Kifo cha Rais John Pombe Magufuli: Aliyotufanyia kiongozi huyo hatutamsahau

Chanzo cha picha, Getty Images
Kifo cha Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kilipokelewa kwa mshutuko sana na watu wengi ndani na nje ya Tanzania .
Rais huyo wa zamani ambaye anazikwa leo nyumbani kwake Chato mkoani Geita alikuwa amegusa nyoyo za wengi ambao aliwafanyia mambo mbali mbali mazuri .
Hata hivyo kunao ambao pia vitendo na kauli za rais huyo pamoja na na utawala wake huenda viliwakwaza kwa njia moja au nyingine . Hawa hapa baadhi ya wanaomkumba Hayati Magufuli kwa aliyowafanyia .
Prof.Costa Ricky Mahalu: 'Hadhi nikarejeshewa .. nilisoma tu magazetini'
Balozi Costa Ricky Mahalu ni miongoni mwa watu ambao wamekwazwa sana na kifo cha hayati Magufuli kwani Rais huyo wa zamani alimpa usaidizi wakati ambapo alihisi kuonewa .
Mahalu alipokonywa hadhi yake ya ubalozi mwaka wa 2007 na hata kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa ubadhirifu wa fedha katika sakata ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania huko Italia .
Wakati huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchinI Italia . Katika kilichovunja historia mwaka wa 2012 rais mstaafu hayati Benjamin Mkapa alikuwa shahidi kortini kumtetea Mahalu jijini Dar es Salaam .
Baadaye mwaka wa 2018 Mahalu alikutana na hayati Magufuli ambaye alimjulia hali na kumuuliza kuhusu hadhi yake ya Ubalozi . Hakujua kwamba rais Magufuli alikuwa na nia ya kumrejeshea hadhi yake hiyo aliyokuwa amepokonywa . Anasema alishangazwa alipoona uamuzi huo uliofanywa na rais kupitia magazeti
'Lakini rais alijua kwamba nilikuwa nimeonewa...hatimaye siku moja mimi nikashangaa kwamba hadhi yangu ya ubalozi imerejshwa . Hakunieleza kama atairudisha..hapana nimekuja tu.. nimesoma kwenye gazeti …nikashangaa na nikamshukuru mwenyezi Mungu ..nami nikampelekea ujumbe kumuambia kwamba nimeshukuru'
Mahalu anasema Hayati Magufuli alikuwa muelewa sana na ndio maana alifahamu fikra na matatizo yaliyowasakama Watanzania wengi ambao ni maskini .
'Magufuli alijua kwamba kuna watu wenye pesa waliotaka kuwatumia wanyonge kwa kujifanya kwamba wanawajali kumbe waliwataka maskini kusalia tu hivyo katika umasikini ..' Mahalu anasema kumhusu Hayati Magufuli
Fatma Karume: 'Imekuwa ni miaka mitano ya kuogofya nchini Tanzania..'

Kando na waliomjua rais Magufuli kwa mazuri aliyowafanyia ,kuna wale ambao msumeno wake uliwakata ncha mbili .
Bi Karume ni mmoja ya watu ambao walikuwa ni wakosoaji wakuu wa utawala wa Magufuli nchini Tanzania, alitumia ukurasa wake wa Twitter kueleza fikra zake ambazo mara nyingi zilikuwa ni mwiba kwa mamlaka.
Kupitia mtandao huo pia amekuwa akieleza namna gani hayati Magufuli ama utawala wake ulikuwa kwake.
Muda mfupi baada ya kutolewa kwa tangazo la kifo cha Rais Magufuli alituma ujumbe: "Imekuwa ni miaka mitano ya kuogofya nchini Tanzania lakini nashukuru na kujivunia kuwa nilibaki na utu wangu hata pale ambapo uovu ulitamalaki. Asante nyote ambao mlifanya miaka mitano hii kuvumilika."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Na baada ya kukosolewa kwa kuendelea kumkosoa Magufuli hata baada ya kufariki akatuma ujumbe huu: "Alivyokuwa hai, niliambiwa: "Usimseme! Atakudhuru! Ana visasi! Ana power na anaitumia vibaya" Alivyofariki niliambiwa: "Usimseme! Dini, mila na desturi haziruhusu mabaya ya maiti kusemwa" Swali: Kuna watu wako untouchable? Hatuna rukhsa kusema mabaya yao wakiwa hai na wakifariki?"
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Pia ameeleza kuwa hajafurahia kifo cha Magufuli kama baadhi ya watu walivyodhania: "…Kuna wale ambao wanaweza kuamini kuwa nilisherehekea niliposikia (taarifa ya ) kifo cha Magufuli lakini ukweli ni kwamba nilihisi "faraja" na "shukrani" kwa uwezekano wa mwanzo mpya."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Anna Erasto: 'Alikuja kula hapa'
Anna Erasto- Mhudumu wa mgahawa wa Victoria uliopo nje ya uwanja ndege jijini Mwanza ni mtu mwingine ambaye kifo cha hayati Magufuli kimemuacha na makovu .
Akizungumza na BBC alisimulia jinsi alivyoshtushwa kumuona hayati Rais Magufuli mgahawani mwao mwaka wa 2016 alipokuwa safarini kuelekea Chato kwa mapumziko.
Anna anasema kuja kwa Magufuli katika mgahawa wao ni jambo ambalo lilibadilisha biashara yao kwani watu wengi baadaye walitaka kuja kula hapo wakitaka kujua alichoagiza rais. Amesema kifo cha hayati Magufuli kimewasononesha wengi .
Rais Magufuli ametambulika kama mtetezi mkubwa wa wafanyibiashara wadogo wadogo na kuna mifano mingi akitangamana nao na hata kuwasaidia kadhaa nchini Tanzania .
Kasara Mnaku: 'Tulisoma na hayati Magufuli'
Mwalimu mstaafu Mnaku alisoma darasa moja na hata kuketi kiti kimoja na hayati Magufuli .
Anasema alikuwa akitafutwa na rais ili kumpa ushauri . Mnaku amesimulia jinsi yeye na rais Magufuli walivyozingatia sana masomo na hawakupenda mchezo. Zawadi kubwa ambayo anasema Magufuli aliwaachia watu wa Chato ni kulipandisha hadhi eneo hilo hadi likawa la kutambulika
'.....Chato ilikuwa ni kijiji .Lakini ameiandaa hadi ikawa Wilaya hadi mpaka sasa hali iliyopo hii'
Tulikuwa sote Walimu
Mwalimu Mnaku anasema amemfahamu hayati Magufuli tangu utotoni na hata wote walijipata wakiwa walimu .
Amesimulia jinsi safari yao ilivyobadilika wakati Magufuli alipoamua kujitosa katika siasa naye akaendelea kuwa Mwalimu lakini hilo halikuwazuia kukutana mara kwa mara kusalimiana na hata kuzungumzia mambo ya maisha ya kila mmoja wao.
'Ilikuwa ni vigumu mimi kumtafuta kwa hivyo ni yeye aliyekuwa akinitafuta na tulikuwa tukikutana na kuongea mawili matatu'














