Black Hawk Down: Vita vikali vya Somali vilivyobadili sera ya Marekani kuhusu Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani imetangaza kuwapeleka wanajeshi wake nchini Somalia ili kupambana na kundi la Al shabaab .Lakini sio mara ya kwanza kwa jeshi la Marekani kutumwa nchini humo na mara ya mwisho liliondoka katika hali ambayo hadi leo huzua hofu katika nyoyo za walioshuhudia matukio ya siku za mwisho za kuondoka kwao.Hii hapa simulizi mwanajeshi mmoja aliyekuwa katika kikosi cha Marekani kilichokuwa Somalia.

Picha za miili ya wanajeshi wa Marekani wakiburuzwa katika mitaa ya Mogadishu ilikuwa hatua ya kugeuza moja wapo ya hatua za hali ya juu zaidi nchini Marekani barani Afrika.
Picha hizo, zilizopeperushwa ulimwenguni kote, ziliwakasirisha wengi.
Mnamo Oktoba 1993, wanajeshi wa vikosi maalum vya marekani walianzisha uvamizi katika mji mkuu wa Somalia ,Mogadishu.
Lengo lao lilikuwa kukamata washirika muhimu wa mbabe wa kivita wa Somalia, Jenerali Mohamed Farah Aideed. Lakini majeshi ya Marekani yalipata upinzani mkali kutoka kwa wanamgambo wa Aideed.

Chanzo cha picha, US aRMY
Helikopta mbili za Black Hawk za Marekani ziliangushwa .
Katika vita vilivyofuata, mamia ya Wasomali walikadiriwa kufa. Wamarekani 18 na wanajeshi wawili wa UN waliuawa.
Wakati huo, Marekani ilikuwa ikiongoza ujumbe wa UN kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na njaa nchini Somalia.
Ndani ya miezi sita, Marekani ilikuwa imeondoa vikosi vyake kutoka Somalia. Kushindwa kwa misheni yake nchini Somalia kulifanya Marekani iogope kuingilia kati mizozo ya barani Afrika.
Kutuzwa kwa baadhi ya wanajeshia walioshiriki vita hivyo
Wanajeshi 18 wa Marekani waliopigana huko Somalia wamepewa tuzo za heshima.
Nishani ya silver star ilipewa wanajeshi hawa, ambao miaka 28 iliyopita walitumikia katika Kikosi cha 3 cha Jeshi la Marekani cha brigedi ya 75, na hapo awali walikuwa na medali za nyota za shaba.
Wanaume hao waliostaafu waliopata medali hizo walikuwa: Alan Barton, John C. Belman, Kenneth P. Boorn, James M. Cavarco, John M. Collett, Michael Collins, James C. Joyce, Brad M. Paulsen, Larry D. Perino, Robert R. Phipps II, Dominick M. Pilla, Randall J. Ramaglia Jr., John D. Stanfield, Michael Steele, Richard Storus, Jeffrey D. Struecker, Joseph F. Thomas na Sean T. Watson.

Chanzo cha picha, JEFF STRUECKER
Wote waliopokea tuzo hiyo walikuwa wanajeshi walioondoka Somalia baada ya vita ambapo wanajeshi 18 waliuawa mnamo 1993, vilivyopewa jina la Black Hawk Down (moja ya majina ya ndege zilizodunguliwa wakati huo).
Uongozi wa jeshi ulisema katika sherehe ya tuzo kwamba maveterani hao waliheshimiwa kwa kazi yao mnamo Oktoba 3 na siku iliyofuata, Oktoba 4, 1993.
Imekuwa miaka 28 tangu wanajeshi wa Marekani nchini Somalia wauawe katika operesheni hiyo, ambayo pia ilisababisha vifo na majeruhi kwa wanajeshi wa UN waliopelekwa Somalia.
Hali ya kibinadamu kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe kufuatia kuanguka kwa serikali kuu ilisababisha nchi nyingi ulimwenguni kutangaza kile kinachoitwa operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa iliyopelekea kuletwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia.
Jeff Struecker, mwanajeshi wa Kikosi cha 75 kilichotumwa Somalia na wahudumu wa afya - sasa kwenye orodha ya tuzo - alisema hangeweza kulinganisha chochote na tukio la Somalia wakati wa kazi yake kama mwanajeshi .
'Sijawahi kushuhudia kitu kama hiki'
Katika miaka 23 kama mwanajeshi wa Marekani, Jeff Struecker amesafiri kwenda Panama, Afghanistan na Iraq, lakini anasema hajawahi kuona hali mbaya zaidi katika mitaa ya Mogadishu kama alivyshuhudia mnamo Oktoba 1993.
"Nimepigana huko Somalia mara kadhaa kabla na mara nyingi baadaye, lakini sijawahi kuona ujasiri huo na mapigano kama tulivyoona katika barabara za Mogadishu, Somalia. Hata sijakaribia," alisema Struecker.
Mapema siku hiyo, Jeff Struecker alisema yeye na wenzake walikuwa wametumwa Somalia kumkamata Jenerali Mohamed Farah Aideed na kuelezea kile kilichotokea mapema Oktoba 1993.

"Mimi na kikosi changu tulitumwa kwenye operesheni yetu ya saba na ya mwisho, kwa lengo la kumkamata Aideed, wakati wa misheni hiyo ya Black Hawk Down," alisema Jeff Struecker.
Jeff alisema hofu aliyopata wakati wa operesheni ya kumkamata Aideed ilikuwa kubwa na hataisahau kamwe.
Bwana Struecker, ambaye alioa miaka michache iliyopita, alisema aliamini kwamba hangemwona tena mkewe na mtoto wake kwani ndiye alikuwa akisimamia operesheni hiyo.
Filamu maarufu iliyotengenezwa Hollywood baadaye iliyoitwa "Black Hawk Down", inasimulia hadithi ya matukio yaliyohusisha wanamgambo wa Kisomali na jeshi la Marekani nchini Somali














