Virusi vya Corona: Je, Tanzania inajitenga na majirani kwenye mapambano ya corona?

Uhuru Kenyatta, Paul kagame, Yoweri Museveni na John Pombe Magufuli

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marais wa Afrika mashariki Uhuru Kenyatta, paul kagame, Yoweri Museveni na John Pombe Magufuli
Muda wa kusoma: Dakika 4

Kufungwa kwa mpaka wa Tanzania na Zambia kumeongeza mjadala wa namna Tanzania inavyopambana na corona na athari kwa nchi zinazoizunguka.

Siku ya Ijumaa Kuu mwezi uliopita, Rais Magufuli alisisitiza msimamo wake wa kutofunga mipaka ya nchi akisema kuna nchi ambazo hazina bandari zinazotegemea mizigo yao kupita kutokea bandari ya Dar es Salaam.

"Sisi tumezungukwa na nchi karibu nane, tuna nchi kama ya Burundi, Rwanda, DRC, Uganda... Tungefunga mipaka wale tungekuwa tumewaua. Maana yake hakuna mafuta yeyote ambayo yangefika kwao. Maana yake hata magari yasingeendeshwa...ambulensi zinazowabeba wagonjwa wala zisingewachukua."

Mwezi mmoja kufikia sasa, madereva wa malori kutoka Tanzania wanaonekana kuwa ni tatizo katika nchi za Rwanda, Uganda na Zambia.

Kumekuwa na wasiwasi kwa baadhi ya wakaazi wa nchi zinazozunguka Tanzania kuwa kwa kuwa nchi hiyo inaweza kuchangia kuenea kwa kasi kwa maambukizi katika nchi zai kwa kuwa Tanzania haijachukua hatua kali kama za kufunga maeneo ambayo yameathirika zaidi na virusi.

Zambia imetangaza hatua ya kufunga mpaka wake na Tanzania wa Nakonde/Tunduma baada ya watu 76 kati ya 85 waliokutwa na maambukizi hivi karibuni kuwa ni maderva wa malori ama wafanya biashara ya ngono.

Rais John Pombe Magufuli

Kufungwa kwa mpaka wa Zambia pia kunamaanisha mizigo ya kutoka na kwenda katika eneo la kusini mashariki mwa DRC hususaji mji wa Lubumbashi pia itatatizika. Jiji la Lubumbashi lipo karibu na mpaka na Zambia na wafanyabiashara wake wamekuwa wakitumia bandari ya Dar es Salaam kwa mahitaji yao muhimu.

Je juhudi za kikanda zipoje?

Suala la madereva wa malori limekuwa likijadiliwa katika ngazi mbalimbali hususani nchini Uganda.

Mpaka kufikia Mei 5, zaidi ya madereva 30 wa malori walikutwa na maambukizi ya virusi vya corona, 12 wakiwa na Tanzania na 13 wakitokea Kenya.

Mwezi Aprili, Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliweka wazi msimamo wan chi hiyo kuwa wanahiji mizigo iiingie nchini humo lakini hawavihitaji virusi.

Mwishoni mwa mwezi Mei, rais Museveni alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa amezungumza na kukubaliana kuwa na mpango mmoja wa kusuluhisha suala la madereva wa malori na rais Paul kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya lakini alifanya mazungumzo tofauti kidogo na rais Magufuli.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kufikia sasa, Rwanda na Uganda wamechukua hatua ya kudhibiti maderva hao wa malori. Rwanda wanazuia malori mpakani na Tanzania ambapo dereva mwengine aliyepo Rwanda huchukua gari hilo ama mzigo kutoka Tanzania kushushwa katika eneo hilo la mpakani.

Kwa upande wa Kenya, mamlaka zimeagiza madereva wote wapimwe kabla ya kuingia bandari za nchi hiyo na kutoka nchini humo.

Museveni pia alisema kuwa janga la corona linatakiwa lishughulikiwe kwa pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kusikitika kuwa hilo halipo nan chi zinachukua njia tofauti hali ambayo amesema ni hatari.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ndiye mwenyekiti wa EAC kwa sasa na hivi karibuni amesema kuwa licha ya kuwa na wadhifa huo hawezi kuongoza nchi wananchama katika njia moja ya kupambana na janga hilo.

Kagame amesema kulikuwa na jaribio la kuitisha mkutano wa wakuu wa nchi wanachama kwa njia ya mtandao kujadili namna ya kukabiliana na janga hilo lakini ni nchi tatu tu ambazo zilikuwa tayari, huku nchi nyengine tatu viongozi wake kushindwa kujiunga.

"Kutokana na taratibu za EAC mkutano mkuu ili kufanyika lazima viongozi wote wahudhurie…hivyo ilishindikana na hata jaribio la kufanya mkutano mwengine pia limeshindikana…" amesema Kagame mapema mwezi huu.

Jinsi chanjo itakavyofanyakazi

Kwa mujibu wa runinga ya NTV ya Kenya na gazeti la The East African nchi ambazo hazikuhudhuria ni Tanzania, Burundi na Sudani Kusini.

Kiongozi wa upinzani wa Kenya na Rafiki wa karibu wa Magufuli, Raila Odinga aliliambia Shirika la Habari la Afrika Kusini SABC kuwa amefanya juhudi za kumtafuta Magufuli na kuzungumza nae lakini hajafanikiwa.

Kwa mujibu wa Odinga, viongozi wengine wa EAC pia wamekuwa wakimtafuta Magufuli.

Odinga pia amesema suala hilo linaweza kulazimisha baadhi ya nchi kwenye ukanda wa EAC kufunga mipaka yao na kuwa anatumai majadiliano yatafanyika ili kunusuru hali hiyo.

Tanzania pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na rais Magufuli ndiye mwenyekiti wa juimuiya hiyo kwa sasa.

Hata hivyo, Ijumaa ilopita ulifanyika mkutano wa baadhi ya mataifa wananchama ambayo yanapakana na Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa rais Cyrill Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye aliongoza mkutano huo wa mtandaoni, awali aliwasiliana na mwenyekiti Magufuli ambaye alimwambia angeshindwa kuhudhuria mkutano huo na kutaka viongozi wanachama kutoa mapendekezo yao.

'Tanzania haijalegalega'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Prof Palamagamba Kabudi amekanusha tuhuma kuwa nchi hiyo imelegalega ama kujitenga katika mapambano dhidi ya corona.

Kabudi amesema badala yake, nchi hiyo ikiwa kama kiongozi wa SADC imetoa uongozi madhubuti katika kukabiliana na janga hilo kwenye ukanda huo.

"Si kweli kama Tanzania imejibagua, si kweli kama Tanzania imejitenga…Tanzania imetoa uongozi katika eneo tulilopewa la dhamana la SADC, ndio maana sasa tuna miongozo ya usafirishaji wa bidhaa muhimu na miongozo hiyo minne imetolewa na kukubaliwa nan chi zote za SADC…"amesema Kabudi baada ya kupokea dawa za mitishamba kutoka Madagascar.

"Tanzania imefanya vizuri sana katika kuratibu SADC katika kukabiliana na tatizo la corona. Tanzania akiwa mwenyekiti ameitisha mikutano mitatu, mkutano wa kwanza ulikuwa wa mawaziri wa Afya, ambao moja walikubaliana kuwa mikutano yote ya SADC ifanyike kwa njia ya mtandao, pili tukaunda timu ya wataalamu wa SADC kuandaa muongozo na utaratibu wa kukabiliana na Corona. Na miongozo hiyo imekamilika."