Vita vya Ukraine: Fahamu ongezeko la bei ya bidhaa linavyoathiri Ramadhani

Sudanese men sit together as they are served Iftar at sunset during the Muslim holy month of Ramadan, at their protest outside the army headquarters in Sudan - 10 May 2019

Chanzo cha picha, AFP

    • Author, Issa Ahmed
    • Nafasi, BBC Business

Ramadhan ni mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu. Mwezi huo mzima waumnii hujinyima kula na kunywa kuanzia macheo hadi machweo.

Baada ya kuzuka kwa vita vya Urusi na Ukraine mnamo Februari 24, 2022, mzozo wa usalama wa chakula barani Afrika sasa unaleta tishio kwa uchumi wake.

Hali tete ya usalama wa chakula katika mabara inatokana na sekta ya kilimo kutokuwa na uwezo wa kuzalisha nafaka za kutosha, hasa ngano, na mbegu za mafuta kukidhi walau nusu ya mahitaji ya ndani ya Afŕika.

Kwa mfano Cairo inategemea kiasi kikubwa cha uagizaji wa ruzuku kutoka nje ili kuhakikisha usambazaji wa kutosha na wa bei nafuu wa mkate na mafuta ya kupikia kwa raia wake milioni 105. Kupata bidhaa hizo kumeifanya Misri kuwa nchi inayoagiza ngano kutoka nje na miongoni mwa waagizaji 10 wakubwa wa mafuta ya alizeti duniani.

Huku Urusi ikiwa muuzaji mkubwa wa ngano duniani na Ukraine ikiwa ya tano kwa ukubwa, ikichukua jumla ya 30% ya mauzo ya nje ya ngano duniani, bei zinaweza kuendelea kuwa juu kipindi hiki cha vita.

Waislamu kote Barani Afrika wanahofia vita hivyovitaathiri mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Wakati wa Ramadhani milo miwili mikuu huliwa, suhoor(daku) ambayo huliwa kabla ya alfajiri, na iftar(futari) ambayo huliwa baada ya jua kuzama.

Suhoor inatakiwa kuwa chakula cha afya ambacho kinampa mtu nguvu ya kuhimili makali njaa siku nzima — mwisho wake kuliwa ni kabla ya sala ya afajiri. Waislamu hutumia ngano kwa wingi kwa sababu ni nyepesi na haimfanyi mtu kuvimbiwa.

Ngano

A wheat field situated in eastern Ukraine

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashamba ya ngano ya Ukrainia hulisha mamilioni ya watu katika Mashariki ya Kati

Bei ya vyakula imekuwa ikiongezeka kuanzia mwaka 2021 kote duniani kutokana na kutokana athari zinazohusiana na janga la Covid-19, hali ambayo huenda ikawa mbaya zaidi ikiwa usafirishaji wa chakula kutoka Urusi na Ukraine utatatizwa na vita.

Nchi hizo mbili ni miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa uzalishaji wa bidhaa kuu zikiwemo mafuta na gesi, ngano na mafuta ya alizeti, ikimaanisha kwamba usumbufu wowote wa usambazaji unaweza kuathiri uchumi wa dunia.

Ngano, ambayo Urusi na Ukraine hutoa takriban 30% ya pato la kimataifa, imeathiriwa zaidi. Siku ya Jumanne, bei ya ngano ilipanda hadi kiwango cha juu zaidi kilichowahi kufikiwa tangu 2008, hali ambayo inaashiria uwezekano wa nchi zinazotegemea uagizaji bidhaa ikiwa ni pamoja na Misri kuathirika.

Kulingana na Mamlaka Kuu ya Bidhaa za Ugavi wa Misri (GASC) Urusi ilitoa takriban 50% ya ngano iliyoagizwa nchini Misri mwaka 2021, wakati Ukraine ilikidhi asilimia 30 ya mahitaji ya nafaka nchini humo.

