Mzozo wa Ukraine: Marekani inapeleka silaha gani Ukraine na kwa kiasi gani zinawasaidia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabaki ya vifaru Urusi yamezagaa kama uchafu, wakati katika moja picha inamuonyesha, mwanajeshi wa Ukraine kabeba silaha zinazosemekana kusababisha uharibifu huo.
Picha zilizotumwa kwenye mtandao wa Twitter na Jeshi la Ukraine zinazoonekana kama ushindi, zikitangaza kuwa hii ni matokeo ya "pigo la (silaha) Javelins kwenye vifaa vya kijeshi vya Urusi".
Javelin, silaha ya kukabiliana na vifaru ya kubebwa begani ambayo inauwezo wa kwenda mbali hadi kilometa 4 (maili 2.5).
Uwepo wa silaha za aina hii zilizotengenezwa na Marekani "zimeleta hofu" kati ya majeshi ya Urusi, na kwa mujibu wa madai ya kijeshi ya Ukraine - inakaribia kupata zaidi ya silaha hizo 2,000.
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Makombora ya Javelin ni miongoni mwa vitu vilivyoahidiwa na Marekani kupeleka Ukraine katika mpango mpya wa msaada wa kijeshi wadola $800m uliotangazwa na Rais Joe Biden siku ya Jumatano.
Silaha nyingine ni pamoja na ndege zisizo na rubani ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa mabomu ya kuruka na silaha za kupambana na ndege ambazo zinaweza kupiga helikopta kutoka angani.
Lakini silaha hizi zitaisaidia Ukraine kushinda nguvu nyingi zaidi za Urusi - yenye vifaa bora - na nguvu ya uvamizi?
Je Marekani itapeleka nini Ukraine?
Msaada mpya wa Marekani kwa Ukraine unahusisha vifaa mbalimbali vya kijeshi, kuanzia seti 25,000 za silaha za mwili, helmeti, bunduki, maguruneti, maelfu ya silaha nyingine za kupambana na vifaru na mabomu.
Mbali na makombora ya Javelin, silaha zenye nguvu zaidi ni pamoja na mifumo 800 ya kupambana na ndege za Stinger, ambayo iliwahi kutumia kutungua ndege za Soviet nchini Afghanistan.
Marekani pia ina mpango wa kupeleka "ndege ndogo zisizo na rubani - ambazo hurushwa kwa mkono na ni ndogo kutosha kupenya popote.
Askari wanaweza kuzitumia kushambulia wakiwa nje ya uwanja wa vita, kimsingi ni kushambulia kwa mbali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangazo la Bwana Biden siku ya Jumatano linafikisha jumla ya kiasi cha msaada wa kijeshi wa Marekani ulioahidiwa kwa Ukraine hadi dola bilioni 1 katika kipindi cha wiki moja pekee iliyopita - ukiwa ni msaada mkubwa wa haraka ikilinganishwa na dola bilioni 2.7 zilizotolewa kati ya mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka 2022.
Ni "hatua muhimu" na inashughulikia mapungufu ya awali, kwa mujibu wa John Herbst, balozi wa zamani wa Marekani huko Kyiv.
Hatua hii inamaanisha nini dhidi ya mashambulizi ya ardhini na angani ya Urusi?
Wataalamu wa kijeshi wanasema kuwa silaha za kupambana na vifaru zinazosambazwa na Marekani zinaweza kuwa na athari kubwa zaidi nchini Ukraine.
Vikosi vya Urusi vilivyovamia Ukraine "kimsingi ni vikosi vya mitambo" - ikimaanisha misafara ya silaha - kwa hivyo "jambo bora zaidi unaweza kufanya ni kushambulia [vifaa au magari] yao", alisema Kanali wa zamani wa Jeshi la Marekani Christopher Mayer.
Ukraine imekuwa ikipokea vifaa na mifumo mbalimbali ya kupambana na vifaru kutoka nchi mbalimbali, ambayo vinasaidia Ukraine kusambaratisha magari ya Urusi, Bwana Mayer alisema.
