Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 04.04.2021: Mata, Haaland, Odegaard, Icardi, Winks, De Gea, Lingard, Fekir

Manchester United playmaker Juan Mata

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juan Mata mchezaji wa Old Trafford

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Uhispania Juan Mata, 32, yuko tayari kupokea mkataba mpya wa mwaka mmoja katika klabu yake. (Daily Star Sunday)

Mkuu wa soka Sebastian Kehl amekubali Borussia Dortmund huenda ikafika kiwango ikashindwa kuendelea kumlipa mshambuliaji raia wa Norway Erling Braut Haaland, 20. (Goal)

Erling Braut Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Erling Braut Haaland amefunga magoli 39 kwa klabu ya nchi yake msimu huu

Haaland amempiku mshambuliaji wa Barcelona raia wa Argentina Lionel Messi, 33, kama mlengwa mkuu wa Manchester City licha ya kocha Pep Guardiola kusema klabu hiyo haina uhakika kama itamnunua mbadala wa Sergio Aguero, 32 ambaye anatoka nchi moja na Messi. (Sunday Mirror)

Inaaminika kuwa Haaland anataka kuhamia Real Madrid lakini klabu hiyo ya Uhispania haitatoa ofa kwa mchezaji huyo badala yake itamsubiri kwanza aondoke na ihakikishe kuwa hayupo tena Dortmund. (AS - in Spanish)

Martin Odegaard, amewasiliana na Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Martin Odegaard, amewasiliana na Arsenal

Arsenal huenda ikalazimika kufikiria kuwauza wachezaji nyota vijana kama vile winga wa England Bukayo Saka, 19, ili kupata pesa za kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid raia wa Norway Martin Odegaard, 22, kwa mkataba wa kudumu, pamoja na wachezaji wengine wapya kuleta nguvu mpya katika timu. (Sunday Times - subscription required)

Manchester United italazimika kutoa kitita kizuri tu kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa juu zaidi David de Gea huku mlinda lango huyo, 30, raia wa Uhispania akiwa tayari kuondoka Old Trafford. (Sunday Mirror)

Mauro Icardi goes for goal against Bordeaux

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mauro Icardi

Mshambuliaji wa Paris St-Germain raia wa Argentina Mauro Icardi, 28 amejitokeza kuwa mlengwa wa Manchester United kama mbadala ya kudumu wa Edinson Cavani, 34. (Teamtalk)

Everton imeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala lakini mchezaji huyo atakataa ofa yoyote atakayopewa na Toffees. (CaughtOffside)

Harry Winks

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harry Winks akisherehekea kufunga goli

Atletico Madrid inafuatilia kwa karibu kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na England Harry Winks, 25, ambaye amekuwa na wakati mgumu kupata fursa ya kucheza chini ya utawala wa Jose Mourinho. (Sky Sports)

Kocha wa West Ham David Moyes hana wasiwasi eti mkataba wa sasa wa kiungo wa kati wa England na Manchester United Jesse Lingard, 28, haujumuishi kipengee cha kumnunua. (Mail on Sunday)

Oli McBurnie became a favourite among Swansea fans after joining the club as a teenager in 2015

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency

Maelezo ya picha, Oli McBurnie

Wolves imetenga dau la pauni milioni 15 kwa Sheffield United wakati ina mnyatia mshambuliaji wa timu hiyo na Scotland Oli McBurnie, 24. (Sun on Sunday)

Aliyekuwa nahodha wa Chelsea na England John Terry, ambaye sasa ni wale walionyuma ya timu ya Aston Villa, amejitokeza kuwa miongoni mwa wanaogombea nafasi ya kocha wa Sheffield United ambayo iko wazi kwa sasa. (Sunday Mirror)

Manchester City inataka kuwa na beki wa kushoto wa FC Groningen raia wa Sweden Gabriel Gudmundsson, 21. (TodoFichajes - in Spanish)

Nabil Fekir waves after the 2018 World Cup final

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Nabil Fekir

Barcelona inafikiria uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Real Betis raia wa Ufaransa Nabil Fekir ingawa mchezaji huyo, 27 pia amehusishwa na Arsenal. (Estadio Deportivo)

Manchester United inafuatilia mbinu za kumsajili mlinzi wa Ureno, 18, Nuno Mendes kutoka Sporting Lisbon na kwa upande wake huenda ikatoa ofa kwa Mbrazil Alex Telles, 28. (Record - in Portuguese)

Adrien Rabiot

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Adrien Rabiot

Kiungo wa kati wa Juventus Adrien Rabiot, 26, ambaye amehusishwa na Everton, huenda pia akanyatiwa na Barcelona. (Calciomercato)

Mlinzi wa Eintracht Frankfurt Mholanzi Jetro Willems, 27, na winga wa Crystal Palace Andros Townsend, 29, wanaweza kurejea Newcastle msimu huu. (Chronicle)

Na, Eddie Howe anafuatilia kumleta nahodha wa Bournemouth Steve Cook, 29, ikiwa atatajwa kama kocha wa Celtic. (Sun on Sunday)