Mzozo wa Tigray: Jukumu la Eritrea katika mzozo wa Ethiopia

Eritrea's leader, Isaias Afwerki, and Ethiopian Prime Minister Abiy Ahmed

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika ishara ya kuonesha mabadiliko ya kisiasa ya mtu ambaye wakati mmoja alikuwa ametengwa, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amemesimama na mshirika wake mkuu, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, kwa kuwapatia wanajeshi wake msaada waliohitaji kupigana na vikosi vya Tigray People's Liberation Front (TPLF) katika jimbo la Tigray.

Katika hotuba ya hivi karibuni katika bunge la Ethiopia, mshindi huyo wa Tuzo ya Amani Nobel alifichua kwamba Eritrea, iliwapa chakula, mavazi na silaha wanajeshi wa Ethiopia ambao walikuwa wamerudi nyuma wakati TPLF walipowashambulia mara ya kwanza na kuteka kambi zao mjini Tigray, eneo la Ethiopia ambalo linapakana na Eritrea.

Bw. Abiy alisema hatua hiyo iliwawezesha kurudi na kupigana na TPLF, vugu vugu la zamani la wapiganaji karibu 250,000, hadi lilipoondolewa katika utawala wa eneo hilo Novemba 28.

"Watu wa Eritrea wametuonesha... kuwa ni jamaa zetu kwa kusimama nasi wakati mgumu," aliongeza kusema.

Addis Sissay, 49, walks in front of his destroyed house in the village of Bisober, in Ethiopia's Tigray region on December 9, 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mzozo katika jimbo la Tigray umeathiri maisha ya watu wengi

Tamko hilo la Bw Abiy lilikuwa muhimu, japo hakuthibitisha madai kwamba Bw. Isaias, pia alituma wanajeshi wake kusaidia kuwashinda TPLF, adui wa muda mrefu wa kiongozi huyo wa Eritrea ambaye amkuwa madarakani tangu mwaka 1993.

Hospitali zadaiwa kushambuliwa

Madai ya kwamba wanajeshi wa Eritrea wameingia Tigray yalitolewa na TPLF, raia waliokuwa wakitoroka mapigano na Waeritrea wanaoishi ndani na nje ya nchi.

"Isaias anatuma Waeritrea wadogo kwenda kufariki Tigray. Vita hivyo pia vitadhoofisha uchumi wetu zaidi. Lakini Isaias atakuwa madarakani kwa muda mrefu. Anawaacha watu katika hali ngumu ili wasipiganie uhuru wao," alisema Paulos Tesfagiorgis, mwanaharakati wa Eritrea wa kutetea haki ambaye alilazimishwa kukimbilia mafichoni nautawala wa Asmara.

Msemaji wa kitengo cha mambo ya nje ya Marekani pia alisema kulikuwa na "ripoti za kuaminika" za uwepo wa wanajeshi wa Eritrea huko Tigray, na akutaja "madai hayo kuwa makubwa".

Serikali zote mbili zimekanusha ripoti hizo, huku waziri wa mambo ya nje wa Eritrea Osman Saleh Mohammed, akiyataja madai hayo kuwa ''propaganda''

Map
2px presentational grey line

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Gueterres, alisema Bw. Abiy amemhakikishia hakuna wanajeshi wa Eritrea waliongia Tigray, isipokuwa kataika maeneo ambayo Ethiopia likubali kupeana kufuatia mkataba wa kihistoria wa amani uliyofikiwa kati ya nchi hizo mbili mwaka 2018.

Mkataba huo ulimaliza mzozo wa mpakani wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili tangu mwaka 1998-2000, ambao ulisababisha vifo vya watu 100,000.

Kufikiwa kwa mkataba huo kulimfanya Bw. Abiy kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel, ingawa eneo hilo lilikuwa halijahamishiwa Eritrea wakati mzozo wa Tigray ulikuwa umeanza mapema Novemba.

