Je watoto wa binadamu wa kale wana utofauti gani na watoto wa sasa?

Reconstrucción del rostro de un neandertal

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika kipindi cha kawaida cha kiangazi, fukwe maarufu ya Castilla, yenye mchanga safi wa takribani kilomita 20 ukiwa umezungukwa na uoto wa asili karibu na eneo la mapumziko la Matalascañas lililopo Huelva, huko Andalusia, huenda kungekuwa na alama nyingi za miguu za watalii waliotembelea eneo hilo.

Lakini mwezi Juni 2020, wakati safari za ndege za kimataifa zilipositishwa kutokana na mlipuko wa covid-19, fukwe hiyo ikawa si kama ilivyozoeleka, ilibadilika na kuwa kimya.

Wanabaiolojia wawili, María Dolores Cobo na Ana Mateos, ambao walikuwa wanatembea pembezoni mwa maji, hata hivyo walibaini vielelezo vingi vya watu kupita eneo hilo.

Lakini ilikuwa vigumu sana kubaini ni wageni wa aina gani. Wakati wa dhoruba kali na mawimbi ya nguvu pembezoni mwa bahari kupiga Kusini-magharibi mwa Uhispania kutokea mwanzoni mwa mwaka 2020 , mawimbi makubwa yalisomba mchanga kutoka katika fukwe na kuacha wazi eneo kubwa la miamba, lililofunika kwa mita za mraba 6,000.

Wanasayansi walibaini nyayo zilizokuepo kwenye mwamba.

Lakini wakati wakati wanasayansi hawa walivyoangalia kwa karibu, alama hizo hazikuwa za wanyama tu, kilichoshangaza ni kuwa zilikuwa zinafanana na wanadamu.

Na vilevile alama hizo zilionekana kuachwa muda mrefu uliopita.

Katika utafiti wa awali unaonesha kuwa alama hizo ziliachwa muda mrefu uliopita wa kati ya miaka 80 au 120,000 iliyopita, na hivyo zilikuwa alama za watu wa kale.

Tunaweza kukisia tu ni jambo gani walikuwa wanalifanya na walikuwa wanaelekea wapi, lakini kati ya nyayo 87 zilizopatikana, zingine zilikuwa ndogo zaidi ya nyingine.

Na alama hizo ziliachwa na kundi la watu wakiwemo watoto.

Huellas de neandertales

Chanzo cha picha, Eduardo Mayoral et al/Scientific Reports

Maelezo ya picha, 70% ya nyayo hizo zilizopatikana kwenye fukwe zilikuwa za vijana na watoto.

Mpaka hivi karibuni , maisha ya watoto wa binadamu wa kale yalikuwa na usiri mkubwa.

Lakini katika mapinduzi ya kisayansi katika miongo mitatu iliyopita wameweza kuanza kupata taarifa za ndani juu ya watoto wa binadamu wa kale.

Kutafuta chakula

Huko Matalascañas, watafiti walikuwa wanatumia ndege zisizo na rubani na teknolojia ya picha ya hali ya juu katika kurekodi na kutengeneza katika mfumo wa kidigitali kuonesha nyayo za watu wa kale kabla ya kufunikwa na mchanga tena katika siku za kugundulika kwao.

Je walijifunza kuwinda wakiwa vijana wadogo?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Je walijifunza kuwinda wakiwa vijana wadogo?

Vipimo vya nyayo au alama za miguu zilibainika kuwa za watu wazima wa sasa, lakini takribani 71% zilikuwa za watu wazima na watoto waliopita miaka sita.

 Walikuwa wanafanya nini?

Kulikuwa na alama za wanyama pia, lakini zilikuwa zinaonekana katika maeneo ya majimaji, wakati alama za watu wa kale ziliweza kuonekana mbali ya ukingoni wa maji.

Watafiti walidhani kuwa labda walikuwa wanawafuatilia wanyama au samaki. Nyayo zilizokuwa katika maji madogo zikiwemo za watoto wadogo hivyo haiwezekani kuwa walikuwa wanasaidia kutafuta chakula, labda walikuwa wanajifunza na kucheza kama ilivyo kwa watoto wa siku hizi.

Reconstrucción del cuerpo de un neandertal

Chanzo cha picha, Getty Images

Maendeleo yanayofanana

Shukrani kwa mbinu kadhaa za wanasayansi kama hizo pamoja na suala la kuwa na bahati, wanaakiolojia wanaweza sasa kutengeneza picha ya kufikirika ya watu wa kale kutoka kichwani mpaka kwenye vidole.

