Eneo la kuvutia nchini Venezuela ambako hakuna anayetaka kuishi licha ya kuwepo nyumba nzuri

Barlovento has been a traditional vacation destination for middle and upper class Venezuelans.

Chanzo cha picha, ANDRES MORANTE

Kwa miongo kadhaa lilikuwa ni eneo la paradiso lililokuwa maarufu ambapo watu walifika kubarizi kwa siku zao za mapumziko , eneo ambalo Wavenezuela wengi walikwenda kujivinjari na kuliwazwa na bahari ya Caribbean ili walau kusahau mahangaiko ya maisha ya kila siku ya jiji.

Sasa ni ngome ya wahalifu.

Kila wikendi, mamia ya wakazi wa jiji kuu la Caracas walikwenda mashariki mwa barabara kuu ambayo wakati huo ilikuwa moja ya barabara zenye shughuli nyingi nchini humo kusaka jua na raha.

Katika eneo la Barlovento, jimbo lililopo kaskazini mwa Venezuela lililojaa vivutio vya utalii kama vile majumba ya kifahari na fukwe za kuvutia, nyingi kati ya nyumba za kifahari ambazo wakati mmoja zilitumiwa na watalii sasa zimetelekezwa na kubaki mahame.

Fernando Valera, mmoja wa watu wachache walionunua nyumba katika mji wa Río Chico na ambaye anasita kuondoka, anasema: "Ile ni nyumba ambayo inauzwa kwa dola 3,000 za kimarekani, lakini wengi wa wamiliki walitelekeza nyumba zao tu na kuondoka ."

Kuna mali nyingi zilizopo katika mji huo. Wengi wanaziuza kwa bei ya chini sana au wamiliki wake wanaamua kuzitoa tu bure kwa watu walio tayari kuzitunza.

The Police Special Actions Force has been accused of committing extrajudicial executions. (File image)

Chanzo cha picha, Getty Images

Raúl López, ambaye alikuwa katibu wa Maendeleao ya kiuchumi ya jimbo la Miranda, ambalo liko jirani na jimbo la Barlovento , anakumbuka kuwa " katika nyakati nzuri, nyumba hapa iliuzwa dola 80,000 za Kimarekani.

"Sasa nilisikia mtu ambaye alikuwa anauza nyumba zake mbili kwa dola 30,000 ."

Lakini, licha ya kuwa nyumba hizi zina kila kitu, watu wa kuzinunua hawajitokezi.

Madimbwi ya maji, na hata viwanja vya gofu vilijengwa. Biashara ilikuwa na malipo . Lakini sasa mambo yamebadilika.

Nini kilichobadilika?

Mambo yalianza kubadilika kwa haraka katika mwaka 2013 wakati serikali ilipoanza mchakato wa mazungumzo na makumi ya magenge ya wahalifu ili kupigia debe mpango wake wa kuwashawishi waweke silaha chini na kuwaingiza katika jamii.

Waliuita mpango huu Quadrants of Peace, ambapo maeneo yaliyoacha ghasia, serikali ilisitisha kuwanyanyasa wahalifu na kuwapatia raslimali ili waweze kuimarika kiuchumi bila kutekeleza uhalifu.

"Maeneo hayo ya amani yaligeuka haraka hifadhi ya magenge na kutoka Barlovento waliweza kutekeleza uhalifu wao katika mji wa Caracas,"anasema López.

Amri ilianza kutolewa kwa wamiliki wa nyumba . "Kwanza walikabiliwa na wizi mdogo, kwa hiyo kila wakati walipokuja nyumbani kukaa nyakati za wikendi walikuta vitu vimeibiwa, lakini baada ya muda mambo yalikuwa mabaya zaidi na utekeji nyara ulianza ."

"Nyingi kati ya nyumba nzuri zenye vidimbwi vya kuogelea na ukarabati pekee wa vidimbwi hivyo tayari unagharimu pesa nyingi ",anasisitiza López.

This image from a few years ago shows some of the houses in the area.

Fernando Valera ni mmoja wa watu wachache ambao hawakukata tamaa anasema " Nimewahi kuibiwa hapa mara tano," anasema..

"Mara ya kwanza walikuwa kati ya wanaume 15 na 20 wakiwa na silaha ndefu na magwanda ya kijeshi. Waliondoka mlimani, wakamuelekezea bunduki mke wangu na wapwa wangu, ambao walikuwa kwenye kidimbwi cha kuogelea, na kuniondoa ndani ya bafu ambako nilikuwa ninaoga ."

