Mzozo wa Tigray: Jinsi daktari wa Ethiopia alivyotoroka mashambulio ya wanamgambo

Madaktari wa Ethiopia wakifanya kazi katika kambi ya wakimbizi wa Tigray nchini Sudan

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Madaktari wa Ethiopia wakifanya kazi katika kambi ya wakimbizi wa Tigray nchini Sudan

Daktari mmoja wa Ethiopia amesimulia BBC wagonjwa walivyosafirishwa kwa lori na tinga na jinsi yeye mwenyewe alivyojificha msituni baada ya ghasia kuzuka katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia mwezi uliyopita.

Dkt Tewedros Tefera alitoroka mji wa kilimo wa Humera na baadae kuelekea mji wa karibu wa Adebay, akiambia BBC jinsi ilivyokuwa hatari kubaki katika miji hiyo.

Mwezi Novemba tarehe 4, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliamuru oparesheni ya kijeshi ya ardhini na angani dhidi ya chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) kinachoongoza jimbo la Tigray, baada ya vikosi vyake kushambulia kambi za wanajeshi wa muungano.

A donkey and residents on a street in Humera, Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Humera ni eneo linalosifika kwa kilimo ambalo linapakana na Eritrea

Bwana Abiy alisema majeshi ya Ethiopia hayakuua hata raia mmoja iliposhambulia mji wa mkuu wa Mekelle, na kuchukua udhibiti Novemba 28.

Serikali ya Eritrea pia imekana kuhusika na mzozo huo ili kusaidia kushindwa kwa TPLF, licha ya TPLF kurusha makombora katika himaya yake.

Imekuwa vigumu kupata taarifa za uhakika kuhusu mzozo huo kwasababu huduma za mawasiliano zimekatizwa katika eneo hilo.

Mji wa Humera - ambao unakaliwa na watu karibu 30,000 - ulikuwa moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya na mzozo huo, baada ya mapigano kuanza huko Novemba 8.

Onyo: Baadhi ya maelezo huenda yakawaathiri baadhi ya wasomaji.

Short presentational grey line

Ushahidi wa Dkt Tewedros:

Kulikuwa na mashambulio makali ambayo yalilenga kila sehemu ya mji wa Humera - sokoni, karibu na misikiti na makanisa na hata maeneo yaliyokaribiana na hospitali.

Kuna siku nakumbuka tulipokea karibu miili ya waty 10 waliouawa na karibu raia 75 waliojeruhiwa. Mashambulio hayo yaliendelea kwa muda mrefu saa za mchana.

Mji huo ulishambuliwa kutoka upande wa mashariki ambako vikosi vya ulinzi wa kitaifa wa Ethiopia vilikuwa, na upande wa kaskazini unaopakana Eritrea. Mpaka wa Humera kuingia Eritrea ni karibu miita 200 kwa hivyo bila shaka mashambulio hayo yalikuwa yanatoka upande wa Eritrea pia.

A member of the Amhara Special Forces in Humera watches on at the border crossing with Eritrea - 22 November 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Humera katika mpaka wa Ethiopia na Eritrea ambako walioshuhudia wanasema mashambulio yalifanyika kutoka upande huo

Siku ya pili mashambulio yalianza mapema asubuhi lakini yalipumgua mwendo wa saa tano. Tulipokea miili nane na watu wengine kadhaa waliojeruhiwa. Baadae tukaamua kuwa sehemu hiyo haikuwa salama kwa wagonjwana sisi wenyewe.

Tukaamua kuondoka. Tuliwachukua wagonjwa wetu waliyojeruhiwa na kuwaweka ndani ya lori na kuwasafirisha hadi Adebay, karibu kilomita 30 kutoka mji wa Humera. Huko kulikuwa kumetulia hakukua na mashambulio ya makombora lakini mapigano yalikuwa yakiendelea.

Tuliendelea kuwatibu wagonjwa katika kliniki ya Adebay. Raia zaidi walikuwa wanakuja kutoka Humera.

Siku ya kwanza, siku ya kwanza tuliwatibu majeraha yaliyotokana na mashambulio ya makombora, lakini baada ya vikosi vya serikali kuwasili Humera, walianza kuja wakiwa na majeraha ya kupigwa kwa fimbo na vifaa butu - kubwa kuliko zile zinasababishwa na kuchomwa kisu.

A mother looking after her daughter who was wounded in shelling on Humera, Ethiopia - 22 November 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwanamke mjini Humera akiwa na binti yake aliyejeruhiwa katika mashambulio

Katika maeneo tofauti ya magharibi mwa Tigray, mambo yafuatayo yalikuwa yanafanyika:

  • Kwanza mashambulio ya makombora
  • Kisha vikosi vya serikali vikaingia
  • Na nyayo zao zilikuwa kutoka kwa vikosi maalumu Amhara na fanos.

Katika mji wa Adebay, tuliwahudumia wagonjwa kwa siku mbili. Baadae mapigano yakawa makali na kufika karibu kliniki tuliyokuwa.

Ethiopian soldiers on the back of a lorry on a road near the city of Humera, Ethiopia - 21 November 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ethiopia, wanaonekana hapa wakiwa kwenye barabara karibu na Humera, waliwasili mjini humo baada ya mashambulio maalum

Tuliamua kuwasafirisha wagonjwa wetu kwa lori hadi maeneo mengine ya Tigray, ambako angalau kulikuwa salama, huku sisi tukitembe kwa miguu kupitia njia za ndni karibu kilo mita 250

Tulijificha huko kwa siku mbili. Siku ya tatu tukaamua kuondoka tena kwasababu usalama ulikuwa umezorota baada ya watu zaidi kuuawa, ghasia zaidi zikiendelea Adebay. Tulikuwa tukisikia milio ya risasi na wakati mwingine milipuko ya makombora mazito.

Kwa hivyo tukaamua kutoroka kwa miguu hadi mpaka wa Sudan katika mji wa Hamdayet, ambao ni karibu kilo mita 50 kutoka mahali tulikuwa. Wanamgambo walitufuata kupitia njia za mmsituni hadi ukingo wa Mto Tekeze .

Map of Tigray

Kwa sasa niko katika kambi ya wakimbizi, Bado nawahudumiwa wagonjwa. Nina wagonjwa kutoka maeneo tofauti ya Tigray - wengine kutoka umbali wa karibu kilomita 300 kutoka mpakani. Watu waliotembea kwa miguu wameona miili mingi ya raia waliofariki njiani.

Nina wagonjwa ambao wanasema waliona vikosi vya Eritrea ndani ya jimbo la Tigray vikifanya ukatili, kuchoma nyumba na kuharibu memea mashamba.

Haya yote yalifanyika gizani, wakati huduma za intaneti na umeme zilipokatizwa na mfumo wa benki kufungwa. Hakuna anayejua ni nini hasa kilifanyika ndani ya Tigray.

Nimesema ukweli, kulingana na kile nilichoona. Natumai watuwa watatuma wachunguzi huru kubaini kilichotokea.

Short presentational grey line