Ufahamu mji wa kipekee unaosimamiwa na viongozi Waislamu nchini Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukitembea kwenye mtaa mkuu wa mji wa Hamtramck huko Michigan nchini Marekani unahisi kama unafanya ziara ya dunia nzima.
Duka la soseji na duka la kuoka mikate kutoka Mashariki mwa Ulaya likiwa kando na duka la Yemen kando na duka la nguo la Bengali.
Kengele za kanisa zinalia sambamba na adhana.
"Ni dunia ndani ya maili mbili mraba" - Hamtramck unaishi kwa kauli mbiu yake, ukiwa na karibu lugha 30 zinazozungumzwa ndani ya ukubwa wa kilomita tano mraba.
Mwezi huu mji huo wenye wakaazi 28,000 umefikia hatua muhimu. Hamtramck umechagua baraza la mji lenye Waislamu tupu na meya Muislamu na kuwa mji wa kwanza nchini Marekani kuwa na serikali ya Wamarekani wenye asili ya kiislamu.
Baada ya kutengwa, wakazi wa Waislamu wamekuwa wenye umihumu kwenye mji huu wenye tamaduni nyingi na sasa idadi yao ni zaidi ya nusu ya mji huu.
Licha ya changamoto za kiuchumi na mijadala mikali ya kitamaduni, wakazi wa Hamtramck kutoka dini na tamaduni tofauti wanaishi kwa amani na kuufanya mji huo kuwa mfano bora wa Amerika ya siku za baadaye yenye muingiliano.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hamtramck una historia ya mji wa walowezi wa Kijerumani hadi mji wa kisasa - ulikuwa mji wa kwanza wenye Waislamu wengi nchini Marekani.
Maduka yanaonyesha alama za kiarabu na Kibengali, mavazi ya kutoka Bangladesh na Jambiya, kifaa kutoka nchini Yemen vinaonekana kwenye madirisha ya maduka.

Katika Karne ya 20 ulijulikana kama Warsaw ndogo, wakati wahamiaji kutoka Poland walimiminika kutafuta ajira. Mji huo ulikuwa kati ya ile aliyotembea Papa John Paul II wakati alifanya ziara nchini Marekani mwaka 1987. Mwaka 1970 asiliamia 90 ya mji huo ulikuwa na watu wa asili ya Poland.
Hata hivyo mwongo huo ulishuhudia kudorora kwa sekta ya utengenezaji magari nchini Marekani, watu matajiri walianza kuhamia vitongoji vya mji. Mabadiliko hayo yalifanya Hamtramck kuwa mmoja wa miji maskini zaidi huko Michigan lakini unafuu wake uliwavutia wahamiaji.

Chanzo cha picha, Courtesy of Amanda Jaczkowski
Kwa muda wa miaka 30, Hamtramck ulibadilika tena na kuwa chaguo la wahamiaji kwa nchi za Kiarabu na Asia hasa wale kutoka Yemen na Bangladesh. Asilimia 42 ya wakaazi wa mji huo leo hii ni wazaliwa wa nchi za kigeni, zaidi ya nusu wanaaminiwa kuwa Waislamu.
Serikali mpya iliyochaguliwa inaashiria mabadiliko mjini humo. Baraza la mji litawajumuisha watu wawili wenye asilii ya Bengali, watatu wenye asili ya Yemen na mmoja mwenye asili ya Poland aliyebadili dini na kuwa Muislamu.
Baada ya kuibuka mshindi kwa asilimi 68 ya kura Amer Ghalib atakuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya Yemen kuwa meya nchini Marekani.
"Najiskia kuheshimiwa lakini ninajua nina wajibu mkubwa," Bw Ghalib 41, alisema. Mzaliwa wa kijiji kimoja nchini Yemen alihamia Marekani akiwa na umri wa miaka 17 alikoanza kufanya kazi kwenye kiwanda cha kuunda vipuri vya magari karibu na Hamtramck. Kisha akajifunza kiingereza na kupata mafunzo ya uuguzi na sasa anafanya kazi kama mtaalamu wa masuala ya afya.
Badala ya kuwa sufuria ya kuyeyusha, Hamtramck sasa ni zaidi ya keki ya tabaka saba ambapo makundi tofauti yanajuimisha tamaduni zao na kuishi kwa amani.
Lakini Hamtramck sio Disneyland, anasema Karen Majewski, meya anayeondoka ambaye angehudumu kwa miaka 15 kabla ya kung'atuka. "Ni eneo dogo, na huwa tunazozana."

