Mauaji ya Daunte Wright: Watu 40 wakamatwa baada ya maandamano mapya kukumba Minnesota

Protester in Brooklyn Center

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 2

Karibu watu 40 wamekamatwa kaskazini mwa Minneapolis katika usiku wa pili wa ghasia kufuatia tukio la polisi kumuua kwa kumpiga risasi mtu mweusi.

Waandamanaji katika mji wa Brooklyn Center walikaidi amri ya kutotoka nje na kuwarushia vifaa butu polisi, ambao walijibu kwa kuwarushia vitoa machozi.

Polisi wanasema Daunte Wright, 20, alipigwa risasi na kuuawa baada ya afisa kutumia kimakosa buduki yake akidhani ni kifaa cha kufisha ganzi dhidi ya mshukiwa barabarani.

Mauaji hayo yamezua mjadala mkali wakati kesi ya mauaji ya George Floyd ikiendelea.

Afisa aliyempiga risasi Bw Wright siku ya Jumatatu ni Kim Potter, 48, ambaye amefanya kazi katika kituo cha polisi cha Brooklyn Center kwa miaka 26.

Bw, Wright aliagizwa kuegeshe gari kando ya barabara siku ya Jumapili baada ya kukiuka sheria ya trafiki, lakini mvutano ulizuka alipojaribu kurudi katika gari lake.

Baada ya kutoa bunduki yake, kimakosa, afisa huyo alisema: "Mungu wangu, Nimempiga risasi."

Waandamanaje

Chanzo cha picha, Reuters

Nini kilitokea usiku wa kwanza?

Vitoa machozi vilitumiwa na amri ya kutotoka nje kutolewa wakati wa maandamano ya hasira baada ya polisi kumpiga risasi mtu mweusi aliyesimamishwa na polisi wa trafiki katika jiji la Brooklyn Centre nchini Marekani kaskazini mwa Minneapolis.

Mwanamume huyo alitambuliwa na jamaa zake kama Daunte Wright mwenye umri wa miaka 20.

Meya wa Brooklyn Centre alitoa amri ya kutotoka nje mjini kote hadi saa 06:00 (11:00 GMT), akiwaambia watu " muwe salama, nendeni nyumbani".

Taharuki huko Minneapolis iko juu wakati kesi ya afisa wa zamani anayedaiwa kumuua George Floyd ikiendelea.

Gavana wa Minnesota Tim Walz alisema "alikuwa akifuatilia kwa karibu hali hiyo" na akiombea familia ya Bw Wright.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Nini kilimkuta Daunte Wright?

Mkuu wa polisi Tim Gannon anaamini mauaji ya Bw. Wright "yalifanyika kwa bahati mbaya".

Katika mazungumzo na wanahabari siku ya Jumatatu, alicheza kanda ya video kutoka kwa kamera iliyokuwa imevaliwa na afisa wapolisi ikimuonesha Bw. Wright akijaribu kurudi katika gari lake huku maafisa wakijaribu kumvisha pingu kando ya barabara.

Afisa baadaye anasikika akisema "Taser, Taser, Taser" - mpango wa kawaida wa unaofanywa na polisi kabla ya kupiga moja ya bunduki ya kufisha ganzi.

Bw. Wright anaonekana akiingia kwenye gari lake na kujaribu kuondoka, huku afisa huyo akikiri kwamba amempiga risasi.

Daunte Wright

Chanzo cha picha, Katie Wright

Maelezo ya picha, Mama yake Daunte Wright, Katie, anasema mwanawe alimpigia simu akimwambia amesimamishwa na polisi

Bw. Wright aliyekuwa amejeruhiwa vibaya aligongesha gari katika barabara tofauti.

"Naamini afisa alikuwa na nia ya kutumia kifaa tofauti badala ya bunduki lakini kwa bahati mbaya akampiga risasi moja," Gannon alisema, akiongeza: "Sina la kusema kupunguza machungu waliyo nayo."

Shangazi yake Daunte Wright, Naisha Wright, aliiambia CNN haamini kauli ya polisi, akisema maafisa wanajua tofauti kati ya bunduki na Taser.

Afisa huyo amepewa likizo ya muda - na atapokea mshahara wake kama kawaida.

Meya Elliot amesema afutwe kazi. Atafanya maamuzi leo Jumanne ikiwa Gannon atasalia kazini, gazeti la StarTribune limeripoti .

Map
Presentational white space

Unaweza pia kusoma: