Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Huenda Rais wa Urusi, Vladimir Putin amewashangaza wengi kwa kuivamia Ukraine, hatua yake kubwa zaidi katika eneo hilo tangu kulinyakua jimbo la Crimea mwaka 2014 lakini hajawahi kufanya azma yake ya kurejesha ushawishi wa Urusi kuwa siri.
Putin amekuwa madarakani tangu 2000 - akihudumu katika nafasi za urais na uwaziri mkuu wa Urusi kwa nyakati tofauti na ndiye kiongozi wa Kremlin aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi tangu kiongozi wa Soviet, Joseph Stalin, ambaye alifariki dunia 1953.
Kura ya kitaifa yenye utata kuhusu mageuzi ya katiba mwaka 2020 ilimpa Putin fursa ya kusalia kiongozi zaidi ya muhula wake wa sasa wa nne, ambao utakamilika mwaka wa 2024. Hivyo anaweza kusalia Kremlin hadi 2036.
Lakini alifikaje hapa? Huu hapa ni muelekeo wa maisha ya kisiasa na ya kibinafsi. Kwa sasa anagonga vichwa vya habari kote duniani.
Jasusi wa zamani
Wakosoaji wanaona kuwa sifa za enzi ya Usovieti ziliunda mtazamo wake wa ulimwengu.
Alikuwa jasusi katika KGB - wakala maarufu wa usalama wa Soviet - kabla ya kupanda kwake wakati wa machafuko ya kuanguka kwa USSR.
Wengi wa wasaidizi wake wa karibu na marafiki walikuwa wanafanya kazi za siri.
Kazi ya kisiasa ya Putin ilianza mapema miaka ya 1990, alipofanya kazi kama msaidizi mkuu wa meya wa St Petersburg, Anatoly Sobchak, ambaye hapo awali alimfundisha sheria katika Chuo Kikuu.
Mnamo 1997, aliingia Kremlin kama mkuu wa Huduma ya Usalama ya Shirikisho (FSB - mrithi mkuu wa KGB) na baada ya kipindi kifupi aliteuliwa kuwa waziri mkuu.
Katika mkesha wa mwaka mpya, 1999, Rais wa Urusi Boris Yeltsin alijiuzulu na kumteua Putin kuwa kaimu rais.
Amekuwa madarakani tangu wakati huo, ingawa alilazimika kuhudumu kama waziri mkuu kati ya 2008 na 2012 baada ya katiba ya Urusi kumzuia kuwania muhula wa tatu mfululizo.
Putin alirejea mamlakani kwa kushinda uchaguzi wa 2012 kwa zaidi ya 66% ya kura, huku kukiwa na shutuma za kuiba kura.
Amerejesha maonesho ya mtindo wa Kisovieti kwa magwaride ya kijeshi, na picha za Stalin, zilizopigwa marufuku zimeonekana tena.
Putin alielezea kuporomoka kwa USSR kama "janga kubwa zaidi la kisiasa la Karne ya 20" na mara kwa mara amekosoa upanuzi wa umoja wa kujihami wan chi za Maghari NATO hadi mipaka ya Urusi tangu 1997.
Mahusiano ya Frosty na Mataifa ya Magharibi
Mvutano wa awali kati ya Urusi na Ukraine na hatua ya Moscow kuingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria kumuunga mkono rais Bashar al-Assad tayari ilikuwa imeibua tena tuhuma za nchi za Magharibi kuhusu Putin.
Mahusiano yalikuwa ya baridi kama yalivyokuwa wakati wa Vita Baridi, ingawa mtu pekee alikuwa Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ambaye alionesha wazi kufurahishwa na mwenzake wa Urusi.
Mrithi wake, Joe Biden, kwa upande mwingine amemtaja Putin kama "muuaji".
Rais Putin anaonekana kufurahia taswira yake ya macho, akisaidiwa na matukio ya uchaguzi kama vile kuruka hadi Chechnya kwa ndege ya kivita mwaka wa 2000 na kuonekana kwenye tamasha la waendesha baiskeli wa Urusi karibu na Bahari nyeusi mwaka 2011.
