Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
"Watu wa Ukraine wanazitaka nchi za Magharibi kulinda anga letu, huku wakionekana kukata tamaa. Tunaomba kuwe na - no-fly zone."
Hili lilikuwa ni ombi la shauku kutoka kwa mwanamke Mukraine ambaye alimkabili Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mkutano na waandishi wa habarti Jumanne.
"Wanawake wa Ukraine na watoto wa Ukraine wana hofu kubwa kwasababu ya mabomu na makombora ambayo yanakuja kutoka angani ," Daria Kaleniuk alisema.
Lakini licha ya mashambulio ya anga ya Urusi kupiga maeneo ya Ukraine, na kuongezeka kwa idadi ya vifo vya raia, kuna ishara kidogo kwamba nchi za Magharibi zitatekeleza mpango wa kuweka no-fly zone. Hii ndio sababu.
No-fly zones ni nini ?
N-fly zone inamaanisha eneo lolote la anga ambalo limetengwa kwamba aina fulani ya ndge haiwezi kupaa.
Eneo kama hili linaweza kutumiwa kulinda maeneo nyeti, kama vile mazai ya kifalme, au kuwekwa kwa muda mfupi kwasababu ya matukio ya michezo na mikusanyiko mikubwa.
Katika dhana ya kijeshi, no-fly zone huundwa ili kuzuwia ndege kuingia eneo la anga lililowekewa marufuku mara nyingi lemngo likiwa ni kusuwia mashambulizi au ujasusi.
Lazima liwekwe kwa njia za kijeshi.
Hilo linaweza kuwa ufuatiliaji, kutokana na mashambulio yanayotarajiwa dhidi ya mifumo ya ulinzi au kuangusha ndege ambayo inaingia katika eneo lililozuiwa.
Kuweka No-fly zone juu ya Ukraine kutamaanisha kwamba vikosi vya kijeshi -hususan vikosi vya Nato - vitahusika moja kwa moja na ndege zozote za Urusi katika anga hizo na kuzilenga kama itahitajika kufanya hivyo.
Kwanini nchi za Magharibi haziwezi kuanzisha eneo hilo katika Ukraine?
Matumizi ya ndege za kivita ya vikosi vya Urusi au silaha yanasababisha hatari ya kuongezeka kwa vita.
"Huwezi kusema tu kwamba 'hilo ni eneo la no-fly zone'. Lazima utekeleze no-fly zone," Jenerali wa zamani wa kikosi cha anga cha jeshi la Marekani jenerali Philip Breedlove aliliambia jarida la Foreign Policy
Jenerali huyo, ambaye alihudumu kama kamanda mkuu wa ngazi ya juu wa muungano wa Nato kuanzia mwaka 2013 hadi 2016, alisema kwamba huku akiunga mkono miito ya kuwekwa kwa no-fly zone nchini Ukraine, ni uamuzi mgumu sana kuuchukua.
"Ni sawa na vita. Kama tungekuwa tumetangaza no-fly zone, tungepaswa kumaliza uwezo wa adui kwa kufyatua ndani na kuathiri eneo letu la no-fly zone."
Waziri mkuu wa uingereza Tobias Ellwood, ambaye ndie mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi, ameunga mkono wazo la eneo la ieneo kamili la - no-fly zone, na kutoa wito kwa Nato wa kuingilia kati kutokana na vifo vya rai ana madai ya uhalifu wa kivita.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA: Wanajeshi wa Urusi wanaotumia parachuti waishambua Kharkiv
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Lakini katibu mkuu wa muungano wa Nato Jenerali Jens Stoltenberg alikataa uhusika wa shirika hilo, aliiambia NBC Jumatatu: "Hatuna nia ya kuingia ndani ya Ukraine, iwe ardhini au angani ."
Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ameeleza wazi kwamba Uingereza haitasaidia utekelezaji wa no-fly zone juu ya Ukraine kwasababu mapigano ya jeti za vita za Urusi yanaweza kusababisha "vita kote Ulaya".
Akizungumza na kipindi cha BBC Radio 4 Today, alisema: "Siwezi kusababisha vita ya Ulaya, lakini kile nitakachofanya ni kusaidia Ukraine kupigana kila mtaa na kila aina ya zana tunazoweza kuwapatia, na tutawasaidia."
Na Marekani pia haitafanya hili, kwa sababu sawa na zetu.
Hatari ya ziada ya ongezeko zaidi la mzozo na Urusi ni matumizi ya silaha za nyuklia. Hofu hiyo inakuja baada ya tangazo la Rais wa Urusi Vladimir Putin kwamba ameweka vikosi ''maalumu'' katika hali ya tahadhari.
Wengi wametafsiri hatua yake kimsingi kama aina ya kiashiria kwa umma, zaidi ya kuashiria lengo halisi la kutumia silaha za aina hiyo.
Je no-fly zones iliwahi kutumiwa kabla?
Baada ya Vita ya kwanza ya Ghuba katika mwaka 1991 marekani na washirika wake walianzisha maeneo mawili ya no-fly zones nchini Iraq kuzuwia mahsambulio dhidi ya kabila na makundi ya kidini. Eneo hili liliwekwa bila kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Katika mwaka 1992 wakati wa mzozo wa Balkans, Marekani ilipitisha azimio ambalo linazuwia ndege za kijeshi ambazo hazijaidhinishwa katika Bosnia.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia liliidhinisha eneo la no fly-zone kama sehemu ya uingiliaji kati wa kijeshi wa mwaka 2011 nchini Libya.
Maeneo ya Wabosnia na Libya yalitekelezwa na vikosi vya Nato.