Chanzo cha picha, Getty Images
Mzozo uliibuka mwaka 2004 kufuatia kura ya kutangazwa kwa sauti ya adhana. Baadhi ya wakaazi walidai kuwa marufuku kwa baa karibu na misiikiti itaathiri uchumi wa mji.
Miaka sita iliyopita wakati ulikuwa mji wa kwanza nchini Marekani kuchagua serikali yenye waislamu wengi, vyombo vya habari kutoka kote duniani viliwasili Hamtramck. Baadhi ya vyombo vya habari vilionyesha mji wenye mvutano wenye waislamu wengi,
Nchini Marekani ofisi ya sensa haikusanyi data kuhusu dini. Lakini kituo cha utafiti cha Pew kinakadiria kuwa kulikuwa na takriban waislamu milioni 3.85 wanaoishi nchini Marekani mwaka 2020 ikiwa ni asilimia 1.1 ya watu wote.
Ifikapo mwaka 2040 waislamu wanatarajiwa kuwa dini ya piliakwa ukubwa nchini Marekani baada ya ile ya kikiristo.
Licha ya kuendelea kuongezeka, waisalmu wanaoishi nchini Marekani wamekumbwa na ubaguzi.
Miaka 20 baada ya shambulizi la Septemba 11, bado kuna chuki dhidi ya waislamu wamarekani wengi wenye asili ya kiarabu. Karibu nusu ya waislamu watu wazima walikiambia kituo cha Pew mwaka 2016 kuwa wamekumbwa na namna fulani ya ubaguzi wakati mgombea wa urais Donald Trump alipendekeza wahamiaji kutoka nchi za kiislamu kuzuiwa kuingia Marekani.
Zaidi ya nusu ya raia wa Marekani wanasema hawamjui mwislamu yeyote lakini wale wanawajua wanaamini kuwa uislamu unatetea ghasia kuliko dini zingine.

Mwaka 2017 wakati uongozi wa Trump ulitangaza marufuku, wakaazi walikuja pamoja kuandamana.
"Kwa njia fulania iliwakusanya na kuwaleta watu pamoja kwa sababu kila mmoja anajua kuwa ili kuishi Hamtramck ni lazima uheshimi watu wengine,
Kitaifa waislamu nchini Marekani wamepata nafasi katika siasa nchini Marekani. Mwaka 2017, Mudemokrati kutoka Minnesota Keith Ellison alichaguliwa kuwa mbunge wa kwanza muislamu, Bunge la sasa la Congress nchini Marekani lina wanachama wanne waislamu.
Wakati wa siku ya kura huko Hamtramck, wakaazi kadhaa walikusanyika mbele ya kituo cha kupiga kura kusalimiana, wengine wakionyesha ishara za kuonyesha kuwa wamepiga kura.
Wahamiaji walifurahia kishiki demokrasia, Bi Jaczkowski alisema. Ni kawaida kwa Amerika kuwaleta watu pamoja.
Hamtramck inakumbwa na changamoto zikiwemo kuzoroka kwa miundo msingi.
Mvua kubwa mzimu wa joto zililemea mifumo ya maji taka, maji yakafurika kwenye makazi ya watu. Viwango vya juu vya madini ya risasi kwenye maji ya kunywa mjini ilizua wasi wasi.
Karibu nusu ya watu wanaishi katika hali ya umaskini. Haya ni baadhi ya masuala uongozi mpya utahitaji kukabilana nayo.













