Watu 36 wafariki katika maporomoko ya udongo magharibi mwa Kenya

People gather around the road that was destroyed by heavy rain near Kapenguria, West Pokot County

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mvua kubwa yasababisha maporomoko ya ardhi ya magharibi mwa Kenya
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mafisa nchini Kenya wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na tukio la maporomoko ya udongo katika eneo la Pokot magharibi imefikia 36.

Hii ni baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko iliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Maporomoko hayo yameathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, ambavyo vinasemekana kutenganishwa baada ya daraja kusombwa na.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametuma risala za rambi rambi kwa familia zilizoathiriwa na mkasa huo.

''Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mkasa huu, kwa wale waliojeruhiwa na ambao wanaenelea kupokea matibabu katika hospitali mbali mbali, nawaombea uponyaji wa haraka'' alisema rais Kenyatta.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Rais aidha ameagiza ndege ya kijeshi kupelekwa katika eneo hilo kusaidia katika shughuli ya uokozi na kutoa wito kwa mamlaka katika eneo hilo kushirikiana na asasi za usalama kufanikisha oparesheni ya uokozi.

Chifu wa Nyarkulia Joel Bulal, amenukuliw na vyombo vya habari akisema kuwa kuwa shughuli za uokozi zinaenedelea huku na kuwatafuta wale ambao hawajulikani waliko.

Kamishena wa jimbo hilo Apollo Okelo amesema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na kuongeza kuwa shughuli ya kuwaokoa zinaathiriwana hali mbaya ya hewa.

Viji vilivyosombwa na maji ya mafuriko

Chanzo cha picha, Mark Meut

Maelezo ya picha, Vijiji vilivyosombwa na maji ya mafuriko

Hali ya hewa imekuwa mbaya zaidi

"Tunajaribu kutafuta mahali ambapo daraja limesombwa na maji ya mafuriko,"alinukuliwa na mtando wa habari wa Standard nchini Kenya.

Licha ya tamko hilo la bwana Okello baadhi ya wanakijiji wanasema kinachoendelea kwa sasa ni ndege aini ya helikompta imekuwa ikizunguka katika eneo la tukio.

Shughuli za uchukuzi zimeathirika kabisa katika eneo hilo huku magari ya usafiri zaidi ya 200 zikikwama.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha miti iliyosombwa na maji na mingine kung'olewa, huku matope yakisambaa barabrani.

Katika Twitter yake, Shirika la Msalaba mwekundu limethibitisha ripoti zinazoashiria tukio la maporomoko "makubwa" ya matope.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Map of Kenya showing West Pokot county and Nairobi
Maporomoko hayo yalioathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua,

Chanzo cha picha, Mark Meut

Maelezo ya picha, Maporomoko hayo yalioathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua,

Kumeshuhudiwa mvua nyingi katika eneo la Afrika Mashariki na upembe wa Afrika kwa wiki kadhaa sasa.

Kijiji kizima kimesombwa na maji nchi Sudan Kusini huku visa ajaliya maporomoko ya ardhi ikiripotiwa Tanzania, Ethiopia na Somalia.

Wanasayansi wanasema hali mbaya ya hewa inatarajiwa kukumba baadhi ya nchi katika kanda hiyo kwasababu viwango vya joto katika bahari Hindi vinatarajiwa kupanda kupita kiasi cha kawaida, hali ambayo huenda ikasababisha mvua kubwa.