Virusi vya corona: Uvumbuzi kumi wa Kiafrika unaosaidia kupambana na Covid-19

Doctor robot on the hospital ward

Chanzo cha picha, Ecole Supérieure Polytechnique Dakar

Maelezo ya picha, Roboti ya gari la Daktari
Muda wa kusoma: Dakika 4

Huku idadi ya watu zaidi ya milioni wakithibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya coprona Afrika, wavumbuzi barani Afrika wamejitokeza kukabiliana na janga kwa aina mbalimbali za ugunduzi. Huu hapa ni uvumbuzi 10 tulioweza kukukusanyia.

1. Roboti ya 'Doctor Car'

Mwanafunzi kutoka shule ya Dakar Polytechnic School nchini Senegal alijenga roboti inayoweza kufanya mambo mbalimbaliiliyotengenezwa kwa ajili ya kupunguza hatari ya maambukizi ya wahudumu kutoka kwa wagonjwa wa Covid-19.

Chombo hicho kina kamera na kinaweza kuongozwa kufanya kazi kwa mbali kwa kutumia app. Walioitengeneza wanasema inaweza kuzunguka katika vyumba vya wagonjwa waliowekwa karantini kuchukua vipimo vyao vya joto la mwili na kuwapelekea chakula na dawa.

2. Mashine ya kunawa mikono Kiosha mikono

Stephen Wamukota

Chanzo cha picha, James Wamukota

Maelezo ya picha, Stephen alipata tuzo ya rais kwa uvumbuzi wake

Mvulana mwenye umri wa miaka tisa mwanafunzi nchini Kenya Stephen Wamukota alivumbua mashine ya mbao ya kunawa mikono ili kusaidia kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Mashine inawawezesha watumiaji kuchota maji kwenye ndoo ya maji kunawa mikono yao kwa kutumia ubao unaokanyagwa kwa mguu. Hii inawasaidia watumiaji kuepuka kugusa mahali popote na mikono yao na kupunguza hatari ya maambukizi.

Stephen alipewa tuzo na rais mwezi Juni.

3. The Respire-19 portable ventilator ( kifaa kinachosaidia kupumua)

Huku kukiwa na upungufu wa mashine zinazosaidia wagonjwa kupumua katika wodi za wagonjwa wa Covid-19 wards in nchini Nigeria, mwanafunzi wa uhandisi mwenye umri wa miaka 20 nchini Nigeria Usman Dalhatu alijaribu kusaidia kupunguza upungufu huo.

Usman Dalhatu carri ventilator wey im build

Chanzo cha picha, Instagram / Usman Dalhatu

Maelezo ya picha, Usman Dalhatu anasema anasubiri kuidhinishwa kwa matumizi ya mashine yake ya kusaidia kupumua (Ventilator)

Dalhatu alitengeneza ventilator inayotumiwa moja kwa moja ili kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupumua ambayo mara nyingi husababishwa na maambukizi ya virusi vya corona. Sasa anapanga kutengeneza mashine hizo 20.

4. Chapisho la 3D

Natalie Raphil ni muasisi wa kampuni ya Intelijensia gudhi ya -Robots Can Think South Africa.

Anatumia mfumo wa 3D wa matbaa kutengeneza barakoa 100 kwa siku katika baadhi ya hospitali kuu za Johannesburg. Afrika Kusini ina nusu ya idadi ya watu wote wenye virusi vya corona waliohesabiwa barani Afrika.

5. Solar-powered hand-washing sink (Siki ya kunawa mikono inayotumia miale ya jua)

Wakati ilipowekwa tahadhari ya kutotoka nje nchini Ghana iliyolenga kukabiliana na Covid-19, mtengenezaji viatu Richard Kwarteng na kaka yake Jude Osei waliamua kutengeneza beseni ya kunawa mikono inayotumia miale ya jua.

Wakati mikono inapokaribia kifaacha utambuzi kwenye beseni, maji ya sabuni hutoka moja kwa moja . King'ora hulia kwa sekunde 25 baadae za kunawa mikono- kipindi ambacho kinashauriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kunawa mikono.

