Maandamano yafanyika Indonesia kupinga sheria mpya inayodhibiti ngono

Protesters clash with police outside parliament in Jakarta

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamanaji walikabiliana na polisi nje ya bunge la Indonesia katika mji mkuu Jakarta

Polisi wamefyatua gesi za kutoa machozi na maji kwenye makundi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana nje ya bunge la Indonesia juu ya mapendekezo ya sheria mpya ya uhalifu itakayozuwia tendo la ngono kabla ya ndoa.

Maandamano dhidi ya mswada huo pia yalifanyika katika miji mingine nchini humo.

Mswada huo pia unaharamisha kisheria aina nyingi za utoaji mimba na kumtusi rais itakuwa ni kinyume cha sheria.

Mswada huo umekuwa ukicheleweshwa, lakini waandamanaji wanahofu kuwa inaweza hatimae kupitishwa na bunge.

Ni utata gani ulipo ndani ya muswada?

Pendekezo la sheria mpya ya uhalifu inajumuisha yafuatayo;

  • Ngono kabla ya ndoa litakuwa ni kosa la jinai na mhusika anaweza kufungwa mwaka mmoja jela
  • Kuishi pamoja nje ya ndoa inaweza kukusababishia kifungo cha miaka sita jela
  • Kumtukana rais, Makamu wa rais , kiongozi wa kidini, taasisi za serikali na nembo kama vile bendera na wimbo wa taifa itakuwa ni ukiukaji wa sheria
  • Iwapo mtu atatoa mimba atafungwa kifungo cha miaka minne jela iwapo hakutakuwa na sababu za kimatibabu au ubakaji

Awali muswada huo ulipangiwa kupigiwa kura Jumanne- lakini rais Joko Widodo aliahirisha kura hadi Ijumaa, akisema kuwa sheria hiyo mpya inahitaji kuchunguzwa zaidi

Licha ya kucheleweshwa kwa kura hiyo, Waindonesia wengi wanahofia kwamba muswada huo unaweza kupitishwa na bunge na hivyo kuwazuwia ''haki zao''.

Police are seen during clashes outside parliament in Jakarta

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Polisi warushiwa mawe wakajibu kwa gesi za kutoa machozi

Aidha wanahasira juu ya kupitishwa kwa sheria mpya inayodhoofisha mamlaka ya tume ya kupambana na ufisadi , ambayo ni muhimu katika juhudi za kumaliza rushwa.

Na ni ni kilichotoea Jumanne?

Maelfu ya waandamanaji, wengi wao wakiwa ni wanafunzi , waliingia katika mitaa ya miji kote nchini Indonesia kupinga mswada huo.

Makabiliano makubwa zaidi yalikuwa katika mji mkuu Jakarta ambapo waandamanaji walidai kukutana na spika Bambang Soesatyo.

Waandamanaji waliwarushia mawe polisi , ambao walijibu kwa kurusha gesi za kutoa machozi na kuwapiga waandamanaji na maji.

Students tend their injured friends during protests in Jakarta

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanafunzi wakimhudumia rafiki yao aliyejeruhiwa wakati wa maandamano ya Indonesia mjini Jakarta

Moja ya mabango lililobebwa na mwanamke muandamanaji liliandikwa : "Uchi wangu sio mali ya serikali ".

Waandamanaji katika maeneo mengine ,kama vile Yogyakarta na Makassar katika kisiwa cha Sulawesi yaliendelea kwa siku ya pili.

"Tunaenda bungeni kupinga sheria mpya ya shirika la kupambana na rushwa ambazo haziwajali watu bali zinawajali mafisadi ," aliliambia shirika la habari la Reuters Fuad Wahyudin, mwanafunzi wa kuo kiku cha Kiislam katika West Java mwenye umri wa miaka 21.

Zaidi ya polisi 5,000 wameripotiwa kuhusika katika kuimarisha usalama katika mjin mkuu Jakarta.