Lakini Putin pia ameonesha upande mzuri kwenye vyombo vya habari vya serikali ya Urusi, akiwakumbatia mbwa wake na kusaidia kutunza Amur walio hatarini kutoweka.
Utafiti uliofanywa na Kituo cha Levada cha Urusi mnamo Februari 2021 ulipendekeza kwamba 48% ya Warusi wangependa Putin abaki katika wadhifa wa urais hadi 2024.
Alipata umaarufu wa kisiasa kwa kuiweka Urusi katika hali ya utulivu baada ya machafuko ya baada ya ukomunisti miaka ya 1990.
Kando na kurejesha fahari ya kitaifa, Rais Putin ameruhusu tabaka la kati kuibuka na kufanikiwa, ingawa Moscow bado inatawala uchumi na kuna.
Machafuko nyumbani
Umaarufu wake kati ya Warusi wenye umri mkubwa ni nguvu zaidi kuliko miongoni mwa vijana. Makundi hayo mawili yana watu waliokulia chini ya uongozi wa Putin na wengi wao hasa vijana wanaonekana kuwa na kiu ya mabadiliko.
Maelfu ya vijana wa Urusi waliandamana nchi nzima mnamo Januari 2021 kumuunga mkono Alexei Navalny, mkosoaji mkuu wa Rais Putin, ambaye alikamatwa mara baada ya kurejea kutoka Berlin Ujerumani.
Navalny alijipatia umaarufu kwa kufichua ufisadi uliokithiri, akikitaja chama cha Putin cha United Russia kuwa "chama cha walaghai na wezi".
Maandamano ambayo yaliibuka yalikuwa ni baadhi ya maandamano makubwa zaidi ambayo Urusi iliwahi kuona katika miaka iliyopita.
Polisi walifanya msako mkali na maelfu ya watu kuwekwa mahabusu.
Navalny, ambaye sasa ana afya mbaya gerezani, aliyehukumiwa kwa utata kutokana na kesi ya zamani ya ubadhirifu, ni sababu nyingine kuu kwa nini uhusiano wa Bw Putin na nchi za Magharibi kuvunjika.
Mnamo Agosti 2021 alinusurika chupuchupu kushambuliwa na wakala wa neva wa Novichok, ambao serikali za Magharibi baadaye zililaumu moja kwa moja juu ya Huduma ya Usalama ya Shirikisho ya Bw Putin (FSB).
Novichok - sumu ya kiwango cha silaha ya Kirusi - pia ilitumiwa kuwatia sumu jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake Yulia nchini Uingereza mnamo 2018.
Bw Putin alikanusha uhusiano wowote na mashambulizi hayo na mengine dhidi ya wapinzani mashuhuri wa kisiasa.
Navalny, ambaye sasa ana afya mbaya gerezani, aliyehukumiwa kwa utata kutokana na kesi ya zamani ya ubadhirifu, ni sababu nyingine kuu ya kuvunjika kwa uhusiano wa Putin na nchi za Magharibi.
Mnamo Agosti 2021 alinusurika chupuchupu kushambuliwa na kwa sumu ya Novichok, ambao serikali za magharibi baadaye zilielekeza lawama moja kwa moja kwa Huduma ya Usalama ya Shirikisho ya Rais Putin (FSB).
Novichok - sumu ya Kirusi ya kiwango cha silaha - pia ilitumiwa kuwatia sumu jasusi wa zamani wa Urusi, Sergei Skripal na binti yake Yulia nchini Uingereza mwaka 2018.
Putin alikanusha serikali yake kuwa na uhusiano wowote na mashambulizi hayo na mengine dhidi ya wapinzani wake mashuhuri wa kisiasa.
Utoto mgumu
Vladimir Putin amekulia katika mtaa mgumu wa makazi ya jumuiya huko Leningrad - sasa ni St Petersburg - na alipigana na wavulana ambao mara nyingi walikuwa wakubwa na wenye nguvu kumzidi. Hiyo ilimsukuma kuchukua mafunzo ya judo.
