Sarah Baartman: Mfahamu Mwanamke mweusi kutoka Afrika Kusini aliyesafirishwa Ulaya kwa maonesho

Chanzo cha picha, Science Photo Library
Karne mbili zilizopita Sarah Baartman alifariki baada ya kuishi akifanya "maonyesho ya vituko ". Sasa tetesi kwamba kuna uwezekano wa kutengenezwa kwa filamu ya Hollywood inayohusu maisha ya Baartman zimeibua utata.
Sarah Baartman alifariki dunia tarehe 29 Disemba 1815, lakini maonyesho yake yakaendelea
Ubongo wake, mifupa, na viungo vyake vya uzazi viliendelea kuoneshwa katika jumba la makumbusho ya Paris hadi mwaka 1974. Masalia yake hayakuwahi kuhamishwa na kuzikwa mpaka ilipofika mwaka 2002.
Aliletwa Ulaya kwa njia za madai ya uongo na daktari Muingereza , akiitwa kwa jina la jukwani "Hottentot Venus", ambapo alioneshwa katika kumbi za "maonyesho ya vituko" mbali mbali katika miji ya London na Paris, huku umati wa watu ukialikwa kuyaangalia makalio yake makubwa.
Lakini sasa anaangaliwa na wengi kama kielelezo cha unyonyaji wa kikoloni na ubaguzi wa rangi, kejeli na utumiwaji wa watu weusi kama vyombo.
Taarifa kwamba Beyonce anapanga kuandika na kucheza katika filamu kuhusu Baartman zilikanushwa na wawakilishi wa mwanamuziki huyo. Lakini minong'ono ilikuwa tayari imesababisha hofu ya kutosha.
Jean Burgess, chifu kutoka kikundi cha Khoikhoi ambacho ndicho alichotoka Baartman , alidai kuwa Beyonce alikosa "utu wa kimsingi wa binadamu kuweza kuwa na thamani ya kuandika hadithi ya Sarah, mbali na kucheza filamu kama Sarah ".
Lakini Jack Devnarain, mwenyekiti wa Shirikisho la wachezaji filamu wa Afrika Kusini alisema kuwa watengenezaji wa filamu walikuwa na ''haki ya kuelezea hadithi za watu unaopata kuwa wanavutia na hilo ndio tunapaswa kuwa waangalifu na hilo".
Hata katika kukanusha kuhusika katika filamu, alisema mwakilishi wa Beyonce : "Hii ni hadithi muhimu ambayo inaweza kuelezewa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Maisha ya Baartman yalikuwa ni moja ya maisha magumu sana.
Inadhaniwa kuwa alizaliwa katika jimbo la Afrika Kusini la Eastern Cape mwaka 1789, mama yake alifariki dunia alipokuwa na umri wa miaka miwili na baba yake, mfugaji, alifariki alipokuwa katika umri wa kubalehe.
Aliingia katika utoaji wa huduma za nyumbani mjini Cape Town baada ya mkoloni Mholanzi kumuua mwenza wake, ambaye alikuwa tayari amezaa naye mtoto ambaye alikufa.
Mwezi Oktoba 1810, ingawa hakuwa amesoma, Baartman alidai kuwa alisaini mkataba na daktari wa upasuaji wa meli ya Uingereza William Dunlop na mjasiriamali chotara Hendrik Cesars, ambaye alimfanyia kazi kama kijakazi, akisema alisafiri kwenda Uingereza kushiriki katika maonyesho.
Haya yalimfanya asababishe mvuto wakati alipokuwa akifanya onyesho katika eneo la Piccadilly Circus jijini London baada ya kuwasili.
"Unapaswa kukumbuka hilo, wakati ule ,ilikuwa ni kitu kilichokuwa kwenye fasheni na kupendwa kwa wanawake kuwa na makalio makubwa, kwa hiyo watu wengi walimuonea wivu kwa kile alichokuwa nacho cha asili yake, bila kuongezea umbo lake ," anasema Rachel Holmes, mwandishi wa kitabu cha maisha na kifo cha Bi Baartman-The Hottentot Venus: The Life and Death of Saartjie Baartman.
Jukwaani alivaa nguo ya kubana mwili wake ( skin-tight) yenye rangi, pamoja na shanga na manyoya na alikuwa akivuta tumbaku. Wateja matajiri walikuwa wanalipa pesa zao kwa ajili ya kuburudishwa kibinafsi majumbani mwao, huku wageni wakiruhusiwa kumgusa.
Kuwasili kwake nchini Uingereza kulitokea wakati kukiwa na tetesi juu ya iwapo Lord Grenville na muungano wake Whigs - wanaofahamika kama "makalio mapana" kwasababu ya ukubwa wa nyuma wa Grenville- wangejaribu kuiteka serikali . Hii ilikuwa ni zawadi kwa wachoraji wa vibonzo.
Katuni moja, iliyokuwa na kichwa cha habari-A Pair of Broad Bottoms, iliwaonesha Grenville na Baartman wakiwa wamesimama mmoja nyuma ya mwingine, huku mtu mwingine akipima ukubwa wa makalio yao.