Serikali ya Bw. Abiy imedhibiti kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutoa misaada na ya kutetea haki za binadamu kufika Jimbo la Tigray kuchunguza madai ya ukatili uliyofanywa na pande zote katika mzozo huo - ikiwa ni pamoja na hospitali kushambuliwa kutoka ndani ya eneo la Eritrea.

Eritrea haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo, yaliyoangaziwa katika taarifa iliyotolewa na mkuu wa UN wa kutetea haki za binadamu. Bw. Abiy amekana akisema wanajeshi wake hawakuua hata raia mmoja katika jimbo la Tigray.

"Vita hivi vimepiganwa gizani. Hakuna mtu anayejua kiwango cha mzozo huo na athari zake," alisema mchambuzi wa masuala ya Upembe wa Afrika Rashid Abdi mwenye makazi yake Kenya.

Vikosi vya Eritrea vyashutumiwa kwa wizi

Mchambuzi wa mwenye makao yake Marekani Alex de Waal amesema kuwa amefahamishwa na vyanzo vya UN kwamba mzozo huo umesababisha watu "kuhamishwa kwa kiwango kikubwa" katika eneo hilo, linalokaliwa na watu karibu 5,000 masikini zaidi nchini Ethiopia.

"Ikiwa madai hayo ni ya kweli, kutakuwa na njaa mkubwa Tigray," Bw de Waal alisema.

Aliongeza kuwa amepokea taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Tigray, zinazoashiria kuwavikosi vya Eritrea vilihusika na wizi.

"Tunasikia kwamba waliiba hata milango [na] vifaa vya bafuni, "alisema.

2px presentational grey line

Maelezo zaidi:

2px presentational grey line

Waeritrea wengine walisema wanajeshi hao wakishirikianana wa jamaa zao walikuwa wakikabiliana na vikosi vya TPLF kutoka maeneo kadhaa na baadahi yapo walikuwa wamevalia mavazi ya Wethiopia.

Eritrea inasisitiza kuwa hakuna wanajeshi wake ndani Tigray, waziri wake wa mambo ya nje akinukuliwa kusema: "Hatujahusika na hilo."

Lakini mwanadiplomasia wa zamani wa Eritrea aliye mafichoni Abdella Adem amesema anawajuwa wanajeshi waliojeruhiwa, huku vyanzo vya habari katika hospitali ya umma katika mji wa Senefa kusini mwa Eritrea vikifahamisha BBC kwamba wanajeshi wa Eritrea na Ethiopia wametibiwa hapo.

'Isaias nataka kuvunjwa kwa TPLF'

Vyanzo vingine vya habari nchini Eritrea vilisema wanajeshi wa Ethiopia wameonekana wakijikusanya tena katika eneo la kati mwa mji wa Hagaz, na kuwapeleka wenzao waliyojeruhiwa katika hospitali ya kijeshi ya Gilas.

Msomi wa Eritrea anayeishi Uingereza Gaim Kibreab amesema anaamini kwamba Bw. Isaias alipeleka wanajeshi wake Tigray kwa lengo "kuvunja" TPLF, ambayo aliongeza, imekuwa lengo kuu la kiongozi huyo wa Eritrea tangu wakati wa vita vy ampakani vya kati ya mwaka 1998-2000.

TPLF wakati huo ilikuwa madarakani nchini Ethiopia na katika jimbo la Tigray.

Military tank graveyard, Central region, Asmara, Eritrea on August 22, 2019 in Asmara, Eritrea.

Chanzo cha picha, Art in All of Us/Getty Images

Maelezo ya picha, Sehemu ya kuhifadhi magari ya kijeshi ilijengwa nchini Eritrea kufuatia vita vya uhuru vya 1961-1991

"Katika vita vya 1998-2000, TPLF ilimdhalilisha rais [Bw Isaias] kwa kuchukua kijiji kidogo cha Badme. Hata baada ya mahakama ya kimataifa kuamua kwamba kijiji hicho kilikuwa cha Eritrea, TPLF ilikataa kujiondoa katika eneo inalokaliwa kwa miaka 18.

