Virusi vya corona: Mgonjwa wa Covid-19 hupona vipi baada ya kuwa ICU ?

Chanzo cha picha, Reuters
Watu wengi zaidi kuliko kawaida wako katika matibabu ya uangalizi mkubwa kwenye hospitali mbalimbali duniani kwa sababu ya Covid-19.
Katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ICU, kazi ya kuokoa uhai inaendekea kwa msaada wa mashine zinazowasaidia wagonjwa kupumua na kuwezesha viungo vyao muhimu kufanya kazi za msingi, pia kusukuma dawa kwenda kwenye mwili.
Wakati sasa kukiwa bado hakuna tiba iliyothibitishwa ya virusi vya corona, suala muhimu kwa wagonjwa walio katika hali mahututi ni kupata hewa safi ya kutosha (oksijeni) kwenye mapafu yao wakati mfumo wao wa kinga ukipambana na virusi.
Lakini kwa kawaida huu ni mwanzo tu wa kuelekea kupona, kwa mujibu wa wataalamu.
Safari ya mgonjwa ambaye amefanikiwa kuonesha matokeo chanya kwa tiba ya chumba mahututi na ikawezekana kutoka hospitali ni safari ngumu wakati mwingine huchukua miaka kadhaa kisaikolojia ni suala linaloathiri.
Kujifunza kupumua
Baada ya kukaa kwa muda mrefu ICU, ni kawaida kwa wagonjwa kupata tiba ya mazoezi ya viungo ili waweze kujifunza jinsi ya kutembea au hata kupumua tena.
Wanaweza kuwa wamepata tatizo la kisaikolojia na matatizo ya msongo wa mawazo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na kadiri muda wanaoutumia kuwa kwenye matibabu unavyokuwa mrefu, ndivyo inavyochukua muda zaidi kwa wagonjwa kuanza kujisikia vizuri tena.
''Ikiwa utakuwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, ni mchakato wa kubadili maisha. Hubeba gharama kubwa hata kama utapata nafuu,'' anasema dokta David Hepburn, mshauri wa masuala ya tiba kwa wagonjwa mahututi katika hospitali ya Royal Gwent nchini Uingereza.
''Wakati wagonjwe wetu wanapoamka, huwa dhaifu hawawezi kukaa wima bila kusaidiwa. Wengi hawawezi kunyanyua mikono kwa sababu mwili ni dhaifu.''
Kama tiba itawataka kuwekewa mipira na kulishwa kwa mipira, wanaweza kupata matatizo ya kuzungumza na kumeza.
''Hupata nafuu baada ya kipindi fulani, lakini inaweza kuchukua mwaka mmoja kama watahitaji tiba ya mazoezi ya viungo, kuzungmza, lugha na saikolojia''.

Chanzo cha picha, Getty Images
Muda uliotumika ICU unaweza tu kuwa sehemu ndogo tu ya tiba ya matatizo yote ya kiafya ambayo yatapaswa kutazamwa baada ya kutoka kwenye uangalizi maalumu, wanasema wataalamu.
Matatizo ya kisaikolojia huathiri robo ya wagonjwa wanaokuwa ICU
Mwandishi nchini Uingereza David Aaronovitch amezungumza na BBC kuhusu aliyoyapitia alipokuwa akipatiwa matibabu ya kifua mwaka 2011.
''Nilikuwa na hasira, nilikuwa ninafikiri vitu ambavyo havip- nilikuwa kama mtu ninayesikia mazungumzo ya watu ambayo kiuhalisia si kweli kuwa nilikuwa nikisikia watu wakizungumza''. alisema
''Nilihisi kama vitu vinanitokea lakini haikua hivyo. Niliamini kuwa tiba ilinifanya niwe kama majitu. Ambayo nikaanza kufikiria kuwa yameamua kunitafuta.''
Aaronovitch anasema, kwa siku tatu mpaka nne zilikuwa za kutisha sana maishani mwangu.''

Alibaini kuwa idadi kubwa ya watu hupitia hayohayo wanapokuwa wamepitia tiba kwenye vyumba vya uangalizi wa karibu.
Watafiti wana maelezo mengi kuhusu hali hii, ikiwemo ugonjwa wenyewe, upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye ubongo na dawa zinazotumika kwa ajili ya kumpoza mgonjwa.
Lakini Aaronovitch anasema hali hii ya kiakili haizungumziwi sana, kwa sababu wagonjwa huogopa kuonekana kuwa watu waliorukwa na akili.
Pamoja na kuwepo kwa wauguzi waliofuzu vyema na wenye uzoefu, ICU ni maeneo yanayoogopesha.
''Kama utafikiria kuhusu vitu vinavyotesa, utavipitia vingi kwenye vyumba vya ICU ,'' anasema Hugh Montgomery, profesa wa tiba za wagonjwa mahututi Chuo cha tiba jijini London.
Akizungumza na gazeti la the Guardian, ameeleza wagonjwa wanayoyapitia kama vile mara zote kusikia kengele kamaza tahadhari mara kwa mara, usingizi wao kukatishwa na utaratibu wa kumeza dawa hata nyakati za usiku.
Wakati mwingine huhisi kuchanganyikiwa, kuwa na uoga na kutishwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Si jambo la kushangaza,kurejea nyumbani baada ya kukaa kwenye ICU, wagonjwa hata familia wanaweza kuwa na tatizo la kisaikolojia.
wanaweza kupata tabu nyakati za kulala, au wakakosa usingizi kabisa.
Muda mrefu wa kupona
Kwa wagonjwa wa Covid 19, kuwekwa kwenye mashine za kusaidia kupumua inamaanisha kuwa watahitaji muda mrefu zaidi kwa hali zao kutengamaa.
Mshine hizi husaidi watu kusafirisha hewa ya oksijeni kwenye mapafu na kuondoa hewa ya ukaa- wakati mfumo huo hauwezi kufanya kazi bila usaidizi.
Ili kuwezesha hilo,mgonjwa atawekewa mpira kupitia mdomoni au puani, wakati wengine wanahitaji upasuaji kabisa ili kuweka mrija moja kwa moja kwenye mapafu, hali ambayo humchukua mgonjwa muda mrefu zaidi kurejea kuwa na afya njema.
Utafiti kwa nchi ya Uingereza, Wales na Ireland Kaskazini, wagonjwa hutumia siku nne mpaka tano ICU kwa mujibu wa ripoti ya tarehe 4 mwezi Aprili.
Kati ya wagonjwa 2,249 ambao data zao zilipatikana, asilimia 15 pekee waliokuwa kwenye ICU waliruhusiwa kutoka.














