Walio hai wanaoishi na wafu - hayo ndio maisha yao

mfu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alitengeeneza mtoto mfu katika Chinchorro. Anasemekana kuwa na umri wa miaka katika ya 6-7. Lakini sio watoto tu waliokufa wanaohifadhiwa, pia miili ya watu wazima

"Huenda ikaonekana kama jambo la ajabu kwa baadhi ya watu kuishi makaburini, lakini hilo ni jambo tulilolizoea ,"anasema Ana Maria Nieto, anayeishi katika mji wa bandari wa Chile unaoitwa Arika.

Mji wa Arica uko mpakani mwa Chile na Peru na juu ya mlima wa mchanga uliokusanywa na upepo ulipo katika jangwa la Atacam, eneo lenye ukame zaidi dunaini.

Lakini zamani kabla ya kujengwa kwa mji huo wa katika karne ya 16, eneo hili lilikuwa linakaliwa na watu wa jamii ya Chinchor.

Mamia ya wafu waliohifadhiwa wa jamii hii wamejumuishwa katika orodha ya hifadhi ya urithi ya dunia ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).

Wafu wa Chinchorro waliohifadhiwa kwa kutolewa viungo vya ndani ya mwili, kukaushwa na kufungwa walipatikana kwa mara ya kwanza katika mwaka 1917 na Mwanaakiolojia Mjerumani Max Ule, ambaye alipata miili iliyofichwa kwenye ufukwe. Lakini ilichukua miongo kadhaa kubaini umri wao.

Kipimo cha miaka waliyoishi wafu-Radiocarbon hatimaye kimefichua kuwa miili hiyo ya wafu iliyohifadhiwa iliishi miaka 7,000 ikiwa ni miaka elfu mbili zaidi ya wafu wa Misri.

Utamaduni wa Chinchilla

COURTESY UNIVERSITY OF TARAPACÁ

Chanzo cha picha, COURTESY UNIVERSITY OF TARAPACÁ

Kipindi cha kuanzia mwaka 7,000 BC hadi 1,500 BC

  • Wavuvi na wawindaji;
  • Kwa sasa Chile kaskazini na Kusini mwa Peru;
  • Walihifadhi miili ya wafua wao kwa kuondoa viungo vyao vya ndani, kuwakausha na kuwafunga katika bandeji njia iliyokuwa sahihi na ya kuwakumbuka
  • Inasemekana kuwa njia ya kuwahifadhi wafu baada ya kuondoa viungo vyao na kuwakausha na kuwafungia kwenye bandeji inayofahamika kama mummification -ilianza kama njia ya kutunza kumbukumbu hai ya mfu;

Hii iliifanya miili ya wafu wa Chinchorro kuwa ya zamani zaidi inayofahamika kwa ushahidi wa Wanaakiolojia iliyohifadhiwa kwa njia hiyo.

Kulingana na Bernardo Arias, Mwanaakiolojia na mtaalamu wa jamii ya Chinchorro, wafu hao (mummies) walitengenezwa kwa njia ya kipekee. Ingawa walitunzwa kwa njia za asili za kuwahifadhi maiti, waliwatengeneza kwa lengo la kuwatunza katika maeneo yenye hali kavu ya hewa isiyo na unyevunyevu.

Mwili ulikuwa unatobolewa, viungo vya ndani vinaondolewa, na wakati ngozi inapotoka, mashimo yalikuwa yanakauka, anaelezea, Arrias.

Wachinchorro walijaza maiti wanga asili na majani kabla ya kuipanda na mianzi.

Pia walifunika kichwa cha maiti na pamba nzito nyeusi, na kuifunika kwa tope uso wake na macho ya maiti na kuuziba mdomo kwa barakoa.

Wachinchorro pia walihifadhi miili ya watoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wachinchorro pia walihifadhi miili ya watoto
Walifunika nyuso za kwa barakoa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walifunika nyuso za kwa barakoa
Mmoja wa miili ya wafu wa kale alikuwa na nywele nyeusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mmoja wa miili ya wafu wa kale alikuwa na nywele nyeusi

Njia ya kuhifadhi miili ya wafu ya jamii ya Chinchorro ilikuwa ni tofauti na ile ya Wamisri, Bw Arrias alisema.

