Uchaguzi Malawi: Kufutwa kwa uchaguzi kuna maana gani kwa demokrasia Afrika?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wafuasi wa upinzani nchini Malawi wamekuwa wakisherehekea baada ya mahakama ya majaji watano kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.
Wengi wao walisema kwamba huu ni uhsindi kwa demokrasia baada ya wagombea wawili walioshindwa kusema mahakamani kwamba kumekuwa na makosa katika uchaguzi huo ambapo rais Peter Mutharika alitangazwa mshindi kwa muhula wa pili. Ameamua kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Alitangazwa mshindi akiwa na asilimia 38.6 ya kura zilizopigwa. Hio ikiwa chini ya kura 159,000 zaidi ya mpinzani wake wa karibu lazarus Chakwera. Uchaguzi huo sasa utalazimika kufanyika katika kipindi cha miezi mitano ijayo. Lakini huenda ukafnyika chini ya sheria tofauti.

Chanzo cha picha, AFP
Je majaji walisema nini?
Kwanza , majaji hawakutoa uamuzi wa kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu. Walisema kwamba ushahidi wa wizi wa kura ulitapakaa kila mahali. Na ikajitokeza wazi kuwa uadilifu ulikosekana.
Majaji, kwa upande wao walisema kuwa raia wa malawi wanastahili na watarajie uchaguzi wenye kuzingatia uadilifu siyo eti usio na makosa yoyote lakini ambao hautakuwa na hitilafu ambazo zinaweaza kuepukwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasiwe ni wenye kufanya uchaguzi sawa ambao umezoeleka katika baadhi ya mataifa na taasisi.
Pili, mahakama iliagiza bunge la Malawi kufikiria kuwa tena na tume ya sasa ya uchaguzi kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unafanyika kwa njia ya haki".
Kufanya hivyo, wanaashiria kwamba wale wanaohusika katika kufanya uchaguzi wenye dosari kama hizo wanastahili kuondolewa.

Pia waliashiria kwamba adhabu kidogo tu haitoshi na demokrasia katika taasisi za Malawi inastahili kulindwa na kutetewa ipasavyo.
Hii ilikuwa ni pigo kubwa dhidi ya utamaduni wa kufanya maovu bila kuadhibiwa.
Tatu, mahakimu hao walisema kwamba mfumo wa kuchagua rais kwa misingi ya kwamba amepata kura nyingi hata ikiwa hana wingi wa kura ni kinyume cha sheria.
Kwasababu ya siku za usoni, walisema, mshindi alihitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa na hilo linaweza kumaanisha kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Hilo linaweza kuwa na athari za kisiasa kwa Malawi na cha msingi ni kuhamasisha wagombea wa upindani na vyama vya kisiasa kuingia katika miungano ya kimakakti na kuwapa nguvu ambayo haikutarajiwa.
Kimsingi, umauzi wa mahakama umepunguza nguvu ya kiongozi aliye madarakani, ambayo mara nyingi huwa ni imara na yenye kuweza kutekeleza unyanyasaji dhidi ya wanaotafuta demokrasia
Kwanini umauzi huu ni jambo zito?
Majaji walikuwa na uwezo wa kunyamazia hili.
Walikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi tofauti au hata kuogopa. Pia walikuwa na uwezo wa kusema kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ya udanganyifu, lakini kwasababu hakukuwa na ushahidi wa kuonyesha majibu yalibadilishwa hakukuwa na haja ya kuchukua hatua kama hiyo.
Pia walikuwa na nafasi ya kutoa fursa ya pili ya tume ya uchaguzi.
Walikuwa na uwezo wa kusema kufanyike mabadiliko fulani kabla ya uchaguzi ujao.
Madala yake, mahakama ya juu zaidi ya Malawi, walichukua fursa hii sio tu kutingisha siasa za ndani ya nchi na mfumo wa uchaguzi, lakini pia kutuma ujumbe wa nguvu ya mahakama na uhuru kwa nchi zingine za Afrika ambazo bado zinawakati mgumu wa kuondokana na mfumo wa utawala wa chama kimoja hadi vyama vingi.

Chanzo cha picha, AFP
Kufikiria tu vile uchaguzi wa Zimbabwe au Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulivyofanyika hivi karibuni ungelikuwa tofauti na ilivyoshuhudiwa, iwapo mahakama zao zingekataa kuvumilia tabia ambayo imezoeleka.
Ni rahisi sana kutilia mkazo umuhimu wa uamuzi uliotolewa Malawi.
Kufanyika kwa uchaguzi mwengine kutaingiza hofu ndani katika utawala wa madikteta Afrika. Pia kunaweza kusababisha ukosefu wa uthabiti zaidi wa Malawi yenyewe.
Lakini uamuzi huu umekuwa mfano muhimu, na unastahili kufanya makundi kama vile Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Afrika ya Kusini (SADC) kujifikiria tena ambayo waangalizi wake wameshtumiwa kuwa na haraka ya kuondoa uwezekano wa uwepo wa nia mbaya katika uchaguzi kama huo.
Sadc imekuwa ikijitahidi kuonyesha kwamba haina upendeleo katika uchaguzi wa malawi lakini ukosefu wa uwazi ni jambo ambalo haliwezi kufichika.
Nini kitatokea?
Rais Mutharika ameonyesha nia ya kwasilisha ombi la kupinga uamuzi huo wa mahakama. Uamuzi huenda ukazua wasiwasi zaidi nchini humo hata kama ni kwa muda mfupi.
Kinachosubiriwa kwasasa ni ikiwa kuna ombi la kupinga uamuzi huo litakalo wasilishwa, kasi ya kushughulikiwa kwa ombo kama hilo na iwapo uamuzi wa mahakama unaweza kutenguliwa.
Kando na uamuzi huo kuwasilishwa mahakamani, Malawi ina chini ya miezi mitano kuandaa na kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi mpya, kubadilisha sheria za uchaguzi na kufanya mabadiliko katika tume nzima ya uchaguzi pamoja na kuhakikisha sheria inadumishwa wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa wa kisiasa.
Hili ni agizo zito kwa nchi yoyote ile. Hakuna uhakika kwamba mfumo wa mahakama utaingilia kuhakikisha njia stahiki inafuatwa.
Ina maana gani kwa nchi za kiafrika?
Baada ya miaka kadhaa ambayo demokrasia imeonekana kukua barani Afrika, waangalizi wengi wanaona sasa dalili za kurudi nyuma.
Kwa muktadha huo, Uchaguzi uliofutwa nchini Malawi unaweza kutia chachu kwa watu wanaofanya kampeni wakitaka demokrasia na wanaharakati wa nchi nyinginr, lakini pia inaweza kufanya serikali za kimabavu kukata makali ya majaji huru ili kuweka vikwazo mahakama kuingilia masuala ya siasa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na ni funzo gani vyama vya siasa barani Afrika vinapata kutoka Malawi?
Wengi kwa nia njema, wanasheherekea mafanikoo ya wenzao huko.
Baadhi wanaweza kuhitimisha kuwa njia ya kuwa na mamlaka ipo kwenye mutano wa kisheria, na wakati mwingine maandamano ya sambamba na vurugu.
Somo kubwa kwa vyama vya upinzani-Bado haijajaribiwa nchini Malawi, lakini ilishafanyika DR Congo na nchi nyingi nyingine- ni kuwa mafanikio ni kufanya maamuzi magumu, ustahimilivu, na kuhakikisha kuwa umoja unajengwa,kujenga majukwaa ya sera yenye nguvu.












