Wanasayansi bado hawajajua kilichosababisha mtoto kuzaliwa na sehemu tatu za uume

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanasayansi wamezidi kushangazwa na kilichosababisha mtoto mmoja wa kiume aliyezaliwa na sehemu tatu za uume nchini Iraq miezi kadhaa baada ya kumfanyia oparesheni ya kuondoa sehemu mbili .

Tukio hilo watalaam wanasema ndilo lilikuwa la kwanza kwa binadamu kuzaliwa na sehemu tatu za siri katika kinachojulikana kitaalam kama triphallia. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na sehemu tatu za uume katika eneo la Duhok nchini Iraq na mara ya kwanza madaktari walimuona akiwa na miezi mitatu .

Tangia hapo wamekuwa wakiendelea na utafiti wa kung'amua kwanini alizaliwa na sehemu hizo tatu lakini hadi sasa hawajapata majibu .

Alifanyiwa upasuaji kuondoa sehemu mbili kati ya hizo tatu ambazo zilikuwa zimeanza kujitokeza katika shina la eneo la korodani .Sehemu ya tatu ilikuwa katika eneo la kawaida ambapo uume wa mwanamme huwa .

Kulingana na uchunguzi wa kisa hicho uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Upasuaji la Novemba mwaka jana , kijana huyo alikuwa akiendelea vizuri katika ziara ya ufuatiliaji mwaka mmoja baada ya upasuaji.

Uume wa ziada, au "usio wa kawaida" ni hali nadra ya kuzaliwa, inayotokea mara moja tu katika kila watoto milioni 5 hadi milioni 6 wanaozaliwa kulingana na watafiti.

Sehemu mbili kuondolewa

Kiwango cha ukuaji wa sehemu hizo kwa jina la kitalaam -phallus hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine

Katika tukio la mtoto huyo wa Iraq, sehemu hizo mbili za ziada zilikuwa na tishu za erectile, ziitwayo corpus cavernosum, ambazo hujaa damu wakati wa kuamka, na vile vile tishu inayoitwa corpus spongiosum, ambayo inasaidia mrija unaotumiwa kupitisha mkojo.

Lakini sehemu hizo za uume wa ziada hazikuwa na mirija ya kupitisha mkojo yaani urethra . Hii ilifanya kuondolewa kwa upasuaji kwa viungo hivyo vya ziada kuwa rahisi.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Haijulikani sana juu ya kwanini uume wa ziada huibuka, alisema John Martin, profesa wa anatomia katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha St. Louis

Martin na wenzake wanaofundisha anatomia kwa kutumia mpango wa kuchangia sehemu za miili ya watu wakati mmoja waligundua kuwa mmoja wa wafadhili wa mwili wao alikuwa na diphallia, au sehemu mbili za uume. Mwanamume huyo, ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 84, alikuwa na sehemu mbili za siri zenye ukubwa kamili na pengo la urethra kati yazo katika shina la korodani

Mfadhili hakutaja hali yoyote kwenye fomu zake za kuchangia mwili. Alikuwa na watoto wawili, Martin alisema, lakini watafiti hawajui ikiwa walikuwa watoto wake kibaolojia au ikiwa teknolojia yoyote ya uzazi ilikuwa muhimu kwa mwanamume huyo kupata watoto.

Hakuna uhusiano na kuathiriwa kwa jeni

"Alikufa mwanzoni mwa miaka ya 2000, kwa hivyo wakati alipokuwa hai huenda upasuaji hakuwa chaguo, labda," Martin aliiambia Live Science. "Ni tofauti tu na leo ambapo kitu kama hicho kingegunduliwa mapema na uwezekano mkubwa wa upasuaji kufanywa."

Martin na wenzake walifanya vipimo vya maumbile kwa wafadhili ili kuona ikiwa wanaweza kujua sababu ya matukio haya yasio ya kawaida. Waligundua mabadiliko kadhaa katika jeni inayojulikana kuhusika katika ukuzaji wa sehemu za siri, pamoja na zingine zinazochangia kuunda muundo wa nywele unaitwa cilia kwenye seli za kiinitete.

Cilia hizi ni muhimu sana katika ukuzaji, Martin aliiambia Live Science , kwa sababu hupepea kwa mwelekeo maalum, ikipunguza protini kuelekea upande mmoja au mwingine wa kiinitete kinachokua

Hali isiyo ya kawaida ya ukuaji katika jeni za cilia pia zimeonekana kusababisha maumbile yasiyo ya kawiada ya sehemu za siri na kuleta hali kama situs inversus, ambayo viungo kwenye kiwiliwili hupinduliwa ili viwe pande tofauti kutoka kwa nafasi zao za kawaida.

Watafiti pia walipata mabadiliko katika jeni ambayo husaidia kudhibiti shughuli za jeni zingine katika ukuaji na katika jeni zinazohusika na vipokezi vya androjeni, homoni ambazo zina ushawishi wa kiume na zinazohusika katika ukuaji wa kijinsia.

Jeni nyingine inayohusishwa na ukuaji wa kijinsia ni inayoitwa inayoitwa 'sonic hedgehog' Martin alisema, ambayo ni muhimu kwa mwili wote kukuza ukuaji wakati wa ustawi wa kiinitete.

Haijulikani jinsi jenetiki zinavyofanana visa vya diphallia(Sehemu mbili za uume) au ikiwa matokeo haya yanatumika kwa kisa cha aina moja ya triphallia(Sehemu tatu za uume)

Madaktari waliomtibu mtoto huyo wa Iraqi hawakupata chochote katika historia ya familia ya mtoto au historia ya matibabu, kama vile kufichua dawa au kemikali wakati wa ujauzito, ambayo ingeelezea hali ya kuzaliwa na sehemu tatu za uume .

Mtoto alikuwa mzima kiafya isipokuwa kwa mkusanyiko wa maji kwenye korodani, ambayo ni hali ya kawaida na inayotibiwa kwa urahisi utotoni