Utafiti: Kula mayai kila siku kunaweza kusababisha magonjwa ya moyo

An egg on two pieces of toast

Chanzo cha picha, Getty Images

Kula mayai pamoja na vyakula vingine kunaweza kuusaidia mwili kufyonza madini muhimu kwa afya bora, wataalamu wa afya wanasema.

Kwa mfano utafiti umebaini kuwa kuongeza yai katika saladi kunachangia kiwango cha vitami E tunayopata katika saladi

Lakini kwa miongo kadhaa sasa, wataalamu wamekuwa wakiumiza vichwa ikiwa ulaji wa mayai ni mzuri au mbaya kwa afya yako.

Yawezekana jawabu la swali hilo linategemean na mayai mangapi unakula kwa wiki - hayo ni kulingana na utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la jumuiya ya matabibu wa Marekani (JAMA).

Kwa mujibu wa jarida hilo, kula mayai mawili tu kwa siku kunaweza kusababisha magonjwa ya moyo na hata kifo cha mapema.

Bacon and egg sandwich

Chanzo cha picha, Getty Images

Hilo linatokana na kiwango kikubwa cha kolestro kinachopatikana kwenye kiini. Yai kubwa moja linakuwa na mpaka miligramu 185 za kolestro kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Marekani - zaidi ya nusu ya kiwango cha kolestro ambacho Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri mtu ale kwa siku, miligramu 300.

Na katika takwimu za hivi karibuni kutoka Kamati ya kimataifa ya Yai , kuanzia 2015, inaonyesha kuwa Marekani ni nchi ya tano kwa ulaji zaidi wa mayai duniani - huku kila mtu akila mayai 252 kila mwaka. Lakini nchi hiyo ina matatizo ya moyo ambayo husababisha 20% ya vifo.

Japan, ambako ulaji wa mayai unafikia kiwango cha mayai 328 kwa mtu ,ilirekodi 11% pekee.

"Ulaji wa mayai jisai walau mayai 3 hadi 4 kwa wiki - ni sawa ," Waliongeza wataalamu wa Uingereza

Yai la kukaanga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Siwaambii watu wayaondoe kabisa kwenye milo yao," alisema. "Ninapendekeza tu kwamba watu wayale kiasi ." Tom Sanders

Idadi inayoshauriwa.

Ni mayai mangapi unapaswa kula ?

Muandishi mwenza wa utafiti Allen anapendekeza usile mayai zaidi ya matatu kwa wiki.

Pia anatoa ushauri kwa wanaopenda kula mayai, mfano kula hasa sehemu nyeupe ya yai .

"Siwaambii watu wayaondoe kabisa kwenye milo yao," alisema. "Ninapendekeza tu kwamba watu wayale kiasi ."

Tom Sanders pia anasema kwamba utafiti uliwalenga Wamarekani.

"Wastani wa kiwango cholesterol kinacholiwa na Wamarekani kinaweza kufikia karibu mayai 600, hiki kikiwa ni kiwango cha wastani wa juu kuliko kile kinacholiwa nchini Uingereza ,ambacho ni miligramu 225 kwa siku ," Tom Sanders alieleza.

Mayai yaliochemshwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utafiti umebaini kuwa kula zaidi ya yai moja hata ukiongeza nusu zaidi kunahusishwa na hatari ya kupata ugonjwa wa moyo

Utafiti uliochapishwa mapema mwaka huu unapinga madai kwamba kula mayai hakuna madhara kwa afya yetu.

Watafiti walichunguza data 30,000 ya watu waliofuatiliwa kwa miaka 17 na kubaini kuwa kula zaidi ya yai moja hata ukiongezea nusu kwa siku kunamweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo au hata kifo.

"Tulibaini kula kula zaidi ya yai moja hata ukiongeza nusu kila siku kulichangia kwa 6% hatari ya mtu kupata ugonjwa wa moyo,''anasema Norrina Allen,Profesa mshiriki wa madawa ya kinga katika Chuo Kikuu cha Northwestern University na mwandishi wa utafiti.

Utafiti huo uliangazia data ya aina moja iliyotokana na ripoti ya washiriki waamekula nini - waliulizwa walichokula katika kipindi cha mwezi mmoja au mwaka kisha ikafuatiwa na matokeo ya vipimo vya hali ya afya yao kwa hadi miaka 31.

Hii inamaanisha kwamba watafiti walipata kiasi kidogo kile ambacho washiriki walikua wanakula japo walibadisha chakula mara kwa mara

Mayai

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, …lakini tafiti zingine zimebaini kuwa ulaji wa mayai unauhusiano wa karibu na hatari ya mtu kupata maradhi ya moyo

Tafiti za awali zitofautiana

Utafiti mpya unatofautiana na kazi za tafiti za awali ambazo zilibaini kuwa hakuna uhusiano kati ya ulaji wa yai na uwezekano wa hali ya juu wa kupata magonjwa ya moyo.

Lakini Allenanasema kwamba hazona zilikuwa na sampuli tofauti chache na zilikuwa na muda mfupi wa kufuatilia walaji wa mayai.

hata hivyo, watafiti wanakiri kuwa huenda kuna makosa katika uchunguzi wao.

Data kuhusu ulaji wa yaizilikusanywa kwa njia ya maswali ambapo ilibidi walioulizwa kukumbuka chakula chao katika kipindi cha miezi na miaka

Watafiri wengine pia walisema kuwa matokeo ni ya kuchunguzwa na ingawa walieleza uhusiano kati ya ulaji wa yai na kuongezeka kwa hatari ya ugonjwa wa moyo na kifo cha mapema, hawawezi kuthibitisha sababu.

A poached egg on toast

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Choline, which is found in eggs, may protect us against Alzheimer's disease

Uwiano wa hatari

Utafiti wa JAMA ulichakata taarifa kutoka katika majaribio sita yaliyohusisha zaidi ya watu 30,000 katika kipindi cha miaka 17.

Watafiti wamefikia hitimisho kuwa kula miligramu zaidi ya miligramu 300 za kolestro kwa siku kunaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa 17% na vifo vya mapema kwa 18%.

Uwiano huo wa hatari huongezeka zaidi kwenye ulaji wa mayai, na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo kwaulaji wa mayai, na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo kwa 6% na vifo vya mapema kwa 8%.

Two poached eggs with runny yolks

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Egg yolks are an excellent source of lutein, which has been linked to better eyesight

Kwa mujibu wa utafiti huo, madhara hayo ya mayai hayaathiriwi na umri, nguvu ya mwili, matumizi ya tumbaku na historia ya kuwa na shinikizo la damu.

"Utafiti wetu umebaini kuwa, endapo watu wawili watafuata aina moja ya mlo ya aina moja na tofauti pekee ikawa ni ulaji wa mayai, basi yule ambaye mwenye kula mayai mengi anauwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya moyo," anasema Norrina Allen, Profesa mshiriki wa madawa ya kinga katika Chuo Kikuu cha Northwestern University na mwandishi wa utafiti.