Uchumi wa Ethiopia waathiriwa na mzozo wa Tigray

Chanzo cha picha, AFP
Vita vya Ethiopi vya miezi 10 vimeathiri vibaya nchi hiyo huku maelfu ya watu wakiuawa na mamilioni ya wengine walioachwa bila wakihitaji msaada.
Lakini hiyo sio athari pekee inayoshuhudiwa katika nchi hiyo iliyo na watu wengi -vita hivyo vimesababisha athari za kiuchumi ambazo itachukua miaka kadhaakurekebisha.
Katika mji mkuu wal Addis Ababa, Tigist mwenye umri wa miaka 26, ambaye hakutaka jina lake kamili kutajwa , anasema gharama ya matumizi yake ya mwezi imepanda mara mbili kutokana na sababu mbili: vita vilivyozuka katika eneo la Tigray mwezi Novemba na janga la corona.
"Kabla ya Covid na mzozo, Nilingelitumia birr 1,000 [karibu dola 22] kila mwezi kununua mboga. Sasa natumia birr 2,000," anasema. "Vitu ni bei ghali sana - simu, chakula na nguo."
Takwimu rasmi zinaonesha bei ya bidhaa za matumizi imepanda sana nchini Ethiopia - mwezi Julai ukilinganisha na mwaka jana
Tigist anafanya kazi ya uuzaji katika duka la jumla kukimu familia yake. Jukumu lake ni kununua chakula huku ndugu yake akilipa kodi ya nyumba.
"Kiwango cha ubadilishanaji fedha za kigeni pia haijakuwa nzuri,"anaongeza. "Mwaka jana Dola moja ya Marekani ilikuwa birr 35 sasa imefikia 45."
Faisal Roble,mchambuzi mwenye makao yakeMarekani aliyejikita katika masuala ya Upembe wa Afrika, anasema anasema kuwa matumizi ya vita "yameathiri vibaya uwezo wa Ethiopia kupata dola", na imesababisha kiwango cha ubadilishaji kuzorota.
Haijabaini vita hivyo vimegharimu fedha ngapi lakini lakini Uchumi wa Biashara unatabiri matumizi ya kijeshi yatafikia Dola milioni 502 (£ 365m) ifikapo mwisho wa mwaka, kutoka Dola milioni 460 mwaka jana.
Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema mzozo huo "umetumia mabilioni ya dola kutola hazina kuu ya nchi".
Kabla ya janga la kimataifa na vita, uchumi wa Ethiopia ulikuwa moja ya chumi zinazokuwa kwa kasi katika eneo hili, ukipanuka kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka katika mwongo wa kuelekea mwaka 2019, kulingana na Benki ya Dunia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ijapokuwa Tigist anaangazia viwango rasmi vya ubadilishanaji katika benki, thamani ya birr imeshuka zaidi katika soko isiyokuwa rasmi, Bwana Roble anasema akiongeza kuwa birr imefikia 67 dhidi ya dola.
Nanasema wenye biashara nchini wanahofia hali ya usalama baada ya vita kuenea hadi maeneo jirani ya Afar na Amhara nje ya Jimbo la Tigray.
Wengi wanaondoa fedha zao katika benki na kuwapelekea wafanyabiashara wa fedha katika jimbo la Somaliland lilnalotaka kujitenga Somalia, na hatua hiyo imefanya thamani ya birr kushuka chini zaidi, Bwana Roble anasema.
Benki zafungwa Tigray
Mzozo ulianza baada ya chama tawala katika jimbo la Tigray- Tigray People's Liberation Front (TPLF) kushambulia kambi ya majeshi a ya muungano mwezi Novemba, huku kukiwa na ugomvi unaozidi kuongezeka na Waziri Mkuu Abiy Ahmed juu ya kuvunjwa kwa muungano unaotawala na kuahirishwa kwa uchaguzi.
Tangu wakati huo, Jeshi la Ethiopia - pamoja na washirika wao wa Eritrea, vikosi vya polisi vya kitaifa na wanamgambo wa eneo hilo - wamepigana vita vikali dhdi ya wapiganaji wa Tigray.
Pande zote mbili zimelaumiwa kwa kutekeleza ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na mauaji makubwa ya raia.
Tigray imekuwa bila huduma muhimu, kama vile mawasiliano na benki, tangu serikali kuu ilipozingira eneo hilo mwezi Juni,baada ya waasi kuteka tena mji wa Mekelle.

