Virusi vya corona: Hatari ya dawa ya hydroxychloroquine inayotumiwa na watu kutibu Covid -19

Hydroxychloroquine hupewa wagonjwa kufuatia maelezo ya daktari. Gharama yake ni ndogo zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hydroxychloroquine hupewa wagonjwa kufuatia maelezo ya daktari. Gharama yake ni ndogo zaidi

Mojawapo ya mijadala inayotokana na janga la covid-19 ni dawa za kutibu ugonjwa huo.

Miongoni mwa dawa zinazofanyiwa utafiti ikiwa inaweza kutibu vrusi vya corona ni ile ya hydroxychloroquine.

Ni dawa ambayo imetumika kwa miongo kadhaa kutibu ugonjwa wa malaria.

Pia inatumiwa kutibu ugonjwa wa mapaku mekundu ngozini yaani lupus kwa Kiingereza na ule wa ugonjwa mbaya wa yabisi-kavu yaani severe arthritis.

China ilianzisha uzalishaji wa Chloroquine Phosphate baada ya miaka 15

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, China ilianzisha uzalishaji wa Chloroquine Phosphate baada ya miaka 15

Ingawa dawa hii imekuwa ikichunguzwa, bado hakuna ushahidi unaothibitisha kwamba ni imara katika kutibu

Covid-19, hayo ni kulingana na ripoti ya shirika la the Pan American Health Organization (PAHO) iliyotolewa Aprili 6.

Shirika hilo limeonya kwamba utumiaji wa dawa ya Chloroquine au hydroxychloroquine bila kufuata mwongozo wa daktari kunaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kuumwa kupita kiasi au kifo.

Coronavirus

Je madhara ya dawa hii ambayo rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kwamba inaweza kuwa tiba ya virusi vya corona ni yapi?

WHO imesisitiza kwamba haijathibitisha dawa yoyote kutibu Covid-19

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, WHO imesisitiza kwamba haijathibitisha dawa yoyote kutibu Covid-19

Madhara ya dawa ya hydroxychloroquine

Miongoni mwa madhara ya dawa hii ya hydroxychloroquine kwa baadhi ya wagonjwa ambao wanaitumia kutibu magonjwa mengine mbali na malaria ni kuumwa na kichwa, kukosa hamu ya kula, tumbo lako kuwa na matatizo kama kuvimbiwa, kuharisha ama kupata maumivu ya tumbo, kutapika na matatizo ya ngozi, kwa mujibu wa Maktaba ya Taifa ya Utabibu Marekani

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani kinasema

Hydroxychloroquine ni dawa ambayo madhara yake yanaweza kudhibitiwa na wagonjwa wa malaria kwa kuimeza wakati ama baada ya kula.

Hatahivyo, wataalamu wanaonya kwamba athari mbaya zaidi ya utumiaji wa dawa hii inaweza kuwa kifo.

Tatizo la moyo

Kliniki ya Mayo, Marekani, kupitia taarifa yake iliyotoa Machi 25, ilionya kwamba dawa za kutibu malaria kama hydroxychloroquine na chloroquine pamoja na zile za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi za lopinavir na ritonavir zinajulikana kuwa na madhara ya uwezekano wa kupunguza presha ya kusukuma damu kubadilisha mapigo ya moyo na mtu kupatwa na mshtuko wa moyo na kufa."

Kiwango cha chembe ndani ya mwili: Baadhi ya matibabu yake yanazuia moja ya njia inayopitisha madini muhimu ya potasiamu yanayodhibiti mfumo wa moyo.

" Inapendekezwa kwamba wagonjwa wanaopokea matibabu ya dawa hiyo wafuatilie wanavyoendelea kwa karibu.

Ripoti iliyotolewa Aprili 6 na shirika la PAHO pia inaangazia wagonjwa waliopata matatizo ya moyo wakati wanatumia dawa ya hydroxychloroquine kwa minajili ya kutibu magonjwa mengine.

Kupima ili kujua jinsi inavyofanya kazi inaweza kuchukua kipindi cha kati ya mwezi mmoja hadi mwaka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kupima ili kujua jinsi inavyofanya kazi inaweza kuchukua kipindi cha kati ya mwezi mmoja hadi mwaka

Wagonjwa wa Covid-19

Hospitali ya Center Hospitalier Universitaire (CHU) huko Nice, France, ililazimika kuahirisha utumiaji wa tiba ya hydroxychloroquine na azithromycin kwa mgonjwa wa corona aliyepata matatizo ya moyo baada ya kutumia mchanganyiko wa dawa hizo.

Kulingana na daktari wa moyo, Émile Ferrari, CHU aliyezungumza na gazeti la Nice-Matin Aprili 7,

"Hydroxychloroquine ikitumiwa peke yake, uwezekano wa mgonjwa kupata maradhi ya moyo uko chini. Lakini dawa ya azithromycin ambayo inasemekana kwamba ichanganywe na hydroxychloroquine kukabiliana na covid-19 pia nayo inasababisha hali ambazo si za kawaida," amesema daktari.

"Ikiwa dawa hizi zinatumika kwa mgonjwa zinastahili kufuatiliwa kwa machine maalum ya kupima mapigo ya (electrocardiogram)

Utafiti unaonesha nini?

Shirika la Afya Dunia (WHO ) bado halijathibitisha matumizi ya dawa ya hydroxychloroquine au chloroquine kutibu virusi vipya vya corona.

Lakini ilitangaza Aprili 8 kwamba imezindua majaribio ya kimataifa kwa jina la "Solidarity," kujaribu ufanisi wa dawa ya hydroxychloroquine, chloroquine, na nyenginezi dhidi ya covid-19.

Machi 28, "Shirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani FDA lilitoa amri ya kutumia dawa ya hydroxychloroquine na chloroquine kwa watu wazima na vijana watakaolazwa hospitali kwasababu ya ugonjwa wa covid-19 na hawawezi kushiriki kwenye majaribio ya dawa hiyo.

Rais Trump amekuwa na imani kuhusu matumizi ya dawa ya Hydrochloroquine

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Rais Trump amekuwa na imani kuhusu matumizi ya dawa ya Hydrochloroquine

Aprili 7, Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Kuenea kwa Magonjwa (CDC) kilisema kwamba dawa ya hydroxychloroquine na chloroquine zinafanyiwa majaribio kwa ajili ya kuzuia na kutibu kwa wenye dalili za wastani za ugonjwa wa Corona.

Kliniki ya Mayo ilithibitisha kwamba majaribio ya maabara ya hydroxychloroquine yameonesha kuwa yanawema kuzuia virusi vya SARS-CoV na SARS-CoV-2 ambavyo vinasababisha ugonjwa wa covid-19."

"Ikiwa dawa hizi za kukinga maambukizi zinaweza kufanyakazi kama ilivyo kwa wanyama na binadamu, dawa hii inaweza kutumika kutibu wagonjwa na kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na covid-19," daktari amesema.

Dawa ya Hydrochloroquine hutumika kupitia mdomo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dawa ya Hydrochloroquine hutumika kupitia mdomo

"Mwisho wa siku, ulinganisho wa hatari zilizopo na faida kunategemea na ikiwa dawa ya hydroxychloroquine, ana iwe au isiwe na azithromycin, inafanyakazi kwa uhakika dhidi ya ugonjwa wa covid-19," imesema Kliniki.