Virusi vya Corona: Je, kuna siri ipi ya maambukizi kupungua Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita , Afrika Kusini imeafikia hali ambayo madaktari wameshindwa kuelezea: kushuka kwa ghafla kwa viwango vya maambukizi vya kila siku.
Vitanda hospitalini viko tayari, wadi zote zimeandaliwa, operesheni ambazo hazina dharura zimeahirishwa huku ambulensi zikiongezwa vifaa.
Wakati huohuo maafisa wa Afya wamekuwa wakifanya mazoezi ya maelezo ya kukabiliana na virusi vya corona kwa wiki kadhaa huku wengine wakihudumu masaa mengi katika mikutano ya mtandaoni wakijiandaa na kuimarisha mipango yao ya dharura.
Hata hivyo kufikia sasa na mbali na utabiri uliotolewa , hospitali za Afrika Kusini zimesalia kuwa tulivu:Tsunami ya maambukizi ambayo wataalam wengi walikuwa wametabiri haijafanikiwa. Ni kitu cha kushangaza.
''Hakuna anayejua kile kinachoendelea,'' anasema Dkt Evan Shoul mtaalam wa magonjwa ya maambukizi mjini Johannesburg.
Tom Boyles , daktari wa kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika hospitali ya Helen Jose mojawapo ya kituo kikubwa cha Afya pia anasema kwamba wameshangazwa na hali ilivyo.
''Tumekuwa tukitoa wito wa utulivu kabla ya virusi hivyo kusambaa kwa takriban wiki tatu. Tulikuwa tunaandaa kila kitu hapa. Lakini virusi hivyo havijatuathiri kama ilivyotarajiwa. ni kitu kisichoaminika''.

Chanzo cha picha, EPA
Wataalam wa Afya wanaonya , hatahivyo kwamba ni mapema mno kutumia matokeo hayo kama hatua muhimu iliopigwa, na wana wasiwasi kwamba huenda ikapunguza kasi ya kukabiliana na virusi hivyo
Rais Ramaphosa amependekeza kwamba wiki mbili za kujitenga ndio zilizosababisha hali hiyo na ameongeza masharti hayo kutekelezwa kote nchini kwa kuwa yalitarajiwa kukamilika katika kipindi cha wiki moja, hadi mwisho wa mwezi huu.
Hatahivyo kwa kuwa mataifa mengine pia yameweka masharti makali hayajafanikiwa kupata matokea kama hayo. ivyobasi huku taifa hilo na bara la Afrika kwa jumla likiendelea kujiandaa kwa janga baya zaidi la viruasi vya corona madaktari wanashindwa kuelezea kile kinachoendelea Afrika Kusini.
Usakaji wa juu wa watu waliokaribiana na wagonjwa
Takriban wiki tano zimepita tangu kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa nchini Afrika Kusini , na kufikia tarehe 28 Mwezi Machi idadi ya maambukizi ilikuwa ikiongezeka.
Lakini tangu wakati huo kila kitu kimekuwa kikiwa sawa na mataifa mengine ambapo visa vimekuwa vikigundulika tarehe sawa.
lakini Jumamosi iliopita idadi ya visa vya maambukizi ilishuka ghafla kutoka watu 243 kwa siku hadi 17 na hivyobasi kuwa na wastani wa visa 50 vipya kila siku.


Je inawezekana kwamba masharti makali ya Afrika Kusini ya kujitenga na kutotoka nje na usakaji wa hali ya juu ya watu waliokaribiana na wagonjwa yanaweza kuwa yanazaa matunda? ama ni mapumzika ya muda kabla ya janga baya kutokea?
Mwisho wa wiki iliopita , rais Ramaphosa alisema kwamba ni mapema mno kufanya uchanganuzi wa maana, lakini akisisitiza kwamba tangu karantini kuanza kutekelezwa , ongezeko la maambukizi ya kila siku lilikuwa limepungua kutoka asilimia 42 hadi asilimia 4 pekee.
''Nadhani jinsi tunavyoendelea kuwapima watu zaidi, ndio tutazidi kugundua iwapo ni kiwiliwili au ni kweli . Bado hatujaathirika sana'' , alisema Precious Matotso , afisa wa Afya umma ambaye anachunguza janga hilo Afrika kusini kwa niaba ya shirika la Afya duniani WHO.
Hofu ya kupunguza kasi ya kukabiliana na Covid-19
Nchini Afrika Kusini , mjadala wa kwamba bado ni mapema mno kuafikia hitimisho thabiti kuhusu kuenea kwa virusi vya corona ni wazo la kila mmoja. Ni vigumu kutabiri ni njia gani itakayochukuliwa, ile ya maambukizi ya kiwango cha kadri , ile ya kiwango cha chini ama ile ya maambukizi ya juu.
''Hatuna ushahidi wa kuenea pakubwa kwa ugonjwa huo,'' anasema Stavros Nicolaous, afisa mkuu mtendaji wa Afya ambaye ni mshirikishi wa kukabiliana na janga la corona katika sekta ya kibinafsi.

