Somalia: 'Bado tunawahitaji Wamarekani kwenye masuala ya usalama'

Chanzo cha picha, AFP
Mvutano unazidi kuongezeka nchini Somalia, wakati mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo unapambana na mchakato wa uchaguzi uliopingwa vikali, kuondolewa kwa vikosi muhimu vya jeshi la Marekani, na kuongeza wasiwasi juu ya operesheni za wanamgambo wa Kiislamu wanaozidi kuwa na rasilimali nyingi.
Wanadiplomasia na waangalizi wanaonya kuwa nchi hiyo - miongo mitatu baada ya kuanguka katika machafuko - ipo tena kwenye njia panda, na hatua ya hivi karibuni ya kurekebisha tena hali mbaya sasa iko hatarini.
"Somalia iko katika wakati mgumu sana," mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa James Swann aliambia BBC, akionya kwamba "msimamo mkali" wa viongozi wa kitaifa wa nchi hiyo - wanapobishana kuhusu mchakato wa uchaguzi unaweza kusababisha vurugu.
Kundi la mashirika na nchi zenye nguvu - ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa , Umoja wa Ulaya na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika - umetoa taarifa kuwataka wasomi wa kisiasa wa Somalia kutafuta mazungumzo. "Tishio lolote la matumizi ya vurugu halikubaliki," waliandika.

Chanzo cha picha, Reuters
Somalia ilitarajiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza mwaka jana - hatua kubwa kwa taifa lililovunjika kwa muda mrefu.
Lakini vyama vya upinzani vinavyoongozwa na ukoo vinasusia mchakato huo wakiwa na wasiwasi kuhusu wizi wa kura, makubaliano yaliyosimamiwa kwa uangalifu sasa yameharibika, na Rais wa nchi hiyo, Mohamed Abdullahi "Farmaajo", analaumiwa na wengine kwa kutaka kuweka matakwa yake kwa Somalia.
"Inaweza kuwa janga ikiwa haitarudishwa kwenye njia sahihi na uchaguzi huu wa sasa. Kila mtu anajua demokrasia yetu iko hatarini, na tunahitaji kuirekebisha," alisema mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa wa Bw Farmaajo, Hussein Sheikh Ali .

Chanzo cha picha, Reuters
Wanamgambo wa Kiisilamu waliondolewa kutoka mji wa Mogadishu, na waliondolewa nje ya miji mingine mingi ya Somalia, na Umoja wa Afrika na wanajeshi wa Somalia, lakini Wanaendelea kushikilia sana maeneo ya vijijini.
Wameanza pia kufanya kazi ambayo ni serikali ya kivuli ndani ya Mogadishu, ambapo inatoza ushuru na kutisha wafanyabiashara wengi, inasimamia korti za Sharia, hufanya mauaji ya kulenga, na kupanga mashambulizi ya kujitoa muhanga kwenye hoteli na ofisi za serikali.
"Kila mtu hutozwa ushuru na al-Shabab, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, pamoja na rais - chakula anachokula kinatozwa ushuru [na wao]," mshauri wa zamani wa Bw Farmaajo aliiambia BBC.
"Wamekuwa na wakipata nguvu zaidi ya miaka minne iliyopita. Watu wengi hudharau al-Shabab na wanasema wanakuwa kama mafia. Lakini wao ni shirika lililopangwa vizuri na linaloshabihiana na maono ya kimkakati ya kushinda nchi hii. "

Watu kumi na watano waliuawa mwaka jana mwezi Agosti baada ya al-Shabab kushambulia hoteli moja ya ufukweni, mjini Mogadishu. Mmilika alisema anafiri hoteli ililengwa kwa kuwa alikataa kuwapa fedha wanamgambo.
''Ni kama kikombozi. Walikuwa wakifahamu kuwa hatutafanya malipo yoyote kwa al-Shabab,'' alisema Abdullahi Nor, ambaye kwa haraka alifanyia marekebisho jengo na likaendelea kuwa wazi kwa ajili ya kuendelea na biashara.
Hata baada ya kile kilichotokea, tuko tayari kukataa na kujitetea,'' alisema.
Lakini Bwana Nor, kama wateja wake wengi na familia nyingine zinazofurahia pwani ya Lido alasiri moja, alionesha wasiwasi mkubwa kuhusu maendeleo mapya - kuondolewa kwa wanajeshi wengine wa Marekani kutoka Somalia, kwa agizo la Rais Donald Trump
''Inatusikitisha sana,'' alisema mmiliki wa hoteli. '' Bado tunawahitaji Wamarekani, hasa kwa ajili ya usalama.''

Chanzo cha picha, Reuters
Kuna wasiwasi hasa kwamba - ingawa mashambulio ya ndege zisizo na rubani dhidi ya al-Shabab yataendelea - mafunzo na usimamizi ambao Wamarekani walitoa kwa vikosi maalum vya Somalia yanaweza kuwa mashakani.
"Ni mashambulio tu ya anga ya Marekani na vikosi maalum ambavyo vimekuwa vikipiga al-Shabab kwa nguvu na kuvipunguza kasi," ilielezwa
Mvutano huo ndani ya taasisi dhaifu za serikali ya Somalia pia unachochewa na kutokuwepo na hali ya utulivu nchini Ethiopia, Ghuba na kwingineko, na majeshi matano ya kigeni ya Afrika na washauri wa jeshi kutoka mataifa mengine mengi, ambayo sasa yanafanyia kazi migogoro ya ndani ya Somalia.
Maendeleo makubwa Somalia
"Shida ni kwamba mizozo ya Somalia haijasuluhishwa kabisa bado. Kuna maoni tofauti kuhusu ni nchi gani inapaswa kuwa. Tofauti ndani ya Somalia inatumiwa au kupanuliwa, wakati mwingine na washirika wa kimataifa," alisema balozi wa Uingereza Ben Folder.
Somalia bila shaka imepiga hatua kubwa katika maeneo mengi katika kipindi cha miaka michache iliyopita.
Nchi hiyo imekuwa na ufanisi zaidi katika ukusanyaji wa mapato, Wasomali vijana na wanachama raia waishio nje ya Somalia wanafanya kazi katika asasi za kiraia, Mogadishu yenyewe inabadilika haraka, na ikiwa wanasiasa wanaweza kushinda mkwamo wa sasa na kufanya uchaguzi mwingine mwaka huu, ingemaanisha kuwa nchi imeweza kusimamia mabadiliko ya tatu ya uongozi kwa amani katika kipindi cha chini ya miaka kumi.
Lakini hatua hii kubwa imebaki kuwa tegemezi kwa vikosi vya AU, Amisom, waliokuwa na wanajeshi 20,000, wanaolinda serikali na kwa miaka vimekuwa vikiongoza vita dhidi ya al-Shabab.

''Hatujatekeleza kazi yetu . ni ukweli'' alisema bwana Ali katika kulijenga jeshi la Somalia. ''Lakini Amisom pia haijatekeleza jukumu lao vya kutosha.''
Muongo mmoja uliopita, wakati al-Shabab walipokuwa wakidhibiti zaidi ya nusu ya mji wa Mogadishu, ilikuwa ikiaminika kuwa wanamgambo watauangamiza mji ndani ya saa moja kama Amisom itaondoa vikosi vyake.
Leo, kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa jeshi ambaye hakutaka jina lake litajwe, sasa itachukua "saa 12 tu" kwa al-Shabab kuudhibiti mji wa Mogadishu na miji mingine mingi ikiwa vikosi vya Amisom vitaondoka.