"Rais amekuwa akingojea wakati huu kulipiza kisasi lakini lakini TPLF ilipuuza ujanja na uvumilivu wake na sasa bila shaka wanajutia uamuzi huo ," Bwana Gaim aliongeza.

Kutoka kwa amani na kurejea kwa mzozo

Wafuasi wa Bw Isaias wanasisitiza wanajeshi wa Eritrea hawakuvuka mpaka na juingia Tigray, bali waliendeleza juhudi za kuchukua eneo lao ambalo lilitekwa mjini Badme, na maeneo yaliyo karibu.

Akitoa maoni tofauti, Bw. Paulos alisema: "Badme imerejea mikononi mwa Eritrea, lakini hakuna tangazo rasmi lililotolewa kuhusiana na hilo kwasababu sio lengo kuu la Isaias. Bado anaendeleza ajenda ya kuvunja TPLF.

"Abiy alianza kama mleta amani na mageuzi, lakini ameingia katika mtego wa kulipiza kisasi dhidi ya TPLF, jambo ambalo Isaias alitaka lifanyike."

Women waving and smiling

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wananchi wakisherehekea mpaka wa Ethiopia-Eritrea ulipofunguliwa mwaka 2018

Bw. Abiy anasema alitaka kusuluhisha kwa amani tofauti kati yake na TPLF, lakini alilazimika kuchukua hatua dhidi yao baada ya kambi za keshi la kitaifa kutekwa katika shambulio la usiku wa Novemba 3, na kusema ilikuwa jaribio la kupindua serikali.

Japo Bw. Isaias alimsaidia wakati wa oparesheni ya kijeshi dhidi ya TPLF, vyombo vya habari vya Eritrea viliwaweka gizani wananchi kwa kutoangazia mzozo huo, hata baada ya wapiganaji wa TPLF kurusha kombora ambalo lilianguka viungani mwa mji mkuu wa Asmara mapema mwezi Novemba, na kusababisha mlipuko mkubwa ulioshuhudiwa na wakaazi.

Bw. Abiy anasema alitaka kusuluhisha kwa amani tofauti kati yake na TPLF, lakini alilazimika kuchukua hatua dhidi yao baada ya kambi za keshi la kitaifa kutekwa katika shambulio la usiku wa Novemba 3, na kusema ilikuwa jaribio la kupindua serikali.

Japo Bw. Isaias alimsaidia wakati wa oparesheni ya kijeshi dhidi ya TPLF, vyombo vya habari vya Eritrea viliwaweka gizani wananchi kwa kutoangazia mzozo huo, hata baada ya wapiganaji wa TPLF kurusha kombora ambalo lilianguka viungani mwa mji mkuu wa Asmara mapema mwezi Novemba, na kusababisha mlipuko mkubwa ulioshuhudiwa na wakaazi.

"Televisheni ya Eritrea inazungumza juu ya mabomu huko Syria lakini wakati makombora yalipotua Asmara, haikusema lolote," alibainisha afisa wa zamani wa serikali ya Eritrea Dawit Fisehaye alisema.

'Wakimbizi watekwa'

Huduma za intaneti zimedhibitiwa Eritrea na nchi hiyo haina uhuru wa vyombo vya habari wala vyama vya upinzani - Hatma ya wanasiasa 11 na waandishi 17 waliozuiliwa karibu miaka 20 iliyopita haijulikani.

Mafunzo ya kijeshi ni lazima huku nafasi za ajira zikiwa ni haba, hali iliyowafanya watu wengi - hususan vijana kutoraka nje ya nchi. Karibu 100,000 wamekuwa wakiishi katika kambi ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi katika jimbo laTigray.