Virusi vya Corona: Utaratibu wa mazishi unavyoumiza hisia na imani za jamii

Kifo corona

Chanzo cha picha, SOPA Images/Getty

Maelezo ya picha, Mfanyakazi wa afya akifukia kaburi la mtu aliyefariki kwa virusi vya corona.

Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya namna gani watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona wanastahili kuzikwa.

Nchini Kenya kumekuwa na mawswali mengi yakiulizwa na wengine wakipaza sauti na ghadhabu juu ya namna maiti za corona zinavyozikwa baada ya video moja ya mazishi kuvuja mtandaoni.

Lakini kwa ujumla wake kumekuwa na mjadala mzito katika jamii za Waislamu katika maeneo tofauti duniani juu ya nman ya kuzika ndugu na jamaa zao wanaofariki kutokana na virusi hivyo.

Tahadhari kubwa huchukuliwa na mamlaka ili kuhakikisha kuwa mazishi hayawi sehemu mpya ya maambukizi. Hivyo ndugu hawaruhusiwi kuzika moja kwa moja na badala yake shughuli hiyo hufanywa na wataalamu wa afya.

Serikali ya Kenya hii leo imetangaza mwongozo wa kufuatwa kwenye maziko ambapo watu watakaosimamia mazishi hayo watashirikisha; mwakilishi wa familia, afisa wa Afya ya umma, mwakilshi wa serikali kama vile chifu wa eneo hilo, maafisa wa usalama na afisa mwengine yeyote wa Kiafya atakayehusishwa.

Coronavirus
Banner

Hatua zitakazochukuliwa katika mazishi hayo ni kama zifuatazo.

1. Kuwasili kwa watu watakaohusika na mamzishi

2. Maafisa hao hawafai kuvaa magwanda ya kujilinda na virusi hivyo hadi watakapowasili

3. Wasalimie waliofiwa na kutoa rambirambi kabla ya kuushusha mwili kutoka kwa gari. Shirikiana na mwakilishi wa familia

4. Afisa wa Afya anapaswa kuwasiliana na mwakilishi wa familia kwa jinsi maziko yatakavyofanyika

Kabla ya kuubeba mwili huo maafisa wa Afya watahitajika kuvalia magwanda ya kujilinda dhidi ya maambukizi na wataunyunyizia mwili huo dawa kabla ya kuutia ndani ya karatasi la plastiki .

Iwapo jeneza litahitajika mwili huo utatiwa ndani yake kabla ya kunyunyiziwa dawa nyengine ya kuuwa virusi.

Mazishi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwili huo baadaye utaingizwa katika kaburi.

Baada ya mazishi maafisa wa Afya watanyunyzia dawa chumba, nguo na vitu vingine ambavyo vilitumika na marehemu ama kukaribiana navyo kabla ya kuondoka.

Na je Waislamu wanawazika vipi waathiriwa wa ugonjwa wa corona?

Kulingana na dini hiyo kutoa heshima ya mwisho kwa mpendwa ni kitu kigumu kufanyika katika maisha.

Katika baadhi ya jamii , familia hushiriki katika msururu wa ibada ili kutoa heshima kwa waliofariki.

Maswali ya waislamu ni yapi?

Kuhudhuria mazishi ni jukumu la wote [faradh qifayah] na idadi kubwa ya watu inahitajika kushiriki.

Waumini hutakiwa kwenda msikitini ili kufanya ibada za mazishi [salatul janazah} na nyumbani kwa waliofiliwa kutoa rambirambi zao, lakini huku virusvi vya corona vikiendelea kuuwa watu wengi kote duniani kila siku , wasomi maarufu na maimamu wametoa muongoza mpya ya jinsi maziko ya wale walioathiriwa na ugonjwa huo yakavyafanyika.

Katika makaazi ya kaskazini mwa mji wa Virginia kwa mfano Daoud Nassimi - imam aliejitolea amekuwa akitembelea familia ili kuelezea jinsi mazishi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona yatakavyofanyika.

Maiti corona

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maiti ya kiislamu ikisaliwa kabla ya kuzikwa. Watu imebidi wawe wachache kama tahadhari ya maambukizi ya corona.

Anasema kwamba ameshuhudia subra na uchungu mwingi kwa nyuso za familia ambazo zimepoteza wapendwa wao kutokana na masharti magumu yaliowekwa.

Wakati mtu anapofariki kulingana na dini ya kiislamu , huoshwa na maji- mila na desturi inayojulikana kama Ghusl - na baadaye ibada ya jamii inafanywa kabla ya kuzikwa.

Hutakiwa kuzikwa kabla ya saa 24 kukamilika, bila jeneza na huwa marehemu amefungwa kitambaa cheupe kwa jina Kaffan.

Cha kuvunja moyo ni kwamba mila kama hizo hazifanyiki tena wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.

Sheria mpya za mazishi zilizotolewa miongoni mwa Waislamu.

Kwa wale waliofariki kutokana na ugonjwa huo, miili yao hairuhusiwi kuguswa.

Na uoshaji wa aina yoyote na kukaribiana nao lazima uwe kulingana na muongozo wa Shirika la Afya duniani WHO.

Na kwa kuwa baadhi ya maeneo yamesitisha uoshaji wa kawaida wa miili ili kuafikia maagizo hayo , Waislamu wameanza kutumia mbinu nyengine ya Kiislamu.

Tayammum ni uoshaji wa mwili kupitia mchanga au vumbi.

Kulingana na viongozi hao wa dini mwili hutiwa ndani ya mfuko wa plastiki kabla ya tayammum kufanywa na mtu alievalia glavu ambapo mtu hushika vumbi ama mchanga na kumpaka usoni marehemu na mikononi mwake. baadaye anaombewa na kuzikwa.