Chanzo cha picha, BRITISH MUSEUM
Mapromota wa Baartman walimpatia jina la bandia "Hottentot Venus", huku "hottentot" - sasa ikionekana kama udhalilishaji- wakati ule likitumiwa na Waholanzi kuelezea makundi ya Khoikhoi na San, ambao kwa pamoja huunda jamii ya watu wanaofahamika kama Khoisan.
Himaya ya Uingereza ilikuwa imezuia biashara ya utumwa katika mwaka 1807, lakini sio utumwa wenyewe. Hata hivyo, wanaharakati walishtushwa na jinsi Baartman alivyotumikishwa London.
Waajiri wake walishitakiwa kwa kumshikilia Baartman kinyume na matakwa yake, lakini hawakuhukumiwa, huku Baartman mwenyewe akitoa ushahidi uliowatetea.
"Swali linasalia-je Baartman alilazimishwa, kama wanaharakati wa haki za binadamu wanavyodai, au alikuwa katika maonyesho hayo kwa hiari?" anasema Christer Petley, mwalimu wa historia katika Chuo kikuu cha Southampton .
"Iwapo alilazimishwa, lazima alihisi kutishwa kuelezea ukweli katika mahakama. Hatutajua hilo kamwe.
Baada ya kesi, onyesho la Baartman taratibu lilianza kupoteza umaarufu wake miongoni mwa watazamaji katika jiji kuu la London na akaenda katika maonyesho katika maeneo mengine ya Uingereza na Ireland.

Mwaka 1814 alihamia Paris na Cesars
Alikuwa mtu maarufu sana, akinywa kahawa katika mgahawa wa Cafe de Paris na kuhudhuria sherehe za kijamii. Cesars alirejea Afrika Kusini Baartman akawa muonyeshaji mwenye "tabia ya kinyama", akiwa na jina la jukwaani - Reaux. Alikunywa pombe kali, kuvuta sigara nzito na , kulingana Holmes, alikuwa "huenda kahaba" wake.
Baartman akikubali kufanyiwa utafiti na kuchorwa na kikundi cha wanasayansi na wasanii lakini alikataa kuonekana akiwa uchi wa mnyama mbele yao, akidai kuwa hilo lingekuwa chini ya heshima na utu wake - hakuwahi kufanya hili katika maonyesho yake mengine.
Kipindi hiki kilikuwa mwanzo wa utafiti wa kile ambacho kinafahamika kama "sayansi ya rangi ", anasema Holmes.
Baartman alifariki akiwa na umri wa miaka 26. Sababu ya kifo chake ilielezewa kama "majeraha na ugonjwa wa kulipuka". Ilisemekana kuwa hilo lilitokana na maradhi ya kifua, kaswende au ulevi.
Georges Cuvier, ambaye alicheza densi na Baartman katika moja ya sherehe zilizofanyika katika Reaux nchini Ufaransa, alitengeneza kadi iliyoonesha umbile la mwili wake kabla ya kuichana.
Alitunza mifupa yake na kuchukua ubongo wake na sehemu zake za siri, na kuziweka katika birauli na kuiweka kwenye jumba la maonyesho ya binadamu la Paris . Mabaki ya mwili wake yalioneshwa kwenye jumba hilo hadi mwaka 1974, kitu ambacho Holmes anakielezea kama "cha kutisha"
Baada ya kuchaguliwa kwake aliyekuwa rais wa Afrika Kusini 1994 , Nelson Mandela aliomba kuhamishwa kwa mabaki ya mwili wa Baartman na sanamu yake . Serikali ya Ufaransa hatimaye ilikubali na mwezi Machi mwaka 2002 mabaki hayo yakapelekwa Afrika Kusini.
Mwezi Agosti mwaka huo, mabaki yake yalizikwa katika eneo la Hankey, katika jimbo la Eastern Cape province, miaka 192 baada ya Baartman kuondoka akielekea Ulaya.

Chanzo cha picha, Alamy












