Benki Kuu Zimbabwe imeshindwa kutoa fedha mpya kama ilivyotarajiwa

Uchumi wa Zimbabwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dola ya Zimbabwe

Benki kuu ya Zimbabwe imeshindwa kutoa noti mpya za benki kama ilivyotarajiwa , ambazo zitasaidia kupambana na upungufu wa fedha nchini humo pamoja na kukabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Ilitangaza ingetoa noti za dola mbili na sarafu za dola tano, noti za kwanza za sarafu za kweli katika miaka 10.

Nchi hiyo ilipiga marufuku dola ya Marekani mnamo mwezi Juni mwaka huu lakini imekuwa ikitumia pesa za kienyeji, barua ya dhamana ambayo imekuwa ikipatikana kwa muda mfupi.

Hata hivyo benki hiyo imejawa na hofu kwa sababu kitendo hiki kitachangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei, na kusisitiza fedha hizi hazitoongeza usambazaji wa pesa kwa ujumla.

Mwanzo huu unaonyesha hatua ya mwisho ya marudisho ya dola ya Zimbabwe.

Mwezi Juni benki kuu ilipiga marufuku matumizi ya dola za kimarekani, zilizoanza kutumika mwaka 2009 kama njia mbadala ya fedha za ndani, kusaidia hali ya kiuchumi kurudi kawaida.

Serikali inasema fedha hizi mpya itapunguza upungufu wa fedha ambayo imesababisha watu wengi kutoweza kutoa hela zao zilizopo benki.

Hofu kubwa hapa ni uletwaji wa fedha hizi katikati ya matatizo ya kiuchumi itazidi kuchochea mfumuko wa bei.

Fedha za zamani za Zimbabwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fedha za zamani za Zimbabwe

Mkate uliokuwa unauzwa dola moja mwezi January, kwa sasa unauzwa kwa dola 15 za kizimbabwe.

Tangu kurudishwa kwa fedha hizi, mfumuko wa bei umeongezeka mara tatu zaidi.

Serikali ya Zimbabwe imeacha kuchapisha takwimu rasmi, ila kwa sasa inasemakana kuwa inakiwango cha asilimia 300.

Benki kuu imeiambia BBC kuwa baadhi ya benki zimeanza kukusanya fedha mpya na zitaanza kusambazwa siku ya Jumanne.