Bunge la Rwanda lalaani kauli ya Muungano wa Ulaya 'iliyojaa uongo' kumuhusu mpinzani Paul Rusesabagina

Bunge la Rwanda limesema kuwa linalaa hatua ya Muungano wa Ulaya (EU )ya kusema kuwa Paul Rusesabagina alitekwa nyara na kusema kuwa "imejaa uongo na kufumbia macho kwa makusudi ukweli halisi ".
Katika kikao chake cha jana jioni kilichokaa kwa njia ya mtandao, wabunge walisema pia kwamba yaliyosemwa na wabunge wa EU ni "kuingilia uhuru wa mfumo wa mahakama za Rwanda na mfumo mzima wa utawala wa Rwanda, pamoja na upotoshaji wa ukweli juu ya mauji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watusi ya mwaka 1994''.
Aidha bunge la Seneti la Rwanda pia limelaani taarifa ya EU kuhusu Bw Paul Rusesabagina, na limeazimia kuitathmini na kufikisha " tatizo hilo mbele ya bunge la Ulaya ".
Siku ya Alhamisi , Bunge la Ulaya lilitoa taarifa iliyokuwa na waraka uliosema kuwa wabunge wa bunge hilo wanalaani "utekaji nyara aliofanyiwa Paul Rusesabagina " nchini Rwanda jambo ambalo walisema halikufuata sheria.
Bunge la Rwanda pia limezitaka kamati za mabunge yote mawili zinazohusika na masula ya uhusiano wa kimataifa, kutathmini taarifa hiyo ya EU.
Mabunge yataandaa muswada wa maazimio utaowasilishwa katika vikao vikuu vya mabunge hayo.
Bunge la EU liliidhinisha nini?
Bunge la Muungano wa Ulaya liliidhinisha maazimio matatu kuhusiana na hali ya haki za binadamu katika mataifa ya Rwanda Kazakhstan, Rwanda na Uganda.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika maazimio yao kuhusu Rwanda Rwanda, wabunge walilaani "utekwaji, na kusafirishwa kwa nguvu ambako hakukufuata sheria kwa " Paul Rusesabagina, aliyetoweka tarehe 27/08/2020 alipokuwa Dubai, na baadaye kuoneshwa kwa umma mjini Kigali tarehe 31 ambapo mamlaka zilithibitishwa kuwa zinamshikilia.
Unaweza pia kusoma
Bunge la Ulaya linasema "kutekwa kwa Rusesabagina ni kinyume na yale Rwanda iliyoyaafiki " katika makubaliano ya kimataifa ya kulinda haki za binadamu mu masezerano mpuzamahanga anyuranye yo kubahiriza uburenganzira bwa muntu.
Wabunge wa EU wameitaka Rwanda kueleza wazi ''jinsi Paul Rusesabagina alivyokamatwa na kupelekwa Kigali''.
Wametoa wito "uchunguzi huru wa kimataifa kuchunguza jinsi Rusesabagina alivyokamatwa na kupelekwa Kigali".
Kwanini Rusesabagina anashikiliwa?
Paul Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka mbali mbali ikiwa ni pamoja na ugaidi, na mauaji anayodaiwa kuyatekeleza katika ardhi ya Rwanda.
Ni ni kiongozi wa muungano wa kisasa MRCD-Ubumwe ambao Rwanda inauhusisha na mashambulio ya ugaidi yaliyowauwa Wanyarwanda katika kituo cha polisi cha mjini Kigali.
Rusesabagina alipata umaarufu baada ya kucheza filamu ya Hollywood kwa jina Hotel Rwanda iliyotolewa mnamo mwaka 2004.
Katika filamu hiyo , Paul Rusesabagina aliangaziwa kama mtu aliyetumia ushawishi wake - na rushwa- kuwashawishi maafisa wa kijeshi kuwapa njia salama ya kuwatorosha karibu watu1,200 ambao walitafuta maficho katika Hôtel des Mille Collines, ambayo alikuwa meneja wake wakati wa mauji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.
Baada ya filamu hiyo kutolewa Bw. Rusesabagina alitunukiwa medali ya Rais wa Marekani ya Uhuru 2005,George Bush.
Hata hivyo kundi la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Ibuka lilisema kuwa alitilia chumvi jukumu lake la kuwasaidia wakimbizi kujificha hotelini katika siku 100-za mauaji ya kikatili mwaka 1994.
Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 2011, Bwana Rusesabagina alishutumiwa kudhamini kundi na muungano wa makundi ya ugaidi yenye silaha na itikadi kali.
Rusesabagina ni Naibu kiongozi wa muungano wa vyama vya kisasa vinavyoipinga serikari ya Kigali wenye makundi ya kijeshi -FLN -unaoendesha harakati zake mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Mwaka 2018, kundi la FLN lilidai kufanya mashambulizi kwenye ardhi ya Rwanda kwenye maeneo ya msitu wa Nyungwe ambapo watu wengi waliuawa.












