Taarifa ya kifo: Lata Mangeshkar, muimbaji wa Bollywood aliyeimba wimbo wa Kiswahili afariki akiwa na umri wa miaka 92

Lata Mangeshkar, ambaye amefariki mjiniMumbai akiw ana umri wa miaka 92, alikuwa ni mwakilishi wa utamaduni ambaye alitengeneza jina lake katika Bollywood -licha ya kuonekana katika filamu chache tu.

Nyota yake iling'aa na kumfanya awe maarufu katika sekta ya filamu inayokuwa kama "mwimbaji anayeimba nyimbo za filamu", sauti yake ikisikika na kuigizwa na wacheza filamu nyota wa Bollywood - kazi aliyoifanya kwa zaidi ya nusu karne.

Kwa miongo Lata Mangeshkar ambaye alifananishwa na "ndege wa usiku wa Bollywood" alikuwa ni mwimbaji ambaye alipendwa na kutafutwa na wengi zaidi, huku waigizaji wengi wakitaka aimbe nyimbo zao. Rekodi zake wakati huo huo, ziliuzwa makumi ya maelfu, na aliimba nyimbo zipatazo 30,000 akiimba kwa mitindo mbali mbali na katika jumla ya lugha ya 36.

Lakini pia likuwa ni zaidi ya sauti yake. Mangeshkar alikuwa ni shabiki suku wa kriketi na alikuwa na mapenzi ya kipekee ya magari na mashine za Vegas. Pia alikuwa karibu sana baadhi ya nyota wenye vipaji zaidi wa Bollywood .

'Alithaminiwa kwa kiasi kikubwa'

Lata Mangeshkar alizaliwa katika mji wa kati mwa India wa Indore tarehe 28 Septemba 1929. Baba yake alikuwa muimbaji, mwigizaji wa maigizo na mzalishaji wa muziki uliochezwa kwa lugha ya Marathi.

Alikuwa ni mtoto mkubwa kati ya Watoto watano, huku ndugu zake wakifuata nyayo zake na pia kuwa waimbaji maarufu nchini India.

Maisha yalikuwa magumu wakati baba alipopoteza pes ana kufunga kampuni yake ya filamu na maigizo . familia ilihamia katika mji wa magharibi wa Poona (sasa ukiitwa Pune) baada ya nyumba ya familia katika Sangli I katika jimbo la Maharashtra kupigwa mnada na taifa.

Baada ya kifo cha baba yake , familia yake ilihamia (baadaye iliitwa jina Mumbai).

'Mimi sio muoga '

Bollywood ilikuwa inaingia kipindi chake cha dhahabu, na Mangeshkar walikuwa mahala sawa katika wakati unaofaa. Kwa miongo minne iliyofuata, aliimba nyimbo zinazokumbukwa na nyimbo maarufu katika filamu za nyota wa filamu kama vile Pakeezah, Majboor, Awaara, Mughal e Zam, Shree 420, Aradhana and Dilwale Dulhania Le Jayenge, ambazo zilivunja rekodi kwa miaka 20 .

Lata Mangheskar alikuwa ni Muhindi wa kwanza kuimba katika ukumbi wa Royal Albert Hall alipoimba wimbo Ye Mere Watan ke Logon (Ye watu wa ardhi yangu),

Mangeshkar alikuwa jasiri kiasi cha kukabiliana na waimbaji wa ngazi ya juu wanaume kama vile, Mohammand Rafi, alipata sifa mara kadhaa, na alikuwa mwanamke wa kwanzaambaye alidai malipo bora.

"Mimi ni mtu aliyejijenga. Nimejifunza jinsi ya kupambana. Sijawahi kumuogopa hata mmoja. Mimi sina uoga. Lakini nimekuwa daima nikifikiria ninaweza kupata kile nilicho nacho ," aliwahi kusema wakati mmoja