Kulingana na tovuti ya Kremlin, Putin alitaka kufanya kazi katika ujasusi wa Usovieti "hata kabla ya kumaliza shule".
"Miaka 50 iliyopita mtaa wa Leningrad ulinifundisha sheria: Ikiwa pigano ni lazima urushe ngumi ya kwanza," Putin alisema Oktoba 2015.
Alitumia lugha isiyo rasmi ya mpiganaji wa mitaani wakati akitetea mashambulizi yake ya kijeshi dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga huko Chechnya, na kuapa kuwaangamiza "hata katika choo".
Jamhuri ya Caucasus Kaskazini yenye waislamu wengi iliachwa ikiwa imeharibiwa na mapigano makali ya 1999 hadi 2000, ambapo maelfu ya raia waliuawa.
Georgia ilikuwa kielelezo kingine cha Putin. Mnamo 2008, vikosi vyake vililishinda jeshi la Georgia na kuchukua maeneo mawili yaliyojitenga - Abkhazia na kusini mwa Ossetia.
Ilikuwa ni mgongano wa kibinafsi sana na Rais wa Georgia wakati huo aliyekuwa akiunga mkono Nato, Mikheil Saakashvili na ilionesha utayari wa Putin kuwadhoofisha viongozi wanaounga mkono nchi za magharibi katika majimbo ya zamani ya Soviet.
Marafiki wa mabilionea
Watu wa karibu wa Putin ni wasomi matajiri na yeye mwenyewe anaaminika kuwa na utajiri mkubwa.
Anailinda vizuri familia yake na masuala ya kifedha dhidi ya umma.
Uvujaji wa nyaraka za Panama mnamo 2016 ulifichua mtandao mbovu wa kampuni za nje ya nchi zinazomilikiwa na rafiki wa muda mrefu wa Putin - mwigizaji wa tamasha Sergei Roldugin.
Putin na mkewe, Lyudmila walitalikiana mwaka wa 2013 baada ya takribani miaka 30 ya ndoa.
Kulingana na uchunguzi wa shirika la habari la Reuters, mmoja wa mabinti wa Putin, Katerina, ana kazi ya juu ya utawala katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Moscow na hucheza katika mashindano ya rock 'n' roll.
Uzalendo wa Putin unatawala vyombo vya habari vya Urusi, na hivyo kupeperusha habari zinazomuunga mkono, hivyo upinzani kamili ni vigumu kupata tathmini.
Katika mihula yake miwili ya kwanza kama rais, Putin alichangamshwa na mapato kutokana na mauzo ya mafuta na gesi - mauzo ya nje ya Urusi. Viwango vya maisha kwa Warusi wengi viliboreshwa.
Lakini kwa maoni ya wengi, maboresho hayo yalikuwa na athari ya mmomonyoko wa demokrasia changa ya Urusi.
Tangu msukosuko wa kifedha duniani wa 2008, Putin ametatizika na 'uchumi wenye upungufu wa damu', uliokumbwa na mdororo wa kiuchumi na kushuka kwa bei ya mafuta hivi karibuni.
Urusi ilipoteza wawekezaji wengi wa kigeni na mabilioni ya dola kutokana na ukosefu wa mitaji.
Utawala wa Rais Putin umegubikwa na utaifa wa kihafidhina wa Urusi, unaohimizwa na Kanisa la Orthodox.
Mara tu baada ya kuwa rais, Putin alianza kuwatenga watu walio huru, mara nyingi akiwaweka washirika wenye msimamo mkali au wasioegemea upande wowote wanaoonekana kuwa watu wa kusema zaidi-ndiyo.
Kwa mfano, Watu waliokuwa wafuasi wa Yeltsin, kama vile matajiri Boris Berezovsky na Vladimir Gusinsky, waliishia kuwa wakimbizi wanaoishi uhamishoni nje ya nchi.
Sasa, wakati Urusi inaivamia Ukraine na Putin anaonya kwamba jibu la Moscow litakuwa "papo hapo" iwapo mtu yeyote atajaribu kuingilia masuala ya Urusi - macho yote yapo kwa rais wa Urusi kuona atakachokifanya baadaye.