Wamisri walitumia tu Mafuta na nguo, lakini , kuwatunza maiti kwa njia ya kuondoa viungo vya ndani ilikuwa kuwa sio njia aliyohifadhiwa mfu yeyote, bali ni watu waliotoka katika familia tajiri au za wasomi, huku katika jamii ya Chinchorros, hawakujali nafasi aliyo nayo kati jamii, kulikuwa na wafu wanawake, wanaume na watoto wadogo, watoto wachanga,na hata vijusi waliohifadhiwa kwa njia hii.

Kuishi na wafu

Mamia ya wafu hawa (mummies) wamekuwa wakipatikana katika mji wa Arica na maeneo mengine katika karne iliyopita. Wenyeji wamezoea kuishi kando yao, mara nyingi wakiishi na masalia ya miili hii.

Kwa vizazi, wenyeji wamekuwa wakishuhudia uvumbuzi wa masalia ya miili wakati wa ujenzi wa nyumba au mbwa wakila sehemu ya maiti. Lakini kwa muda mrefu hawakuelewa umuhimu wa masalia haya ya miili.

"Wakati mwingine watu hutuambia kwamba watoto wao walikuwa wanapiga mateke mafuvu ya watu na kutoa nguo za wafu.

Lakini sasa wanatuambia kile walichokipata na hawagusi mwili ," alisema Mwanaakiolojia Janine Campos Fuentes.

Meya Gerardo Espindola Rojas anataka watu kunufaika na pesa zitokanazo na utalii wa miili ya wafu wa kale (mammies)

Chanzo cha picha, IVAN ASTUDILLO

Maelezo ya picha, Maria Nieto (kushoto) na Paola Pimentel wamefurahi uelewa watu kuhusu mammies umeongeka

Wanawake hawa wanaongoza ufufuaji katika maeneo, kwa ushirikiano wa karibu na Chuo kiku cha eneo hilo cha wanasayansi cha Tarapaka, wanasaidia wenyeji kuelewa umuhimu wa kitamaduni wa Chinchor na kuhifadhi maeneo ya thamani.

Kwa sasa, ni sehemu ndogo ya zaidi ya wafu (mammies) 300 wa jamii ya Chinchorro waliowekwa kwenye maonyesho. Wengi wao wako katika majumba ya makumbusho ya akiolojia ya San Miguel de Azapa.

Meya Gerardo Espindola Rojas ana matumaini kuwa kujumuishwa kwa miili ya wafu hao wa kale( mummies) katika orodha ya urithi wa utamaduni wa dunia kutayafanya makumbusho hayo kutembeelewa kwa urahisi na watalii na kupata pesa za ziada.

Meya Gerardo Espindola Rojas anataka watu kunufaika na pesa zitokanazo na utalii wa miili ya wafu wa kale (mammies)

Chanzo cha picha, FELIPE TOBAR ALDUANTE

Maelezo ya picha, Meya Gerardo Espindola Rojas anataka watu kunufaika na pesa zitokanazo na utalii wa miili ya wafu wa kale (mammies)

Lakini anasema ni muhimu kufikiria kwa umakini, sio kuzuru eneo, na kushirikiana na wenyeji.

"Tofauti na Roma, ambako watu huishi na minara, watu wa Arica huishi na masalia ya miili ya wafu, na tunapaswa kuwalinda wafu wafu wa kale(mammies)."

Sheria zimepitishwa, na Wanaakiolojia wanakuwepo popote panapofanyika shuguli za ujenzi ili miili hiyo ya thamani isidhurike.

Maria Nieto anasema umaarufu wa mummies unamnufaisha kila mmoja.

"Ni mji mdogo, lakini ni mji rafiki.

Tunataka wanasayansi na watalii kutoka kote duniani waje na kujifunza kuhusu utamaduni wa Chinchor. Tunaishi na utamaduni huu wa kuishi na wafu.