Vita vya Ukraine: Kamanda mkuu mpya wa vikosi vya Urusi Aleksandr Dvornikov, ni nani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ikikiri kwamba imeumia kwa " majeshi yake kupoteza maeneo,"Urusi imemteua jenerali mpya kuendeleza awamu inayofuata katika uvamizi wa Ukraine.
Naye ni Aleksandr Dvornikov, mwanaume mwenye uzoefu wa kijeshi ambaye alikuwa na nafasi muhimu katika vita vya Syria, akiongoza vikosi ambavyo vilishutumiwa kutekeleza vitendo vya unyanyasaji mkubwa dhidi ya raia n ahata kufanya uhalifu dhidi ya binadamu.
Uteuzi wake ulithibitishwa na afisa wa ngazi ya juu wa Marekani ambaye hakutaka jina lake lijulikane.
Hadi sasa, Urusi haikuwa na kamanda mkuu wa vikosi vyake katika Ukraine.
Dvornikov anachukua wadhifa huo baada ua kushindwa kuliokoigarimu Urusi katika mashambulizi ya awali, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vifo miongoni mwa rai awa Ukraine, pamoja na matatizo ya zana na ''makosa''ambayo yamechangua kupungua kwa kasi ya mashambulizi ya vikosi vya Urusi ndani ya Ukraine, kulingana na maafisa wa Marekani.
Tangu uvamizi ulipoanza mwishoni mwa mwezi wa Februari, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imethibitisha kuwa zaidi ya raia 1,600 wameuawa wakiwemo Watoto 100.
Lakini Rais wa Ukraine Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Jumatatu kwamba mji wa mwambao wa Mariupol pekee unaweza kuwa na maelfu ya vifo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sasa kuna hofu kwamba hali ya kibinadamu itakuwa mbaya zaidi baada ya uteuzi wa Jenerali Aleksandr Dvornikov kama mkuu wa mashambulio ya Urusi dhidi ya Ukraine
Ni mwanajeshi mwenye uzoefu
Dvornikov alijiunga na jeshi la Usovieti katika mwaka 1978 baada ya kuhitimu kutoka shule ya kijeshi iliyoko mashariki mwa Urusi.
Alianza kazi yake kwa kupanda cheo haraka baada ya kupata cheo kama platuni kamanda katika mwaka1982.
Alipata diploma ya masuala ya kijeshi katika chuo cha jeshi cha Frunze katika mwaka 1991, katikati ya kuvunjika kwa Muungano wa Usovieti.
Katika miaka ya 2000, Dvornikov alipigana katika vita ya pili nchini Chechnya na kushikilia vyeo vya juu kadhaa kabla yar ais wa Urusi Vladimir Putin kumteua kuwa mkuu wa majeshi ya Urusi nchini Syria katika mwaka 2015.
Dvornikov alihudumu kama kamanda wa kwanza wa jeshi la Urusi katika operesheni za nchi ya kiarabu, baada ya putin kutuma vikosi huko mwezi septemba 2015 , kuiunga mkono serikali ya rais wa Syria Bashar al - Assad.
Urusi ilimpatia Al-Assad, ambaye alikuwa anahofia kupinduliwa, msaada wa ndege za kijeshi na kumsaidia kumaliza vita lakini kwa kwa garama kubwa.
Chini ya amri ya Dvornikov, vikosi vya Urusi nchini Syria viliripotiwa kukabiliana na wenyeji na na kuangamiza miji kwa kupiga makombora, kutumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa yakiwemo mabomu.
Alipochukua uongozi, Dvornikov alianzisha haraka sana ngome ya majeshi ya anga karibu na mwambao wa Kusini mashariki mwa Syria na kutoka kule aliangamiza miji na jiji katika jimbo la Idlib.

Chanzo cha picha, Getty Images
Dvornikov alikuwa amehudumu kama kamanda wa wilaya ya la kusini la kijeshi nchini Urusi tangu mwaka 2016.
Ni kitengo cha kijeshi ambacho kinajumuisha jimbo la Crimea tangu lilipotwaliwa na Urusi katika mwaka 2014
Kulingana na wataalamu, kazi hii ilimpa Dvornikov uelewa mzuri wa jimbo la Donbas, ambalo limekuwa kipaumbele cha Moscow tangu ilipoondoka kutoka Kyiv
"Utakua ni uanzishaji mwingine wa uhalifu''

Chanzo cha picha, Getty Images
Msemaji wa Putin, Dmitry Peskov, alisema wiki iliyopita kwamba kushindwa kwa Urusi kulikuwa ni "janga kubwa."
"Na marekani , kama nilivyosema awali, imeazimia kufanya kila liwezekanalo kuwaunga mkono Waukraine wanapomkataa yeye na vikosi anavyoviongoza."
Ijumaa iliyopita, Urusi ilikuri kuumia kutokana na "kupoteza eneo kwa vikosi vyake " katika Ukraine, huku uvamizi huo ukiingia siku ya 44.
Majeruhi wa Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia alisema kuwa anamatumaini kuwa Moscow itafanikiwa malengo yake ya vita "katika siku zijazo."
Kauli ya za Peskov zilikuja baada ya urusi kuondolewa katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa siku ya alhamisi.
Kukiri kwake kwamba Urusi imepata majeruhi wengi kuliwashangaza wengi.
Tarehe 25 machi, Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa 1,351 ya wanajeshi wake wameuawa katika mapigano, lakini Ukraine ilisema kuwa idadi ya vifo ilikuwa takriban wanajeshi 19,000.
Makadirio ya Urusi na Ukraine hayawezi kuhakikishwa na duru huru, na wachambuzi wameonya kwamba Urusi inadanganya kuhusu viwango vya waathiriwa, huku Ukraine huenda ikitaja idadi hizo kwa lengo la kuwatia moyo wanajeshi wake.
Viongozi wa magharibi wanaamini baina ya wanajeshi 7,000 na 15,000 wa Urusi wameuawa tangu mwanzoni mwa vita.
Unaweza pia kusoma:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine












