Mambo matano muhimu katika mkutano wa rais Samia na makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan, amekutana na Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris ikulu ya white house nchini Marekani.
Katika mkutano wao walianza kwa kutoa taarifa fupi juu ya mazungumzo yao kwa waandishi wa Habari.
Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika muda mchache ujao , masuala mbalimbali yatajadiliwa baina ya nchi hizo mbili.
Ukuaji wa uchumi

Chanzo cha picha, Getty Images
Jambo la kwanza litakalojadiliwa katika mkutano huo ni ukuaji wa uchumi katika nchi hizo mbili. Kamala Harris amezungumzia jinsi Marekani inafahamu kuwa kipaumbele cha Tanzania ni kukuza uchumi wake.
''Marekani inaangalia sehemu za kuwekeza ili kukuza uchumi wa Tanzania na Marekani na maeneo hayo pia ikiwemo kwenye suala la utalii'' anasema Kamalla.
Afya ya jamii
Katika suala la afya, mkutano huo utaangazia suala muhimu la afya, ikiwemo ugonjwa wa corona ambao unasumbua maeneo mengi duniani. Watajidili pia kuhusu afya ya wanawake na Watoto nchini Tanzania.
''hili ni eneo ambalo tumelipa kipaumbele mimi na rais pia, hivyo tunarajia ushirikiano mkubwa kutoka Tanzania na nchi nyingine za Afrika'' amesema Kamala.
Uhusiano na ushirikiano
Suala linguine ambalo litatawa mkutano huo ni kuangazia ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, ikiwemo miradi ambayo Tanzania inafaidika kutoka Marekani.
''Serikali yangu ingependa kuona uhusiano wetu ukiendelea kwa kasi, tumekua na miradi mbalimbali ambayo imesaidia sana taifa la Tanzania'' amesema rais Samia
Haki za binadamu na demokrasia

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Tanzania alieleza jinsi gani Tanzania imepiga hatua katika kuhakikisha kuna uhuru wa kujieleza, demokrasia na haki za binadamu.
''Tumechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha tunakua na haki, uhuru na demokrasia, kwa upande wa siasa tumeanza majadiliano na ushirikiano baina ya vyama mbalimbali vya siasa.
Uwekezaji na biashara
Uwekezaji ni eneo jingine ambalo litaibuka katika mazungumzo baina ya Samia na Harris ni suala la uwekezaji hususana nchini Tanzania. Rais Samia katika mkutano huo mfupi na waandishi wa Habari alieleza mazingira rafiki ya uwekezaji nchini Tanzania na sera zilivyobadilika.
Samia Suluhu yupo Marekani kwa ziara ya kikazi, mapema wiki ijayo anatarajia kuzindua kipindi maalum cha kutangaza utalii wa nchi yake.