Chanzo cha picha, Getty Images
''Huenda kuna ishara za mapema za kutia moyo, lakini hofu yangu ni kwamba watu wataanza kufurahia na kuwacha kufuata masharti kulingana na data iliopo'', anaongezea.
Hali ya upweke inayosababishwa na kipindi cha utulivu kabla ya kimbunga kikali kama inavyoelezewa na waziri wa Afya Zweli Mkhize wiki iliopita inakamilishwa na uvumi.
Hali ya Hofu
Uvumi uliopo ni kwamba virusi hivyo vilivyoingizwa nchini Afrika Kusini na mataifa mengine ya Afrika na wasafiri matajiri pamoja na raia wa kigeni , vitaingia miongoni mwa watu masikini na maeneo ya mitaa yenye nyumba za kukaribiana na kusambaa kwa haraka.
Kulingana na wataalam , hii ndio awamu iliosalia ya mlipuko huo huku maambukizi kadhaa yakiripotiwa katika baadhi ya mabaraza ya miji.
Lakini madaktari hapa na katika mataifa jirani wamegundua kwamba hospitali za umma hazijapata ishara yoyote ya ongezeko la kulazwa kwa wagonjwa wenye tatizo la kupumua, ikiwa ndio ishara kwamba licha ya ukosefu wa ushahidi virusi hivyo vinasamabaa kwa haraka.
Nadharia moja ni kwamba raia wa Afrika Kusini wanakinga dhidi ya virusi hivyo.
Wengine wanahoji kwamba huneda ni kutokana na tiba kadhaa za afya, kuanzia chanjo ya kifua kikuu ambayo raia wote wanapewa wanapozaliwa , hadi tiba ya kukabilia na virusi vya ukimwi ama hata majukumu tofauti ya enzymes katika makundi kadhaa ya watu.
Lakini madai haya hayajathibitishwa.
''kama haya yamekuwepo kwa muda . Ningeshangaa iwapo ingekuwa matokeo ya chanjo....hizo ni nadharia. huenda sio za kweli''.

Chanzo cha picha, Getty Images
Profesa Salim Karim , mtaalam bingwa wa kukabiliana na HIV anaamini kuna nadharia kadhaa , lakini hakuna la kweli
''Sidhani kwamba kuna mtu duniani aliye na jibu sahihi'', alisema.
Wakati huohuo, alisema kwamba taifa hilo linajiandaa kana kwamba kuna Tusunami inayotarajiwa. Hisia iliopo ni ile ya wasiwasi, alisema.
Hali ya wasiwasi
Ukweli ni kwamba hali hii , mbali na kile kinachotokea kote duniani, kimewafanya wataalam kufikiria iwapo ni utulivu wa muda mfupi kabla ya kile ambacho madaktari wanataja kuongezeka maradufu kwa visa vya ugonjwa huo.
Wakosoaji kadhaa wamewasilisha hofu zao kwamba mfumo wa Afya nchini humo umeshindwa kuweka vipimo vya umma na kwamba serikali inategemea kliniki za kibinafsi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Taarifa za siri kutoka Idara ya Afya ambazo BBC ilizipata zinasema kwamba kumekuwa na ongezeko la hofu kuhusu usimamizi na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa serikali hususan kuhusiana na viwango vya chini vya upimaji wa virusi hiv
Lakini wasiwasi huo pia umekabiliwa na imani kubwa kwamba serikali ina ushahidi ya jinsi inavyokabiliana na janga hilo.












