Virusi vya corona: Dunia ilivyokosa fursa ya kupata chanjo ya ugonjwa wa Covid-19

Daktari Maria Elena Bottazi na mwenzake Peter Hotez katika maabara ya Chuo cha utabibu cha Baylor mjini Houston

Chanzo cha picha, ANNA GROVE

Maelezo ya picha, Daktari Maria Elena Bottazi na mwenzake Peter Hotez katika maabara ya Chuo cha utabibu cha Baylor mjini Houston

Mwaka 2002, mji wa China wa Guangzhou, kirusi kisichojulikana kilisababisha mlipuko wa ugonjwa mbaya ambao wanasayansi waliupatia jina la SARS linalomaanisha ugonjwa wa matatizo ya kupumua.

Ugonjwa huo unaosababisha viini baadae ulibainika kama virusi vya corona ambao chimbuko lake ni wanyama na ulikuwa umesambaa hadi kwa wanadamu.

Ndani ya miezi mitatu, virusi vya corona vilikuwa vimesambaa katikaa nchi 29 na kuambukiza zaidi ya watu 8,000 huku wengine 800 wakiaga dunia.

Coronavirus

Kote duniani kulikuwa na hamu ya kutaka kujua chanjo itakuwa tayari lini ili kumaliza virusi hivyo hatari na wanasayansi kadhaa Asia, Marekani na Ulaya walikuwa wameanza kushirikiana kupata chanjo.

Watu kadhaa walijitokeza huku wengine wakiwa tayari kufanyiwa majaribio.

Lakini wakati huo mlipuko wa virusi vya SARS ulikuwa tayari umedhibitiwa na utafiti wa virusi vya corona ukatupiliwa mbali.

Baada ya mlipuko wa virusi vya corona 2002 wanasayansi wengi waliahirisha tafiti zao kutokana na uosefu wa hamu na ufadhili wa kuendelea na utafiti huo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya mlipuko wa virusi vya corona 2002 wanasayansi wengi waliahirisha tafiti zao kutokana na uosefu wa hamu na ufadhili wa kuendelea na utafiti huo

Miaka kadhaa baadaye, 2012, kukatokea tena mlipuko mwengine wa, MERS-Cov, ukatokea tena na kusababisha matatizo makubwa ya kupumua. Ugonjwa wa MERS (Middle East Respiratory Syndrome) ulisambaa hadi kwa binadamu.

Na wanasayansi wengi wakarejelelea haja ya kutafuta chanjo ya viini hivi.

Leo hii, miaka 20 baadaye, wakati ambapo kirusi kipya, SARS-Cov-2, kimeambukiza watu karibia milioni 2, dunia imeduwaa tena na kutafakari lin chanjo itakuwa tayari.

Kwanini ilikuwa vigumu kujifunza kutoka kwa ugonjwa wa virusi vingine vilivyotangulia iwapo inajulikana kwamba vinaweza kusababisha kifo kama vile Covid-19? Na kwanini juhudi za kutafuta chanjo hazikuendelea?

"Hatuna haja"

Timu ya wanasayansi huko Houston, Texas, Marekani, iliendelea kufanya utafiti na mwaka 2016, ikapata chanjo dhidi ya virusi vya corona.

"Tulikuwa tumemaliza kufanya majaribio na tukaenda mbele zaidi katika hatua ya kutaka kuanzisha majaribio," Dr. María Elena Bottazzi, mkurugenzi mwenza wa Chuo cha Tiba na Utafiti wa Magonjwa ya Kitropiki cha Baylor ameambia BBC Mundo kutoka Houston na mkurugenzi mwenza wa Kituo cha Utafiti wa Chanjo cha hospitali ya Watoto Texas, Marekani.

"Tulienda katika Taasisi ya Taifa ya Afya Marekani na kuwauliza, 'Je tufanye nini ili kuhakikisha chanjo hii inafika katika kliniki haraka iwezekanvyo? Na wakatuambia: 'Kwasasa hivi, hatuna haja nayo.' "

Chanjo hiyo ilikuwa ni ya kukabiliana na virusi vya corona vilivyosababisha mlipuko wa ugonjwa wa SARS, 2002, lakini kwasababu mlipuko huo ambao ulianzia China tayari ulikuwa umedhibitiwa, watafiti hawakuweza kupata pesa za kuendeleza utafiti wao.

Virusi vya SARS na MERS vilitoa onyo kulingana na wataalam

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Virusi vya SARS na MERS vilitoa onyo kulingana na wataalam

Sio tu kwamba chanjo hiyo iliahirishwa. Makumi ya wanasayansi kote duniani walisimamisha utafiti wao kwasababu ya kukosa shauku na pesa za kuendelea na utafiti huo.

