Mwanaume wa Los Angeles nchini Marekani aliyepinga chanjo za Covid-19 afariki kutokana na corona

Chanzo cha picha, CBS
Mwanaume mmoja kutoka jimbo la California, nchini Marekani ambaye aliipinga na kuidhihaki chanjo za Covid-19 kwenye mitandao ya kijamii amefariki baada ya kuugua virusi hivyo kwa mwezi mzima.
Stephen Harmon, ambaye ni muumini katikia kanisa la kubwa la Hillsong, amekuwa mpinzani mkubwa aliyepaza sauti kupinga chanjo , huku akitengeneza msururu wa maneno ya kebehi kuhusu chanjo.
"Nina matatizo 99 lakini chanjo sio moja wapo," Bw Harmon mwenye umri wa miaka 34 alituma ujumbe wa Twitter kwa wafuasi wake 7,000 mwezi Juni.
Alitibiwa kwa maradhi ya kifua -nimonia na Covid-19 katika hospitali iliyopo nje ya Los Angeles, ambako alikufa siku ya Jumatano.
Siku chache kablya ya kifo chake, Bw Harmon alirekodi kumbukumbu ya jinsi alivyopambana kuwa hai, akituma picha zake akiwa katika kitanda cha hospitali.
"Tafadhali ombeni ninyi nyote, wanataka kuniwekea mirija, na kuniweka kwenye kifaa cha usaidizi wa kupumu," alisema.
Unaweza pia kusoma:
Katika ujumbe wake wa mwisho wa Twitter alioutuma siku ya Jumatano , Bw Harmon alisema kuwa alikuwa ameamua kuwekewa mrija wa hewa.
"Sijui ni lini nitaamka, tafadhali ombeni," aliandika.
Licha ya kuhangaika kwake na virusi vya ciorona, Bw Harmon bado alisema kuwa angelikataa chanjo, akisema kuwa imani ya dini yake ingemlinda.
Kabla ya kifo chake, alikuwa akikebehi kuhusu janga na chanjo, akiushirikisha umma mtandaoni kwa kusema aliamini Biblia zaidi ya mtaalamu wa Marekani wa ngazi ya juu wa ugonjwa huo Dokta Anthony Fauci.
Muasisi wa Kanisa la Hillsong Brian Houston alithibitisha taarifa ya kifo chake katika ujumbe wa Twitter siku ya Alhamisi.
"Ben amefariki sasa hivi kwetu ni taarifa ya kusikitisha kwamba rafiki yetu mpendwa , Stephen Harmon amefariki kutokana na Covid . Inavunja moyo," Bw Houston alisema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Katika ujumbe wa mtandao wa Instagram, alitoa rambi rambi zake kwa Bw Harmon.
"Alikuwa mmoja wa watu wakarimu zaidi ninaowafahamu na alikuwa na mengi sana mbele yake," aliandika kwenye Instagram.
"Kila mara alikuwa akija kwenye mchezo wa soka wa wajukuu wetu na watu wengi watamkosa . RIP."
Aliongeza kuwa Kanisa linawatia moyo waumini wake "kufuata mwongozo wa madaktari wao".
California imeshuhudia ongezeko la wagonjwa wa Covid-19 katika wiki za hivi karibuni, wengi wao wakiwa ni wale wanaopelekwa hospitalini ambao hawakuchanjwa chanjo ya corona.













