwa hivyo chochote kilichosababisha moto huo mkubwa - na Ukraine inasema kuwa ni makombora mawili yaliyorushwa na vikosi vyake.

Kwa maneno ya kiutendaji zaidi, tukio hili huenda likasababisha meli za kivita za Urusi kulazimika kusogea nje ya nchi kwa usalama wao wenyewe.

Hii inafuatia mlipuko wa awali kwenye meli ya Urusi, ambayo inaaminika kuwa matokeo ya shambulio la siri la Ukraine.

Shambulizi dhidi ya meli hiyo ni 'jambo muhimu kwa motisha ya Ukraine'

Prof Michael Petersen, mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Bahari ya Russia katika Chuo cha Vita vya Wanamaji cha Marekani, amekuwa akizungumza na kipindi cha Radio 4's Today kuhusu habari kwamba meli ya Urusi ya Moskva imeharibiwa vibaya.

Pande zote zinasema nini?

•Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema kuwa mlipuko ulitokea ndani ya Moskva, meli kuu ya msafara wa Black Sea ya nchi hiyo, "iliharibu vibaya" meli hiyo, na kwamba wafanyakazi wote wameondolewa.

•Urusi haikusema sababu ya moto huo, lakini awali Ukraine ilisema ilifanya shambulio la makombora dhidi ya meli hiyo

• Mapema katika vita hivyo, watu wa Ukrainie waliokuwa kwenye Kisiwa cha Snake katika Bahari Nyeusi walikaidi amri ya kujisalimisha kutoka kwa meli hiyo, wakiiambia Moskva "kwenda kuzimu"

Unaweza pia kusoma