Profesa Susan Weiss wa elimu ya viini katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania, ameiambia BBC mlipuko huo ulipodhibitiwa na kuisha baada ya miezi 7 na 8 hivi, watu, serikali na kampuni za kutengeneza dawa, ghafla wote walipoteza shauku ya kufanya utafiti wa virusi hivyo vinavyosababisha corona. "

"Aidha, ugonjwa wa SARS uliathri pakubwa Asia, huku visa vichache tu vikiathiri mji wa Toronto (Canada) lakini havikufika Ulaya kama ilivyo kwa virusi vipya vya corona."

"Kwa upande mwengine ugonjwa wa MERS, ugonjwa wa pili wa virusi vya corona kwa binadamu, ulijitokeza na huo nao ukasambaa katika nchi za Mashariki ya Kati."

"Kisha shauku ya kutaka kujua kuhusu virusi vya corona ikatoweka. Hadi hili lilipotokea, kwa mtazamo wangu, naona dunia ingekuwa imejitayarisha kitambo, "amesema mtafiti.

Tahadhari mara mbili

Ugonjwa wa SARS na MERS, mtaalamu anasema, ulikuwa ni onyo tosha kuhusu hatari ya kutokea kwa virusi vya corona na juhudi za kuchunguza zaidi zikaendelea.

Ingawa chanjo ya daktari Bottazzi ilikuwa ya ugonjwa mwengine wa corona tofauti na unaosambaa kwa sasa, wataalamu wanakubaliana kwamba iwapo chanjo hiyo ingekuwa tayari, hatua zaidi zingekuwa zimepigwa kwa haraka katika kutengeneza chanjo nyengine kwa milipuko ya siku za usoni.

Jason Schwartz, profesa wa Chuo Kikuu cha Afya chaYale, anasema kwamba kujitayarisha kwa ajili ya mlipuko huu wa sasa kulitakiwa kuwe kumefanyika tangu kulipotokea mlipuko wa SARS, 2002.

"Ikiwa tutaendelea na juhudi za kutafuta chanjo ya virusi vya SARS, tungekuwa tuna tafiti za kuzifuatilia tena zenye uhusiano na mlipuko huu mpya," ameliambia gazeti la The Atlantic.

Ukweli ni kwamba virusi viypa vya corona vya sasa vinavyosababisha ugonjwa wa Sars-Cov-2, uko karibu na ugonjwa wa virusi vya corona uliosababisha ugonjwa wa Sars, 2002.

wanachama wa maabara ya shule ya kitaifa kuhusu dawa za kitropiki iliopo mjini Houston

Chanzo cha picha, ANNA GROVE

Maelezo ya picha, wanachama wa maabara ya shule ya kitaifa kuhusu dawa za kitropiki iliopo mjini Houston

Kwa asilimia 80 magonjwa hayo ya virusi yanafanana, amesema daktari Bottazzi, na tangu kwa vile tayari chanjo yake ilikuwa imepita michakati mingi muhimu na kupitishwa, ungekuwa na msaada mkubwa kwa upatikanaji wa tiba kwenye ugonjwa wa virusi vipya vya corona.

"Tayari tungekuwa tuna tajriba ya kufahamu uwezekano wa matatizo yanayoweza kuibuka kwa chanjo tunayotafuta na kujua namna ya kukabiliana na changamoto hizo. "

"Tayari tungekuwa tunajua usalama wake kwa binadamu uko vipi, aliongeza, na kuwa na uhakika zaidi kwamba chanjo hizo zinaweza kutumika na idadi ya watu wanaozihitaji."

Chanjo mpya

Kwasasa ukweli ni kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19 inahitajika.

Na pengine chanjo hiyo mpya itachukua miezi kadhaa pengine kati ya 12 na 18 kuwa tayari.

Chanjo hiyo haitakuwa karibu kupatikana kwa miezi kadhaa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chanjo hiyo haitakuwa karibu kupatikana kwa miezi kadhaa

Pengine hadi kufia wakati huo, janga hilo huenda likawa limedhibitiwa.

Daktari Bottazzi na timu yake wanashirikiana na kuhakikisha tiba inapatikana kwa ugonjwa wa virusi vya Sars ulitokea 2016 huu wa virusi vipya vya covid-19.

Na pia wanaendelea kutafuta pesa za kufadhili utafiti wao.

"Wafadhili wametoa pesa kuendeleza utafiti wa kutoa chanjo ya ugonjwa virusi ulitokea 2016 haraka iwezekanavyo. Na Taasisi ya Afya ya Taifa ilitupa ruzuku ndogo ya dola 400,000 kuanza kutafuta dawa ya virusi vipya vya corona vya ugonjwa wa covid-19. Lakini kwanza ni lazima tushawishi wafadhili ili watufadhili."

Mchakato mzima unaumisha kichwa, mtafiti huyo amesema.

"Sisi katika maabara tunataka kutengeneza chanjo hizi lakini hakuna ufadhili wa pesa au kutoka kwa mashirika ya serikali ambayo hutufadhili kwa utafiti huu," María Elena Bottazzi ameiambia BBC Mundo.

"Kwasababu hatuna programu endelevu na pia kipaumbele kinabadilika kulingana na kile kinachotokea kwa wakati huo."