Valera anakumbuka kwamba walikuwa na mienendo ya . "Kulikuwa na kiongozi ambaye alikuwa akituamrisha na kutushughulikia kwa usahihi . Wengine walitii, walibeba kila kitu na kundoka navyo."

Wengine walikuwa wakifanya mambo yake "kitalaamu" sana. "Katiak moja wapo ya uvamizi walikuwa wanaonekana wenye hasira na kumuwekea kisu mke wangu shingoni mwake."

"Walichukua kila kitu"

Baada ya wizi mwingi, makazi yake yalionekana wazi. Walichukua vifaa vyake muhimu vya jikoni vya kifahari, na sebule yake, na viti kadhaa na CD player ya zamani . " Sitaki kuwa na kitu chochote ambacho kinavutia wizi, kwasababu sasa wanakuja na kuchukua kila kitu ."anasema.

Sawa na wengine wengi ambao walipitia hali kama yake katika eneo hilo, familia haitaki kurejea katika eneo ambalo lilikuwa ni eneo aliloota kulifanya kuwa eneo lao la mapumziko yao.

Wahalifu "walimalizwa "

Polisi katika eneo la Río Chico wameimarisha uwepo wao kwenye eneo hilo katika siku za hivi karibuni na Fernando anasema ameishi kwa utulivu zaidi tangu walipoweka kikosi cha makamanda wa ulinzi cha kitaifa karibu na nyumba yake. Wanapita na kumuangalia mara kwa mara.

Lakini baadhi ya mbini za polisi zimesababisha utata na ukosoaji wa kimataifa wa serikali ya Rais Nicolás Maduro.

ramani

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu imeripoti baadhi ya visa vya "mauaji ya kiholela" nchini Venezuela katika miaka ya hivi karibuni.

Serikali haikujibu ilipoulizwa na BBC kutaka kupata taarifa kuhusu tuhuma hizi.

Sio kwamba ninafurahia kwamba wanauliwa, lakini ninatumai kuna utulivu," anasema Valera kuhusu mauaji ya wahalifu.

Magofu ya kisasa

Katika manispaa ya Río Chico, sio vigumu kupata majuumba ya zamani ya kifahari yakigeuka kuwa magofu.

Matangazo ya kitalii ambayo yamebaki kwenye mtandao yanaelezea eneo la Caño Copey kama "aneo ambalo utapata huduma muhimu za utalii za siku ya kuwa kimya katika fukwe ."

Pia katika tovuti kuna video ambazo zinaonesha picha iliyopigwa kutoka juu ya nyumba na vidimbwi vya kuogelea, fukwe na mtandao wa mifereji ya maji inayopita kwenye eneo hilo.

Huku likiwa halina wageni wa mjini wa kuvinjari, sasa ni eneo la wakulima wa kakao ambao wameyalipa magenge ya wahalifu ambao Barlovento ngome yao.

Wale waliobaki hapa wamelazimika kuzoea kutoweka kwa utalii, jambo ambalo limesababisha atahri za mzozo wa kiuchumi kuwa hata mgumu zaidi.

Fernando Valera has been assaulted 5 times at his home, but he is reluctant to leave it.
Maelezo ya picha, Fernando Valera ameshambuliwa mara tano nyumbani kwake lakini hataki kuondoka

Quintana, kwa mfano, huwalisha watoto wake wawili zinazomea katika bustani yake na samaki wadogo ambazo anaweza kuvua katika mwambao ambao kwa sasa hauna watu kwasababu mshahara wake unaweza tu kutosha kununua paketi chache tu za mchele.

Anatamani siku ambazo mambo yalikuwa tofauti .

"Katika matamasha ya kitamaduni ( carnivals )n au wikendi, watalii wengi walikuja na kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiishi na kufanya shughuli zao katika majumba ya kifahari kwenye fukwe ," alielezea, huku akionesha kwa kidole majumba yaliyokbaki pweke kwenye fukwe za bahari.

"Wenye majumba haya walikuwa wakienda kwenye paa zake mwisho wa siku kutazama jua linavyotua na kunywa pamoja vinywaji huku wakisikiza muziki ," anakumbuka.

Walipoacha kuja, waporaji walijitokeza . "Walipora vyoo, milango, madirisha, kila kitu ..."

Na inaweza hata kuwa vibaya zaidi. "Mara mtu anapojitokeza kuwa anaishi maisha ya kawaida, wanamnyanyasa au kumteka nyara na kumlazimisha kulipa pesa ."

"Ni nani atakayetaka nyumba hapa?" Quintana alishangaa.