Virusi vya corona: Simba sasa wanapumzika barabarani Afrika Kusini

Lions in Kruger National Park

Chanzo cha picha, Richard Sowry/Kruger National Park

Muda wa kusoma: Dakika 3

Wakati huu ambapo baadhi ya mataifa ya Afrika yameweka marufuku ya kutotoka nje ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corano, bila shaka wanyamapori wamegundua kuwa watu wameondoka.

Katika moja ya hifadhi kubwa ya wanyama pori barani Afrika Simba wameamua kuchukua fursa hiyo kujipumzisha barabarani.

Msimamizi wa hifadhi ya Kruger nchini Afrika Kusini Bw. Richard Sowry siku ya Jumatano, alipokuwa katika operesheni ya kikazi alikutana na kundi kubwa la Simba waliokuwa katika usingizi mzito katikati ya barabara tofauti na hali ya kawaida ambapo watalii au wageni ndio wengi barabarani.

Lakini hifadhi ya Kruger, kama ilivyo hifadhi nyingine zimefungwa tangu Machi 25, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na virusi vya corona.

Walinzi wa hifadhi hiyo wanasema kwa kawaida simba huwa wanaonekana barabarani nyakati za usiku.

Picha hii ilipigwa vipi?

Bw Sowry alikuwa anaendelea na shughuli ulinzi kuangalia kama wawindaji pori hawavamii wanyama katika muda wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.

Simba ambaye ana umri mkubwa zaidi ni miaka 14, hivyo wamezoea kuona magari.Kwa kawaida bwana Sowry huwa anawaona simba wakiwa wamelala katika barabara za hifadhi wakati wa usiku katika majira ya baridi.

Lions in Kruger National Park

Chanzo cha picha, Richard Sowry/Kruger National Park

Wakati alipokuwa akiendesha gari karibu na hifadhi majira ya mchana siku ya Jumatano, aliwaona samba wakiwa wamejaa barabarani wakiwa wamelala jambo ambalo si la kawaida,hivyo ilimbidi arudi nyuma kama mita tano na kuwangalia.

Wakati akipiga picha kwa simu yake, Simba hao hata walikuwa hawajishughulishi kwanza wengi walikuwa katika usingizi mzito.

"Simba wamezoea watu wakiwa kwenye magari," alieleza.

"Wanyama wote huwa wanaogopa watu wakiwa wanatembea, hivyo kama ningetembea wasingeweza kuniruhusu."

Kitu ambacho askari pori hawataki ni kuona simba kudhani kuwa barabara ziko salama kwa wao kupumzika.

Lions in Kruger National Park

Chanzo cha picha, Richard Sowry/Kruger National Park

Marufuku dhidi ya Corona imeathiri hifadhi za wanyama kiasi gani?

Nyakati hizi simba wanakuwa wanaonekana wakiwa maeneo ya wazi kama mbwa pori katika hifadhi lakini kwa upande mwingine bwana Sowry anadhani kuwa marufuku ya kuzuia watu kutoka nje haiweza kuleta mabadiliko makubwa katika tabia za wanyama pori.

"Hifadhi ya Kruger ni eneo la pori sana," alisema. "Limekuwa eneo la wanyama pori na litaendelea kuwa eneo la wanyama pori."

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Anafurahia kuwashirikisha watu kuona picha zake kwa sababu sasa watu hawawezi kwenda kwenye mbuga za wanyama kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

"Hii hali ni ngumu sana kwa kila mtu na lengo langu ni kuwapa watu furaha," alisema.

Siku ambayo Afrika Kusini ilirikodi vifo 34 vya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na idadi ya watu wenye maambukizi kuwa 2,506 na kufanya taifa hilo kuwa ndio lililoathirika zaidi barani Afrika.

Presentational white space

Marufuku ya kutotoka nje nchini, imeongezwa kwa muda wa wiki mbili nchini Afrika Kusini.

"Kila mtu ameelewa umuhimu wa marufuku hiyo na walinzi wa wanyama pori wapo kazini kufanya kazi zao za kila siku," alisema afisa wa habari Isaac Phaala.

Kwa upande wao simba, aliongeza, "kawaida wapo porini kwa sababu na sasa wanafurahia maisha kwa sababu wana uhuru wote, hakuna watu wanaokuja kuwaona".

Lions in Kruger National Park

Chanzo cha picha, Richard Sowry/Kruger National Park

Lakini katika mbuga yeyote ya wanyama, unadhani ukiuliza simba anapenda kukaa kwenye lami au kwenye nyasi?

Lakini labda kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Jumanne, ndio maana waliona bora kukaa kwenye lami kwa wakati huo kwa sababu simba hawapendi unyevunyevu yaani simba hawapendi kukaa katika maji.

Coronavirus
Banner