Na badiliko moja kubwa ni kile kilichofahamika kuhusu ndugu zake wa karibu na pamoja na watoto wao.

Kupata taarifa zaidi , tuanzie mwanzo kwa kuangalia namna walivyokua?

Watafiti wengi walikuwa na idadi kubwa ya mabaki ya watoto wa kale ya kuyafanyia utafiti.

Kama ukiwapanga kwa kuangalia umri, kuanzia vijana mpaka watoto wanaosoma na hata watoto wachanga.

Wakati wa kuangalia mabaki yao, ukuaji wa watoto wachanga ulionekana unafanana na watoto wetu.

Ingawa kuna baadhi ya vitu wanatofautiana.

Utofauti wa meno

Cráneo de un joven neandertal

Chanzo cha picha, cc-by-sa-3.0 Guerin Nicolas

Kuanzia hatua za awali za ukuaji, katika siku chache, kulibainika kuwepo kwa mistari midogo ndani ya meno.

Kwa kutumia darubini au teknolojia nyingine zenye nguvu duniani , watafiti wameweza kuhesabu mistari hiyo na maeneo mengine ya fuvu la binadamu.

Hii inathibitisha kuwa meno ya watoto wa kale, yalikuwa yanakuwa kwa haraka zaidi ya binadamu wa sasa.

Reconstrucción del rostro de un neandertal

Chanzo cha picha, Getty Images

Baadhi ya watoto wa kale walikuwa wanapoteza meno ya utotoni wakiwa ndani ya mwaka.

Masalia mengi ya watoto wa kiume ambao waliishi kaskazini mwa Uhispania miaka ipatayo 50,000 iliyopita yanaonesha kuwa mtoto wa miaka tisa hivi wakati alipofariki lakini mistari ya meno yake ya nyuma na mifupa ya meno yake ya nyuma yalionekana kutokomaa.

Hata hivyo inawezekana ni kati ya wale watoto ambao meno yao yanachelewa kukua lakini inatukumbusha vyema , kama watoto wanavyofananishwa kwa yupi ana meno ambayo hayapo, pia binadamu wa kale nao wanatofautiana.

Ubongo unaofanana

Kama tutaweza kupata muda wa kufananisha jinsi watoto wachanga wa kale na wasasa walivyokuwa wanakuwa duniani kote, tungeweza kugundua kuwa muonekano wa miili yao ingekuwa tofauti zaidi kadri muda unavyoenda.

Ikiwa mtoto wa kale alikuwa amefunikwa ubongo wake kama watoto wetu, kichwa chake kingekuwa kikubwa kidogo.

Inavutia, jinsi fuvu la kale lilivyokuwa licha ya kuwa watu wa kale walikuwa wanakuwa kwa haraka na muonekano wao ulikuwa tofauti na wetu , ikimaanisha kuwa watoto wao walikuwa wanawahi kutabasamu, kutambaa na kutembea ukilinganisha na watoto wetu.

Je watoto wawili - wa binadamu wa kale na sasa -wangekutana, wangeweza kucheza na hata kufurahi pamoja?.

Jinsi ya kuwasiliana

Neno la kwanza kwa mtoto kutamka katika hatua za awali zinatajwa kuwa hatua muhimu sana katika hatua za mwanzoni za maisha, lakini je watu wa kale walikuwa wanaongea?

Ushahidi kadhaa umehitimisha kuwa walikuwa wana namna yao ya kuwasiliana katika maisha yao ya kila siku.

Ilibainika kuwa watu wa kale walikuwa wanaweza kutoa sauti inayofanana kabisa na watu wa sasa.

Lakini pia ukiachilia utofauti kidogo wa jinsi masikio yao yalivyo, lakini walikuwa wanasikia karibu sawa na sasa. Sauti zao zilivyosikika.

Huku neno la kwanza kusikika na kueleweka kilichomaanishwa kuwa rahisi kama ilivyo kwa watoto wa sasa.

Baadhi ya meno ya watoto wa kale yanaonesha kuwa walikuwa wananyonyeshwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya meno ya watoto wa kale yanaonesha kuwa walikuwa wananyonyeshwa

Sauti zilikuwa muhimu katika mazungumzo ya ana kwa ana na vilevile labda tungeweza kubaini lugha ambayo wanatumia.

Kunyonyesha

Miongoni mwa vitu ambavyo watoto wa kale walikuwa wameanza kuongelea ni suala la maziwa.

Mamalia wote wananyonyesha watoto wao wakizaliwa, na unaweza kuona ushahidi wa moja kwa moja katika meno yao.

Kwa mujibu wa takwimu , watoto wao walianza kula chakula kingine wakiwa na miezi minne na saba , muda ambao uko sawa na watoto wa sasa.

Taratibu nyingi bado zinaendelea mpaka sasa katika jamii isipokuwa wao walikuwa wananyonyesha mpaka mtoto anapofikia umri wa miaka minne.

Lakini mabaki yaliyopatikana Ubelgiji , yanaonesha mtoto anaacha kunyonya mara tu anapopita mwaka mmoja, hivyo inawezekana kulikuwa na utofauti kutokana na mama.

Hata kama watoto wengi wa kale walikuwa wanawaachisha kunyonyesha kutokana sababu za kiafya.

Mifano mingine ipo kwenye meno, inahusisha magonjwa , maambukizi na utapiamlo.

Ingawa si rahisi kugundua chanzo cha mtu wa kale, kujua alipata shida gani haswa wakati akiwa mtoto wa umri mitatu hadi mitano, labda wakati ameacha

kunyonya - maziwa huwa yanasaidia kutoa kinga kwa watoto na hata kuzuia watoto kupata magonjwa.

Hata hivyo , sampuli hizi za watoto wa kale zinaonesha kuwa watoto wa kale walikuwa hawapati ugumu kama zaidi ya wale wa awali zaidi.

Matatizo ya kiafya

Huesos neandertales

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya mifupa ya watu wa kale inaonesha jinsi walivyokuwa wameumia

Licha ya kwamba walikuwa na afya duni, watu wengi wa kale walithibitisha kuwa na magonjwa, maambukizi na mengine yalisababisha maumivu na changamoto katika maisha yao.

Baadhi ya mifupa ya watu wa kale inaonesha jinsi walivyokuwa wameumia.

Wenye nguvu na wanariadha

Waliokuwa na afya nzuri walikuwa na nguvu, na waliweza kukimbia sana na hawakuwa wanafanana na sokwe.

Walikuwa sawa kabisa licha ya kuwa na utofauti kidogo wa muonekano na binadamu wa sasa, lakini utafiti umeonesha walikuwa wanatembea sawa kabisa na watu wa sasa.

Watoto wa kale walikuwa wana jukumu gani katika makundi

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wa kale walionekana wakitoka sehemu moja kwenda nyingine sana , na walionekana kuwa na misuli mikubwa kidogo kwenye miguu yao.

Kwa watoto, kile ambacho tungefananisha na nyumbani labda makazi yao yalikuwa si mapango au kwenye mawe tu bali hata kwenye mandhari ya kawaida.

Alama zaidi za miguu

Grupo de neandertales en una cueva

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watoto wa kale walikuwa wana jukumu gani katika makundi

Katika pango la Theopetra, karibu na Thessaly katikati ya Ugiriki, alama kadhaa za miguu zilibainika .

Inawezekana ilikuwa takribani miaka ya 128,000 iliyopita, na ilionekana kwa watu tofauti tofauti.

Mlipuko wa Volkano

Watu wengine wa kale walibainika kuwa katika eneo la wazi , wengi wakiwa vijana.

Mkubwa alikuwa ametoka katika majivu ya volkano yaliyotokea Italia.

Baada ya mlipuko mkubwa wa volkano katika miaka ya 350,000 watu walipata namna ya kusaidiana kwa kushikana mikono.

Maeneo ambayo hayakuachwa nyayo

Reconstrucción del cuerpo de un neandertal

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata hivyo nyayo zilizooonekana hivi karibuni huko Matalascañas nchini Uhispania, ni za kipekee, na zinaweza kutoa ushahidi mdogo hata kwa watoto wadogo kuwa miongoni mwa waliokuwa wanatafuta chakula.

Hata hivyo walikuwa wanapaswa kujifunza kwa namna Fulani.

Hata katika maeneo ambayo hakukuwa na alama za miguu, walilazimika kuhisi ni nani walikuwa hapo.

Ukichukua mfano wa mwaka 330,000-wa eneo la kuwindia Ujerumani, katika pembezoni mwa ziwa kulikuwa na magari ya farasi kati ya 20 na 50 , yaliotoa ushahidi kuwa walikuwa wanayatumia kuwinda mara nyingi.

Licha ya kuwa haiwezekani kuwa na uhakika , bali ni kuhisi tu kulingana na ushahidi uliopatikana.