Ingawa madai yao hayajaweza kuthibitisha, maafisa wa Ukraine wanasema vifaa hivyo vimesaidia kusambaratisha vifaa vya Urusi. Kufikia Machi 16, wanadai kuwa waliharibu zaidi ya vifaru 400 na magari mengine zaidi ya 2,000 ya Urusi.
Silaha za kupambana na vifaru, hata hivyo, haziisaidii chochote Ukraine kupambana na jeshi la anga la Urusi, ambalo kwa wiki tatu limekuwa likishambulia maeneo kote nchini humo.
Stinger, silaha ya begani ni silaha pekee ya kupambana na ndege iliyojumuishwa katika mpango wa misaada ya Marekani kwa Ukraine.
Silaha hizi za begani zina ufanisi dhidi ya helikopta au ndege zinazoruka kwenye anga la chini la hadi karibu 3,800m (12,400ft), hilo linaifanya kuwa silaha isiyo na madhara kwa ndege zinazoruka juu ya urefu huo za Urusi.
Bwana Herbst alisema "Wanahitaji stingers zaidi, hakuna shaka juu ya hilo," alisema. "Lakini wanahitaji silaha za hali ya juu zaidi kupambana na ndegea ... Huku ni kuachwa kwenye mataa."
Marekani haijatuma ujumbe gani?
Wakati Ikulu ya White House imedokeza kuwa silaha za kwenda urefu wa juu zaidi - kama vile kombora la enzi ya Sovieti la S-300 - zinaweza kupelekwa Ukraine kupitia nchi nyingine, hakuna tangazo rasmi lililotolewa.
Maafisa nchini Slovakia wameonyesha nia ya kupeleka mifumo hiyo kwa Ukraine, ikiwa watapata mbadala. Washirika wengine wawili wa Nato - Ugiriki na Bulgaria - pia waliripotiwa kuwa na mifumo hiyo.
Marekani pia imetupilia mbali mapendekezo ya kuitaka Poland kupeleka ndege zake za kivita aina ya Mig-29 kwenda Ukraine ili kuwasaidia zaidi kwenye mapambano anga.
Maafisa wa Marekani wameelezea mpango huo kuwa "hauwezekani" kutokana na kuongezeka kwa hatari ya mgogoro wa wazi kati ya Nato na Urusi.
Bwana Mayer, hata hivyo, alisema kuwa kupelekwa kwa ndege za Mig-29 au sza aina hiyo na washirika wa Marekani - kwa baraka za utawala - itakuwa njia bora zaidi ya kuisaidia Ukraine kupigania udhibiti wa anga zake.
Nchi nyingine zimechukua hatua gani?
Marekani haiko peke yake katika kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Angalau nchi nyingine 30 zimetoa msaada, ikiwa ni pamoja na € 500m kutoka Umoja wa Ulaya, jambo la kihistoria.
Baada ya Marekani kutangaza msaada huo mpya, Hata hivyo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kuwa "msaada zaidi" unahitajika haraka.
"Hata tunavyoendelea kupokea sasa," alisema, na kutoa wito zaidi kwa "mifumo ya ulinzi wa hewa, ndege [na] silaha za kutosha za hatari na risasi ili kuwazuia wavamizi wa Urusi".
Bwana Mayer alisema anaamini kwamba vifaa vya silaha vya Marekani vilivyoahidiwa hadi sasa huenda vinatosha tu kuruhusu Wa-Ukrani "kufa kishujaa".

Chanzo cha picha, Getty Images
Herbst alisema kuwa misaada ya ziada zaidi "huenda" itahitajika katika siku zijazo - na kwamba watakuwa na ufanisi tu ikiwa wataisaidia Ukraine kupambana na jeshi la anga la Urusi.
"Kitu muhimu kwangu ni kama tunatuma kitu ambacho kinakwenda kushambulia vifaa vya Urusi angaani kwa futi 30,000 au zaidi," alisema.
Wakati hakuna tangazo rasmi lilitolewa hadi sasa, Rais Biden aliapa kwamba msaada zaidi utakuwa njiani - na kwamba Marekani inafanya kazi kusaidia Ukraine kupata mifumo ya ulinzi wa angani ya muda mrefu inayohitaji, bila kutoa maelezo.
"Wengine zaidi watakwenda," alisema.