Chanzo cha picha, AFP
Zaidi ya watu 400,000 katika eneo la Tigray tayari wanaishi katika hali ya njaa wakati usambazaji wa misaada umelemazwa- nao umeme na usambazaji wa mafuta unapungua, na kushinikiza bei kupanda
Mkazi wa Mekelle Filmon Berhane ameiambia BBC Tigrinya kwamba chakula na kodi ya nyumba imepanda maradufu hivi karibuni.
"Hakuna pesa na benki zote zimefungwa na ofisi za serikali hazilipi mishahara,"anasema.
Mnada wa simu ya rununu uligonga
Kimataifa, vita hivi vimeathiri sifa ya Ethiopia katika masuala ya uwekezaji, nasema mchumi Irmgard Erasmus kutoka shirika la NKC African Economics consultancy.
"Ikiwa watumiaji wanakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na mfumuko mkubwa wa bei, huwezi kupata ukuaji unaotokana na watumiaji kama inavyofanyika Marekani au Ukanda wa Euro, "anasema.
Bi Erasmus anaashiria ubinafsishwaji wa hivi karibuni wa sekta ya mawasiliano ya Ethiopia, ambayo hapo awali ilivutia maslahi kutoka kwa watoa huduma kadhaa, pamoja na kampuni kubwa ya mawasiliano ya Afrika Kusini MTN.
Mwishowe, ni kampuni moja tu iliyofanikiwa kushida mnada wa moja ya leseni mbili za simu zinazopeanwa, kupitia muungano unaongozwa na Safaricom ya Kenya ambayo iliahidi dola milioni 850.
Sheria za awali ziliwazuia wamiliki wa leseni mpya kuendesha mfumo wa kutuma na kupokea pesa kupitia simu. Hali iliyopunguza walipunguza maslahi ya mwekezaji, vyanzo vya makapuni vinasema mzozo wa Tigray pia ulikuwa na uzito mkubwa fikra za wawekezaji.

Chanzo cha picha, AFP
Shinikizo la kukomesha vita
Ukuaji wa uchumi wa Ethiopia mwaka huu unatarajiwa kushuka kutoka 6% mwaka 2020 hadi 2% mwaka 2021 - kiwango ambacho ni cha chini zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa karibu miongo miwili, kulingana na Shirikal la Fedha duniani IMF.
Nchi hiyo inaagiza bidha za karibu dola bilioni14 kutoka nje kwa mwaka, huku ikiuza nje ya nchi bidhaz za thamani ya dola bilioni 3. tu.
Kingine kinachozua hofu ni deni la kitaifa la Ethiopia, ambalo baadhi ya waangalizi wanatarajia likafikia dola bilioni 60 mwaka huu, au karibu asilimia 70 ya pato jumla la Taifa (GDP)
"Haya ni makadirio ya kihafidhina," anasema Bi Erasmus, akiongeza kuwa matumizi ya jeshi la Ethiopia huenda ikawa juu zaidi ya ilivyokadiriwa,na imechukua deni ambalo halijaripotiwa siku zilizopita.

Maelezo zaidi kuhusu mzozo wa Tigray:

Wakati Marekani imewawekea vikwazo vya usafiri Waethiopia wanaohusika kwenye vita, na kuzuia matumizi, hadi sasa, jamii ya kimataifa imekuwa ikisita kutoa shinikizo kubwa la kiuchumi kwa serikali, au kupunguza mipango ya misaada ya ukarimu.
Karibu robo ya watu wanaishi katika mazingira ya umasikini, na wastani wa mapato ya kila mwaka ni dola 850 tu kwa kila mtu.
"Bila shaka kuna haja ya kuimarisha vikwazo ikiwa Waziri Mkuu Abiy, ambaye alishinda tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 2019, hatazuia mzozo huo," anasema Witney Schneidman mtafiti wa kituo Brookings huko Washington.
Utawala wa Biden umejipata katika njia panda, anasema Bwana Schneidman, haitoshi kumshinikiza Bw. Abiy kumaliza vita bila kuitenga Ethiopia kabisa.
"Zana zote ziko mezani, lakini una watu milioni 110, huwezi kutenga nchi, ni muhimu sana kimkakati," anasema.













