Wafahamu baadhi ya viongozi wa dunia wanaotetea Uislamu licha ya kutokuwa Waislamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Justin Trudeau waziri mkuu wa Canada
Waziri mkuu wa Pakistan anasema atavipa kipaumbele vita dhidi chuki dhidi ya Uislamu. Rais Imran Khan hutumia akaunti yake ya Twitter na hotuba zake kupambana na maoni dhidi ya Uislamu .
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na malalamiko ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu, hususan katika mataifa ya magharibi.
Katika baadhi ya maeneo , Waislamu wamekuwa wakiangaliwa kama magaidi.
Hatahivyo, kuna viongozi wengi ambao sio Waislamu ambao wamekuwa wakiwatetea Waislamu na Uislamu, wakiwemo viongozi wenye nguvu duniani.
Wafuatao ni baadhi ya vongozi wa dunia ambao sio Waislamu ambao wamekuwa wakiwalinda Waislamu dhidi ya chuki dhidi ya Uislamu.

Chanzo cha picha, Reuters
Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Canada Trudeau ni mmoja wa viongozi kadhaa wa Magharibi ambaye amepinga wazi chuki dhidi ya Uislamu.
Mwaka 2020 Trudeau alisema kwamba chuki dhidi ya Uislamu "haikubaliki" na aliapa kuhakikisha nchi yake ni salama kwa waislamu.
"Bila shaka chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi havina nafasi katika Canada," alisema Trudeau.
Aliongeza kuwa, " Tnahitaji kumaliza chuki hii na kuifanya jamii yetu kuwa ya amani na Waislamu nchini Canada."
Alikuwa akizungumza baada ya shambulio dhidi ya msikiti katika mji wa Quebec nchini humo.
JacindaArdern

Chanzo cha picha, Getty Images
Shambulio la vifo katika msikiti katika Christchurch, New Zealand, liliwashitua wengi.
Lakini jibu kutoka kwa Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern lilisifiwa kwa kiasi kikubwa. Bi Ardern alionyesha huruma kwa Waislamu wan chi hiyo na kuelezea kusikitishwa san ana kile kilichotokea.
Alivaa hijabu alipokutana na Waislamu na akasema washambuliaji hawakutoka New Zealand. Shambulio katika msikiti wa Christchurch liliwauwa waumini wa Kiislamu 50 katika msikiti.

Chanzo cha picha, Reuters
Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin ni mmoja wa viongozi ambao sio Waislamu ambaye amesikika mara kwa mara kuwalinda Waislamu.
Hupinga vikali matusi dhidi ya Mtume Muhammad (sws) na chuki dhidi ya Uislamu.
Katika hotuba aliyoitoa mwezi Disemba mwaja jana, Rais Putin alisema kwamba matusi dhidi ya Mtume Muhammad hayawezi kuelezewa "uhuru wa kujieleza".
Kumtusi Mtume Muhammad ni "ukiukaji wa uhuru wa kidini na kukiuka utakatifu wa Waislamu," aliongeza.
Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images
Barack Obama
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama pia alizungumza wazi dhidi ya chuki dhidi ya waislamu wakati alipokuwa madarakani kama rais.
Aliwalinda Waislamu nchini Marekani dhidi ya ubaguzi wa kidini.
Aliwatolea wito Wamarekani wakati ule kupambana dhidi ya chuki kwa Waislamu
"Waislamu nchini Marekani ni Rafiki zetu, wafanyakazi wenzetu, mashujaa wetu wa michezo-na ndio, ni wanawake na wanaume katika jeshi letu ," alisema Obama.