Misri sasa italazimika kutafuta bidha hiyo kutoka sehemu mbadala, lakini huenda ikakosa kukidhi mahitaji ya juu ya uagizaji wa bidhaa nchini humo, kumaanisha kwamba bei za bidhaa kuu zinaweza kupanda zaidi, na kuathiri mapato ya watu katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Mafuta ya alizeti

Alizeti

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alizeti

Kando na ngano na unga wa mahindi, smafuta ya alizeti inasalia kuwa moja ya bidhaa muhimu inayoagizwa kutoka Ukraine hadi Afrika. Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unapoendela, Misri kwa mfano inategemea Ukraine na Urusi kwa sababu sehemu kubwa ya mafuta yake ya alizeti na mzozo unaoendelea kati ya nchi hizo mbili unaweza kufanya bei ya mafuta ya kupikia kupanda na kuongeza shinikizo lililopo kwa bei za vyakula nchini humo.

Kutokuwa na uhakika juu ya usambazaji wa mafuta ya alizeti kabla na wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tayari kumesababisha mahitaji ya mafuta mengine ya kupikia kama vile mawese kupanda kwa kiasi kikubwa badala yake.

Kwa mfano mafuta ya kupikia ya Kenya Watengenezaji wanapambana kuhumili gharama ya kuagiza mawese kutoka Indonesia na Malaysia.

Mtengenezaji mmoja wa aina hiyo kutoka Kenya ni Billow Aden Kerrow ambaye anasema kwamba usambazaji wa mafuta ya kupikia hautakidhi mahitaji katika mwezi wa Ramadhani ikiwa serikali hazitachukua hatua zinazofaa.

"Nadhani athari kwa Ramadhani na Jumuiya ya Kiislamu itakuwa kubwa sana,, itaathiri kila mtu kwa sababu nchi hizi mbili kwa pamoja zitazalisha 1/3 ya ngano, pia huzalisha 75% ya mafuta ya alizeti duniani'' anasema billow.

TH

Aliongeza kuwa ''Nitakupa mfano wa mafuta ya alizeti madhara yake tunayaona sisi wenyewe, tupo katika biashara ya kutengeneza mafuta yakupikia, tunaagiza mafuta ghafi ya mawese kutoka Indonesia na Malaysia, nini kimetokea huko nyuma. wiki moja pekee bei ya mafuta ghafi ya mawese imepanda kwa zaidi ya dola 500 hadi dola 1500 za Kimarekani tani hadi dola 2200 kwa tani na inaendelea kupanda.

Kwa ufupi mtungi wa lita 20ya mafuta ya kupikia ambayo tulikuwa tunauza karibu dola 40 sasa yanauzwa kwa dola 78 na yanakaribia kufikia dola 80 mwezi wa Ramadhani''.

Alipoulizwa kuhusu nchi za Kiafrika zinaweza kufanya nini ili kuongeza uzalishaji wao alisema ''Nitakuambia ni nchi gani duniani zinafanya kama vile India ambayo ni mlaji mkubwa wa mafuta ya kupikia ili kufanya vitu kuwa bei nafuu zaidi wameondoa baadhi ya majukumu au kodi.

Nchini Kenya mafuta ya kupikia inatozwa ushuru wa forodha wa hadi asilimia asilimia tatu na mafuta ghafi ya pal yanatozwa ushuru wa zaida VAT ya 16% kwenye mafuta ghafi tunayoagiza kutoka nje, kwa hivyo kuna haja ya serikali kuwekeza kwenye usalama wa chakula ambao umekuwa ukiyumba katika baadhi ya maeneo ya Afrika hasa nchini Kenya.

TH

Chanzo cha picha, Habarileo

Hii ni nafasi kwa nchi kama Nigeria kuchukua fursa ya uhaba wa usambazaji kwenye soko. Mnamo 2020, tani milioni 73 za mafuta ya mawese zilitumiwa kote duniani , lakini Nigeria ilichangia tani milioni 1.2 au asilimia mbili ya Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA).

Maelezo zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine: