Ndege ya kivita ya India kwa jina 'Mirage' inafanya nini Israel?

Chanzo cha picha, @DRSJAISHANKAR
Israeli kwa sasa inaendesha mazoezi ya vikosi vya kimataifa vya anga yanayoitwa 'Blue Flag 2021', ambayo yamekuwa yakielezewa na Israeli kama mazoezi makubwa zaidi ya kikosi cha anga kuwahi kufanyika.
Kikosi cha anga cha Israeli -Air Force kimesema kuwa mazoezi, ambayo yanafanyika kila baada ya miaka miwili, yanalega kuimarisha uhusiano baina ya mataifa tofauti, na mwaka huu ni mazoezi makubwa na ya mbinu za kisasa zaidi za anga kuwahi kuendeshwa nchini Israeli.
Vikosi vya anga vya nchi saba vinashiriki katika mazoezi hayo ambayo yataendelea hadi tarehe 28 Oktoba.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Vikosi vya anga kutoka mataifa ya Ujerumani, Italia, Uingereza, India, Ugiriki, na Marekani vinashiriki mazoezi hayo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Ni kwanini mazoezi haya ni ya kipekee?
Israeli inasema kwamba ni mazoezi makubwa zaidi ya vikosi vya anga kuwahi kufanyika hadi sasa, ambapo zaidi ya vikosi vya nchi saba vinashiriki.
Kulingana na gazeti la Israeli Haaretz , katika mwaka 2017, afisa wa kikosi cha Israeli cha anga - Israeli Air Force alisema mazoezi ya miaka miwili ni "diplomasia ya anga" inayoonyesha wazi kwamba nchi nyingi zinahofu juu ya mataifa ya kiarabu na masuala ya kisiasa kama vile suala la Palestina. Ukiachana na kwamba, wanahitaji ushirikiano wa kimkakati na Israeli.
Unaweza pia kusoma:
Kikosi cha anga cha Israeli kinasema kuwa mazoezi hayo yanapanua uwezo wake pamoja na vikosi vinavyoshiriki, kuangazia zaidi mashambulio ya anga kwa anga na ya anga kwa ardhi.

Chanzo cha picha, TOMER AIZIK/IAF
Kando na hili, mazoezi haya pia yanajumuisha ukwepaji wa mifumo ya mashambulio yake ya ardhini katika eneo la adui.
Kikosi cha Israeli cha anga kimesema katika taarifa yake kwamba 'hii ni mara ya kwanza kwamba meli za kijeshi za Uingereza zimeshiriki mazoezi yaliyoandaliwa na Israeli.

Chanzo cha picha, TOMER AIZIK/IAF
"Kuendeshwaakwa mazoezi ya kimataifa katika hali hii halisi na muendelezo wa shughuli zetu katika maeneo yote ya vita ni mambo ya mkakati muhimu na mkubwa. Wakati huo huo itakuwa na athari kubwa kwa kikosi cha anga cha Israeli, Kikosi cha ulinzi cha Israeli na kikosi cha taifa cha Israeli ." alisema Meja Jenerali wa Israeli Major General Norkin.
Major General Norkin aliongeza kuwa mazoezi yanayoendelea ni hatua kubwa katika kanda hiyo na ushirikiano wa kimataifa.

Chanzo cha picha, TOMER AIZIK/IA
Jumanne, mkuu wa vikosi vya ulinzi vya , Aviv Kochawi, alimtunuku mkuu wa kikosi cha Ujerumani katika mazoezi hayo Gerhartz Medali ya shukran.
Heshima hii ameipata kutokana na juhudi zake za kuanzisha ushirikiano wa karibu baina ya vikosi vya Israeli na vya Ujerumani.
Norkin alitunukiwa Tuzo la kazi bora la Shirikisho la Ujerumani, likiwa ni tuzo la juu zaidi la kitaifa lililotolewa na balozi wa Ujerumani nchini Israeli , Susan Wasum-Geiner.
Katika sherehe hizo, Wasum-Gyner alisema kuwa ''ndege za Israeli na pia zinajiandaa kwa pamoja kwa kazi ya changaoto kubwa zaidi katika kipindi hiki''
"Ushiriki wa ndege ya Israeli wa mwaka katika mazoezi ya kikosi cha anga cha Ujerumani ilikuwa ni hatua nyingine ya maana ambayo ilionyesha kukua kwa ushirikiano wa kitaaluma na urafiki miongoni mwa wanajeshi wetu.", alisema Wasum-Gyner.












