Israel-Iran: Kuna hatari ya kuzuka kwa mgogoro mkubwa

Chanzo cha picha, Reuters
Mashambulizi ya angani yaliotekelezwa na jeshi la Israel dhidi ya maeneo inayolenga Syria yanaadhimisha hatua ya hivi karibuni ya malumbano kati ya Israel na Iran swala ambalo huenda likazua mgogoro mkubwa.
Iran inataka kuimarisha jeshi lake katika ardhi ya Syria .
Israel iko tayari kuizuia nchi hiyo kufanya hivyo. Lakini Iran haionyeshi ishara za kuchoka ama hata kurudi nyuma , inaendelea kujiimarisha kijeshi na kuonyesha kujiamini.
Mataifa hayo mawili yanajaribu kuweka sheria mpya za kujilinda lakini hatari ni kwamba huku makabiliano hayo ya kijeshi yakiendelea , mgogoro mkubwa huenda ukatokea.
Msururu wa mashambulizi hayo pia ni wa kawaida. Mashambulizi ya Israel yalishinikizwa na mashambulizi ya makombora manne kutoka Syria mapema wiki hii ambayo yalitunguliwa na mfumo wa kuzuia makombora ya angani wa Israel.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa hatahivyo zinasema kwamba makombora yaliorushwa angani huenda yalirushwa na Iran ili kujibu mashambulizi ya Israel dhidi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran aidha nchini Iraq au katika ukanda wa Gaza.
Kiwango cha mashambulizi ya Israel kilikuwa muhimu.
Iliwalenga wapiganaji wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Iran baadhi yao wakiwa ndani ya vifaa vya kijeshi vya Syria.
Makao makuu ya Syria pia yalishambuliwa pamoja na vifaa 6 vya kijeshi vinavyorusha makombora angani kutoka ardhini, ili kutoa fursa kwa ndege za kijeshi kutekeleza mashambulizi yake bila bughdha.
Chanzo kimoja cha usalama nchini Israel kimesema kwamba mashambulizi hayo yalilenga kulipiza kisasi. Ujumbe kutoka Israel kwa Tehran ulikuwa wazi. Mashambulizi yoyote nchini Syria yatakabiliwa na majibu makali.
Lakini pia Iran inatuma ujumbe wake. Licha ya kampeni ya muda mrefu ya Israel inayolenga kuzuia Iran kujiimarisha Syria , Tehran imesema kwamba mipango yake nchini humo itaendelea.
Ni mwandani mkuu wa utawala wa rais Assad mjini Damascus na inaona mpaka kati ya Israel na Syria kama fursa muhimu ya kuishambulia Israel mbali na kuwa eneo muhimu la kushirikiana na wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon.
Kufikia sasa , mambo yanaonekana kuwa ya kawaida. Lakini baadhi ya mikakati ya kijeshi inabadilika huku uadui kati ya Israel na Iran ukiendelea kuwa hatari sana.

Chanzo cha picha, EPA
Mabadiliko ya kwanza ya uwezo wa Iran. Mashambulizi dhidi ya vituo vya mafuta vya Saudia mwezi Septemba kupitia ndege zisizo na rubani na makombora yanadaiwa kutekelezwa na Tehran , licha ya kwamba taifa hilo limekana hayo.
Kiwango cha mashambulizi hayo na jinsi yalivyotekelezwa yaliwashangaza wachambuzi wengi. Israel imejiandaa kukabiliana na adui aliyejihami vikali katika siku za usoni .
Mchanganyiko wa Makombora ya masafa marefu na yale yanayosafiri chini chini mbali na juhudi kubwa ya Iran kuimarisha umbali na lengo la makombora inayowapatia washirika wake wa Hezbollah na makundi kadhaa kule Gaza.
Huu ni mpango wa usahihi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa. Mafanikio ya mashambulizi dhidi ya Saudia yalionyesha kile ambacho Iran inaweza kufanya.
Iran, licha ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa ili kuzuiliwa, imekuwa mshirika muhimu wa kijeshi katika eneo hilo. Hili lilionekana wazi kufuatia chapisho la Pentagon wiki hii kuhusu ripoti mpya ya nguvu za kijeshi za Iran.
Katika upande mmoja kuna mipango ya michakato. Marekani mara kwa mara huweka ripoti kuhusu uwezo wa kijeshi wa Urusi na China , na ili kuonesha kwamba Iran ipo katika orodha ya mataifa hayo ni upuzi.
Lakini Tehrana imenoa uwezo wake, na kulingana na ripoti hiyo , imeangazia vitengo vitatu: Makombora ya masafa marefu, jeshi la wanamaji kutishia meli zinazopitia katika mkondo wa Hormuz uliopo Ghuba mbali na utumiaji wa washirika wake, makundi ya wapiganaji katika eneo lote la mashariki ya kati , ikiwemo Lebanon, Iraq, Yemen na katika ukanda wa Gaza.
Swala la pili ni lile la kidipolamasia katika eneo lote la mashariki ya kati, na hususan kufuatia kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Syria ,hatua iliothibitishwa pekee na Donald Trump baada ya kuviwacha pekee vikosi vya Wakurdi nchini Syria.
Hii imetoa mazingira ambapo washirika muhimu, kama vile Israel, Uturuki na Iran wote wanapigania maslahi yao.
Kuondoka kwa Washington hatahivyo ni fursa kwa Moscow ambayo lengo lake kuu ni kuhakikisha kuwa rais Assad anasalia uongozini.
Mbali na hilo ni kuendeleza ushawishi wake wakati ambapo ushawishi wa Marekani unapungua. Huwezi kusema Urusi ina malengo gani haswa lakini ni mshirika muhimu wa kidiplomasia nchini Syria.
Taifa hilo pia lina uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Israel, na mara kwa mara hupuuza mashambulizi ya Israel nchini Syria licha ya kuwa na mifumo ya kulinda mashambulizi ya angani ya kiwango cha hali ya juu nchini humo.
Lakini licha ya juhudi kutoka kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu , rais wa Urusi Vladmir Putin amekataa kuizuia Tehran.













