Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Everton yamtaka beki wa Arsenal Ben White

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanatazamia kumnunua beki wa Arsenal Muingereza Ben White, 28, ili kutatua tatizo lao la beki wa kulia. (Football Insider)
Borussia Dortmund wanafuatilia hali ya kiungo wa Norway Oscar Bobb, 22, Manchester City kufuatia kuwasili kwa winga wa Ghana Antoine Semenyo, 26. (Florian Plettenberg)
Tottenham inasalia na nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Uingereza Conor Gallagher, licha ya Aston Villa kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (TeamTalks)
End of Pia unaweza kusoma

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wanaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Newcastle United raia wa Denmark William Osula, 22, baada ya kupata pigo katika harakati zao za kumtafuta mshambuliaji wa Real Madrid wa Uhispania chini ya umri wa miaka 21 Gonzalo Garcia, 21. (Talksport)
Liverpool na Chelsea wamefurahishwa na beki wa kati wa klabu ya Como ya Uhispania chini ya umri wa miaka 21 Jacobo Ramon, huku klabu nyingine kadhaa za Premier pia zikituma maskauti kumtazama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (CaughtOffside)
Paris FC ni miongoni mwa kilabu zinazotaka kumsajili winga wa Ufaransa Mathys Tel kwa mkopo mwezi huu, lakini Tottenham wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 abaki. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkurugenzi wa michezo wa Tottenham, Fabio Paratici anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Serie A, Fiorentina baada ya dirisha la usajili la Januari. (Athletic - Subscription Required)
Beki wa kati wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, anatazamiwa kusalia Bayern Munich hadi 2031 baada ya kuondoa chaguo la kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Fichajes - In Spanish)














