Je mzozo wa mpaka wa majini baina ya Kenya na Somalia unaelekea kumalizika?

Chanzo cha picha, Villa Somalia
Somalia na Kenya zimekubaliana kufanya kazi pamoja katika juhudi za kuboresha uhusiano baina yao baada ya rais wa Misri Abdelfatah Al Sisi kuwapatanisha Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzke wa Somalia Mohammed Abdullahi Farmaajo wa pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Viongozi hao wameafikiana kuwa watafanya kazi pamoja bila ya kuathiri kesi juu ya mpaka kati ya mataifa hayo mawili inayoendelea katika mahakama ya kimataifa ya haki ICJ.
Somalia ilienda katika mahakama ya ICJ ikitaka mpaka wa baharini kati yake na Kenya kuchorwa upya ili uweze kushuka chini ukipita mpaka wake wa ardhi badala ya kwenda mashariki.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kenya kwa iliishutumu Somalia kwa kuendelea kutangaza mauzo ya mafuta hayo kwa wawekezaji licha ya kwamba eneo hilo bado linazozaniwa.
Imesema kuwa Mogadishu imekuwa ikitumia ramani ambayo inaingilia Himaya ya Kenya.
Hatahivyo Mogadishu imepinga kauli ya kuingilia himaya ya Kenya.
Kenya ilisema kwamba baadhi ya makampuni yameanza kutafuta mafuta katika meneo hayo hayo yanayozozaniwa na mataifa yote mawili.

Chanzo cha picha, Villa Somalia
Tayari kundi moja la wataalam wa baharini nchini Kenya wameiomba serikali kutotumia nguvu na badala yake kutumia diplomasia kwa minajili ya amani katika eneo la magharibi mwa bahari Hindi.
Kundi hilo limesema kwamba iwapo Kenya itapoteza kesi hiyo kwa mahakama hiyo ya kimataifa itasalia nchi isio na bahari na italazimika kuiomba Somalia na Tanzania ruhusa kwa meli zake kuingia katika bahari ya Mombasa.
Hiyo inamaanisha kwamba kesi hiyo itaendelea licha ya Kenya kuendelea kutafuta suluhu nje ya mahakama hiyo.
Nairobi inasema kwamba kesi hiyo haikustahili kuwasilishwa katika mahakama hiyo kwa kuwa kulikuwa na njia mbadala ambazo zilikuwa hazijatumika.













