Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan wautembelea msikiti wa kale zaidi

The Duke and Duchess of Sussex arrive at South Africa's oldest mosque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni ziara ya kwanza ya Harry na Meghan nje ya nchi kama wazazi

Mwanamfalme wa Uingereza na mke wake wanaofahamka kama The Duke and Duchess of Sussex walikula chakula cha kitamaduni cha Afrika Kusini na kuutembelea msikiti wa taifa hilo uliojengwa miaka mingi katika ziara yao ya siku mbili nchini humo kama sehemu ya zaiara yao ya siku 10 barani Afrika.

Wawili hao kutoka familia ya Ufalme wa Uingereza waliutembelea msikiti wa Auwal uliopo Bo-Kaap, mjini Cape Town, uliojengwa miaka 225 katika siku ya taifa ya urithi na turathi nchini Afrika Kusini - siku ambayo huwa ni ya mapumziko kwa umma kwa ajili ya kusherehekea utamaduni wa taifa hilo.

Unaweza pia kusoma:

Mapema , walitembelea shirika la misaada linalowasaidia vijana wenye matatizo ya kiakili.

Ziara yao ni ya kwanza nje ya nchi kuifanya wakiwa na mtoto wao wa kiume Archie.

Harry and Meghan at a family's home in Cape Town

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Harry na Meghan walipokaribishwa nyumbani kwa familia moja mjini Cape Town
Meghan at South Africa's oldest mosque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meghan akiwa ndani ya msikiti wa kale zaidi
Meghan greets a well-wisher

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meghan akiwasalimia watoto wa shule wakati wa ziara yake nchini Afrika Kusini
Meghan in

Chanzo cha picha, Reuters

Katika ziara yao katika msikiti Mwanamfalme Harry na Meghan walikutana na viongozi wa dini ya Kiislamuakiwemo Imam Sheikh Ismail Londt na kiongozi wa jumuiya ya Waislamu mjini Cape Town Mohamed Groenwald.

Meghan alivalia burqa kichwani alipoingia katika msikiti wa kale uliojengwa mwaka 1794 katika wilaya ya Bo-Kaap unaofahamika kwa mitaa yenye nyumba ailizopakwa rangi za kuvutia r

Kabla ya kwenda msikitini , wawili hao walipigwa picha wakila chakula katika nyumba ya familia moja.

Shaamiela Samodien, mwenye umri wa miaka 63, aliliambia shirika la habari la AFP: "Tumezowea kupika chakula kwa ajili ya sherhe kubwa na familia. Kwa hiyo ihatukutumia juhudi kubwa kuwapikia Harry na Meghan.

Mapema , Harry na mkewe walitembelea ufukweni mwa jiji la Cape Town kujifunza kuhusu mradi wa kuwasaidia vijana wenye matatizo ya kiakili.

Wawili hao walikutana na watu wanaowasaidia wagonjwa hao katika ufukwe wa Monwabisi kusikia kutoka kwao kazi hiyo inayofanywa na shirika lisilo la kiserikali linalofahamika kama Mawimbi ya mabadiliko ama Waves for Change.

Harry na Meghanpia walielezwa kuhusu mfuko unaofahamika kama fedha Lunchbox Fund, ambao huchagiwa kwa misaada ya umma baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa kiume Archie.

The Duchess of Sussex, Meghan, meets with members of the NGO Waves for Change

Chanzo cha picha, Reuters

Meghan with members of Waves for Change

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, The duchess joined the NGO for a session on Monwabisi Beach
Prince Harry and Meghan pose with surf mentors as they visit Waves for Change

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Prince Harry and Meghan met surf mentors and some of the young people they help
Meghan embraces a member of the NGO Waves for Change

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Meghan akimkumbatia mjumbe wa shirika lisilo la kiserikali la Waves for Change

Waves for Change hutoa misaada ya kimwili na kisaikolojia kwa pamoja kama sehemu ya huduma rafiki za watoto kwa ajili ya vijana wadogo wenye matatizo.

Shirika hilo ambalo linawasaidia watoto 1,200 lipo katika eneo la kuegesha kontena zinazosafirishwa ng'ambo lililoko ufukweni.

Lunchbox Fund hutoa takriban milo 30,000 kwa siku kwa watoto walioorodheshwa kwenye mpango huo, pamoja na watoto wa shule.

Unaweza pia kusoma:

Alipoulizwa kuhusiana na suala muhimu katika kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya wagonjwa wenye magonjwa ya akili, Meghan alisema "Ni kuwawezesha tu watu kuzungumza juu ya yake na kuongea pamoja , sawa ?

"Na unaona kwamaba popote utakapokuwa duniani , kama ukiwa miongoni mwa jamii ndogo au mji , kama upo katika mji mkubwa kila mtu anakabiliana na aina tofauti ya suuala linalofanana na hili ."

Mwanamfalme Harry aliongeza kuwa "Kila mtu amekutana na kiwewe au anakabiliwa na uwezekano wa kupata kiwewe wakati mmoja maishani mwake.

"Tunahitaji kujaribu, sio kumaliza tatizo , bali kujifunza kutoka kwa vizazi vilivyopita hakuna jambo lisilokuwa na mwisho ."

Meghan and Harry visit the Waves for Change

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meghan na Harry pia walijifunza kuhusu mfuko wa Lunchbox
People hold up masks depicting Britain's Queen Elizabeth

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu walivalia sanamu za Malkia Elizabeth kama ishara ya maandalizi ya ziara ya Meghan na Harry

Alisema kuwa kizazi chote cha watoto ambmbacho hakina ''watu wanaowaangalia kama mfano wa kuigwa kabisa '' sasa kinapatiwa fursa hiyo.

Ufukwe wa Monwabis uko kando ya mji mkubwa nchini Afrika kusini wa, Khayelitsha.

Wakati wa ziara yao , wawili hao walijiunga na waalimu 25 waliokuwa wakiwashangilia kwa makaribisho

A dancer performing in the Bo Kaap district of Cape Town

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, kikundi cha densi kikitumbuiza kabla ya kuwasili kwa Meghan na Harry katika wilaya ya Bo Kaap mjini Cape Town
Megahn speaks to Jade Bothma, centre, and Hunter Mitchell before handing them the Commonwealth Point of Light award during a reception for young people

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Megahn akizungumza Jade Bothma, katikati na Hunter Mitchell kabwa ya kuwakabidhi zawadi katika makazi ya balozi wa Uingereza mjini Cape Town

Walimalizia mikutano yao na vijana viongozi wa kijamii katika katika ubalozi wa Uingereza

Siku ya kwanza ya ziara yao ilitawaliwa na mikutano na wasichana walio katika umri wa balehe katika mji wa nyanga ambapo walizungumzia kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto