Anne Kansiime: Msanii wa vichekesho aliyevishwa pete ya uchumba, huku akiwa na hasira

Anne Kansiime Msanii wa vichekesho nchini Uganda ni maarufu Uganda na nje ya Uganda

Chanzo cha picha, kansiime

Maelezo ya picha, Anne Kansiime Msanii wa vichekesho nchini Uganda ni maarufu Uganda na nje ya Uganda
Muda wa kusoma: Dakika 2

Msanii maarufu wa Uganda Anne kansiime amesema mchumba wake alimuomba awe mke wake baadaya ''kumuudhi''.

Hata hivyo Bi Kansiime anasema aliamua kukubali ombi la uchumba kutoka kwa mpenzi wake Abraham Tukahiirwa al maarufu Skylanta Skylanta .

Wawili hao walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume hivi karibuni.

Kansiime, ambaye ni msanii wa vichekesho maarufu si kwa Uganda tu bali kwa Afrika nzima alituma ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram ambao uliambatana na picha , kionesha pete mkononi aliyovalishwa na mpenzi wake ambapo aliwaomba mashabiki wake aliowaita ''ninjas'' wamsaidie kusherehekea tukio.

Ujumbe huo ulifuatiwa na jumbe za wafuasi wake zilizomiminika za kumpongeza na kumtakia kheri Bi Kansiime na Skylanta.

"Huenda nimempata mwenza wa maisha katika jox'', aliandika.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Baadaye alituma ujumbe wa video wa dakika 12 kwenye mtandao wa YouTube akielezea ni kwa jinsi gani alivyomkasirikia mpenzi wake wa kiume, ambaye sasa ni mchumba wake, ambaye alikuwa amesahau kuhusu siku ya akia mama Mother's Day mwaka huu.

"Fikiria kwa mara ya kwanza Kansiime amekuwa mama na Sky (Skylanta) anajifanya kusahau siku hii, kana kwamba hakuna kilichotokea kwangu siku ile.

Anne Kansiime na walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume mwezi Aprili, 2021

Chanzo cha picha, Anne Kansiime /Instagram

Maelezo ya picha, Anne Kansiime na walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume mwezi Aprili, 2021

"Sky, ulisubiri nijifungue mtoto wetu mzuri wa kiume, ukasahau kunitakia siku yenye furaha ya akinamama . Hakunipatia hata maua achana na kikombe cha chai…Nilikukasirikia sana…Kwahiyo nilikaa kimya nikasubiri siku moja baadaye ndio kurejea tena kuzungumza naye. "Pia nilikuwa na mambo mengi akilini mwangu, lakini usijali tutaisherehekea ."

Anne Kansiime na mchumba wake Abraham Tukahiirwa aka Skylanta ambaye ni msanii wa muziki

Chanzo cha picha, Kansiime/ Instagram

Maelezo ya picha, Anne Kansiime na mchumba wake Abraham Tukahiirwa aka Skylanta ambaye ni msanii wa muziki

Kwa ucheshi, Kansiime alishangaa ni kwa kiasi gani mpenzi wake wa kiume alikuwa na mambo mengi saana na jinsi watakavyozozana atakapofika nyumbani.

Hatahivyo, siku ilipopita, mpenzi wake alikuja kumtakia siku njema ya wamama na kumvalisha pete ya kumuomba awe mke wake katika video iliyochukuliwa ambayo Kansiime aliipakua kwenye mtandao wa YouTube.