Joto kali Canada: Kwanini joto kali linaweza kuua?

Chanzo cha picha, Getty Images
Joto kali ambalo halijawahi kushuhudiwa hapo awali, sasa hivi limefikia nyuzi joto 50 huko Canada na sehemu zingine za kaskazini mashariki mwa Marekani.
Hali hii inasababishwa na hewa ya joto kali yenye shinikizo la juu ambayo imeanzia California hadi maeneo ya Aktiki.
Vifo 130 vya ghafla vimerekodiwa huko Vancouver peke yake tangu mwezi Februari huku joto kali zaidi likibainiwa kama chanzo.
Lakini vipi unaweza kupunguza joto kali ni hatua gani unazoweza kuchukua kukabiliana na hali hii?
James Gallagher, mwanahabari wa BBC anayeangazia masuala ya sayansi na Afya amejibu maswali yafuatayo.
Joto kali lina athari gani mwilini?
Ama kiwe kipindi cha baridi au joto kali, miili yetu hung'ang'ana kuwa na kiwango cha joto stahiki takriban nyuzi joto 37.5.
Nyuzi joto kiwango hicho ndio miili yetu imezoea kutekeleza shughuli zake.
Lakini, wakati zebaki inaongezeka, mwili unatakiwa kujitahidi zaidi kudumisha kiwango cha joto stahiki.
Kisha, inafungua mishipa ya damu karibu na ngozi kuachia joto linalokuwa jasho.
Wakati jasho linapojifukiza, kiwango cha joto kinaanza kupungua kwa kiasi kikubwa kwenye ngozi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tatizo liko wapi?
Joto linaweka shinikiza ndani ya mwili na kusababisha joto kuongezeka, huku mwanadamu naye akiendelea kupata msongo.
Kufungua mishipa ya damu kunafanya shinikizo la damu kupungua na kufanya moyo kuwa na kazi ya ziada na kupiga kwa haraka ili kusukuma damu kwenye mwili mzima.
Hili linaweza kusababisha dalili kama vile harara kwa kujikuna au kufura miguu wakati mishipa ya damu inavuja maji.
Lakini ikiwa shinikizo hilo litapungua sana, damu haitafika katika viungo kunako hitajika damu na kuongeza hatari ya kupata mshutuko wa moyo.
Wakati huo huo, kutoa jasho kunafanya mtu kupoteza maji mengi mwilini na chumvi na muhimu zaidi, kunasababisha madaliko kati yake na mwili.
Na hili, pamoja na shinikizo la chini la damu, kunaweza kusababisha uchovu unaotokana na joto dalili zake zikiwa ni kama ifuatavyo:
- kuhisi kusunzi au kizunguzungu
- kuzimia
- kuchanganyikiwa
- kuwa mgonjwa
- misuli kukakamaa
- kuumwa na kichwa
- kutoa jasho jingi
- kuchoka

Chanzo cha picha, Getty Images
Nastahili kufanya nini ikiwa nitakutana na mtu mwenye kutaabika kwa joto kali?
Ikiwa wanaweza kupata maeneo ya kutuliza joto kali ndani ya kipindi cha nusu saa, basi uchovu unaotokana na joto kali unakuwa hauna tena nguvu.
Ushauri kutoka wizara ya afya ya Uingereza ni kwamba:
Mpeleke maeneo ya kutuliza joto.
Alale chini na kuweka miguu yake juu kidogo.
Mpe maji mengi ya kunywa; vinywaji vya kuongeza maji mwilini pia anaweza kutumia.
Jitahidi kumtuliza ngozi: mnyunyizie au mpake maji ya baridi na apate hewa.
Vifaa vya kutoa baridi katika maeneo ya kwapa au kwenye shingo pia kunasidia.
Hata hivyo, ikiwa mtu huyo atashindwa kurejea kuwa sawa ndani ya kipindi cha dakika 30, kitakachofuata ni kuzirai kutokana na joto kali.
Hapo mtu anahitaji kupata matibabu haraka sana.
Watu wanaozirai kwasababu ya joto kali wanaweza kuacha kutoa jasho hata kama wana joto kweli. Joto lao la mwili linaweza hata kupita nyuzijoto 40 za selsiasi.

Chanzo cha picha, Reuters
Ni kina nani walio katika hatari?
Watu wenye afya njema wanastahili kukabiliana na hali ya joto kali lakini kuna wale walio katika hatari zaidi.
Watu wazee au wale ambao wameugua kwa muda mrefu kama vile ugonjwa wa moyo, huenda wakawa na wakati mgumu kukabiliana na msongo unatokana na joto kali mwilini.
Ugonjwa wa kisukari aina ya 1 na 2, huenda kukasababisha mwili kukosa maji kwa haraka na athari ya magonjwa mengine kunaweza kuhitilafiana na mishipa ya damu na uwezo wa kutoa jasho.
Pia ni muhimu kuweza kutambua kwamba mwili wako una kiwango cha juu cha joto na kuchukua hatua.
Hili ni jambo ambalo huwa tunalichukulia kama mzaha. Hata hivyo, watoto na wale wachanga, wale wasioweza kutembea mwendo mrefu kutoka sehemu moja hadi nyingine wanaweza kuwa katika hatari.
Pia, magonjwa wa ubongo kama vile dementia huenda kukafanya mtu asijue kuwa amepata tatizo hili au kushindwa kufanya chochote.
Pia, wasiokuwa na makazi huenda wakawa katika hatari ya kumwilikwa na jua zaidi na wale wanaoishi katika maeneo ya juu au ghorofa ya juu pia nao wapo katika hatari ya kukumbwa na joto kali zaidi.

Chanzo cha picha, NATHAN HOWARD / GETTY IMAGES
Kuhakikisha mwili umepata kitu cha kutuliza joto na kuongeza maji ni muhimu kukabiliana na hali hii.
Je joto kali linaua?
Ndio.
Kila mwaka maelfu ya vifo hutokana na kiwango cha juu cha joto.
Wengi wao watapata mshtuko wa moyo na kiharusi kunakosababishwa na juhudi za kuhakikisha joto la mwili liko sawa.
Vifo vingi vinatokewa nyuzi joto ikipita 25-26.
Hatahivyo, ushahidi unaonesha kuwa vifo kusababishwa na joto kali msimu wa kuchipua au mapema msimu wa joto wala sio kilele cha msimu huo.
Ushahidi mwingine kutokana na hali kama hizi zilizotangulia, pia unaonesha kuwa kuongezeka kwa idadi ya vifo hutokea haraka sana ndani ya saa 24 ya kipindi cha joto kali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipi cha kufanywa wakati wa joto kali?
Ushauri ni rahisi kabisa: Hakikisha upo sehemu yenye baridi.
Hakikisha unakunywa maji ya kutosha au maziwa. Chai na kahawa pia sio mbaya lakini kuwa mwangalifu na kiwango cha pombe unachokunywa kwasababu kunaweza kuongeza hatari ya kukosa maji mwilini.