1px transparent line

6. Mashine ya X-ray iliyotengenezwa kwa mtandao yakupima mapafu

Wahandisi nchini Tunisia wamebuni jukwa la mtandao ambalo linafanya uchunguzi wa skani (scan) kwa kutumia X-ray kujaribu kubaini iwapo mtu anaweza kuwa anaumwa virusi vya corona.

lung x ray on screen with covid circled in red

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati X-ray inapopakuliwa kwenye jukwa hilo, hufanya vipimo kubaini dalili zinazoweza kuwa ni za maambukizi ya virusi vya corona. Watafiti katika Taasisi ya sayansi na teknolojia nchini Tunisia wanasema kuwa kifaa hicho hubaini asilimia 90 ya dalili zinazoweza kuwa za maabukizi ya corona.

Jukwaa hilo bado linatengenezwa, lakini vipimo maelfu kadhaa vya X-ray vya mapafu vimekua vikiingizwa ndani ya mfumo ili kuuwezesha kutambua athari za Covid-19 kwa mapafu.

7. Roboti za polisi katika doria ya 'lockdown'

Maafisa nchini Tunisi walituma roboti polisi kwenye mitaa ya mji mkuu mwezi Aprili ili kuhakikisha watu wanazingatia hatua zilizotangazwa za amri ya kutotoka nje.

A police robot questions someone in Tunis, Tunisia - 1 April 2020

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Roboti ya polisi ikiongea na mtu mjini Tunis, Tunisia

Uchunguzi wa roboti , zinazofahamika kama PGuards, uliwafuatilia watu waliokuwa wakitembea katika mtaa na kuwasogelea na kuwauliza ni kwanini walikuwa nje wakati wa amri ya kutotoka nje.

Waliopatikana na kosa hilo walilazimika kuonyesha vitambulisho vyao na nyaraka nyingine kwenye kamera iliyopo kwenye roboti hizo. Roboi hizo zenye magurudumu manne zina kamera na mwanga wa utambuzi na imeunganishwa na teknolojia nyingine kadhaa za mawasiliano.

Coronavirus
coronavirus

8. Sanitizer iliyotengenezwa kwa ubao

Wakala wa usambazaji wa pesa kwa njia ya simu ya mkononi nchini Kenya-Danson Wanjohi alitengeneza chombo cha mbao ambacho kinaweza kusafisha au kutakasa pesa za noti ambazo zinapitishwa katika .

Wanjohi alitengeneza kifaa kinachotumia injini , nati za kufunga pesa na pedeli ambayo inawezesha noti kupita kwenye mashine.

Wakati noti zinapopita kwenye kifaa ,zinasafishwa na kimiminikacha kutakasa( sanitizer)

9. Rapid 65-minute Covid-19 testing kit (kipimo kinachopima Covid-19 kwa dakika 65)

Wajasiliamali wa Afrika Ksuini Daniel Ndima na Dineo Liomaamebuni kifaa cha kupima Covid-19 ambacho hutoa matokeo baada ya dakika 65

Kwa kawaida inaweza kuchukua hadi siku tatu kwa kipimo cha Covid-19 kutoa matokeo.

Kifaa hicho cha kupima kinafahamika kama qPCR, na kina teknolojia inayotumika kupima vinasama-DNA. Kipimo hiki kinahitaji kuidhinishwa na taasisi za udhibiti wa viwango kabla ya kuanza kutumiwa.

10. ( Ukataji wa nywele wa kutokaribiana)

Man getting a haircut with hairdresser behind a wooden shield

Nchini Ethiopia vinyozi wa nywele wamebuni njia ya kukata nywele za wateja waohuku wakipunguza hatari za maambukizi ya Covid-19.

Kinyozi husimama kwenye kijumba kidogo kilichotengenezwa mfano wa kioski ambacho humsaidia kuwa mbali na mteja anayemnyoa na hivyo kupunguza uwezekano wa kumsogelea mteja wake.